CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,357
- 6,424
Kwanza Pole na kazi nzuri.
Pili, naomba hili uliweke maanani: Mzazi Mwenzetu Kikwete na mama Salma walikwazika sana kwa jinsi jamii ilivyokuwa ikimjadili mtoto wao aliyekuwa Feza Girls,matokeo hayakuwa mazuri. Sisi kama wazazi tulikwazika sana. Suppose it were your daughter? Put yourself in the shoes of these parents!!!
OMBI: matokeo ya mitihani yatambuliwe kwa namba za watoto tu. After all matokeo ni haki ya mtahiniwa kuyaweka public or not.
Waweke majina au namba sio suluhisho la chochote, eti aibu kuonekana umefeli. Sasa wewe unataka mtu aliyefeli aonekane kuwa kapata div.1 point 7? Eti sababu ni wa rais au sijui ni maarufu kiasi gani? We utakua mjinga ikiwa mtoto wako akifeli unaogopa eti aibu, watu watazungumza. Hakuna mtoto anayependa kufeli, wala hakuna wazazi ambao wangependa mtoto wao afeli.
Kufeli ni matokeo. Kwa wengi wa watoto wetu kufeli ni mazingira mabovu waliyonayo, ona shule za kata. Kwa kesi ya mtoto wa JK sijui tatizo, kwani mazingira yote mazuri ya kumwezesha afaulu alikuwa nayo.
Sasa Ndelichako aseme huyu kapata div.1 wakati ana f4. kwani F4 ni za kina nani? Alafu mnasema rushwa itaisha?
Inafaa wewe uchunguzwe katika eneo lako la kazi, inawezekana ni miongoni mwa wanaokwamisha rushwa isiishe. Maana ungekuwa nafasi ya Ndelichako usingeonesha huyo mtoto kuwa na div.4, na hiyo usingefanya bure.
Wewe matokeo yako yaliwekwaje?
Rafiki hujanielewa. Ninachosema hapa ni usiri. Hata wewe hapo una siri ambazo hutaki watu wazijue. Privacy ya mtu iheshimiwe. Matokeo ya mtu ni haki kuwa siri yake, natural justice dictates that. It should not be for public consumption. Hatusemi abadilishe matokeo, afiche siri za matokeo ya mitihani ya watoto. Ni mazoea ambayo yanakiuka haki za mwanafunzi. najua tumezoea hivyo tangu ukoloni. It is now time to reverse that trend.
Wewe matokeo yako yaliwekwaje?
Tanzania ya watu kama wewe hatufiki popote.
Na je yangekua mazuri yatangazwe? au kwa sababu ni matokeo mabaya watanzania tufikie mahali tukubali ukweli,kuficha ficha vitu vingine ndio vinaleta mauchakachuaji.
watanzania hatuwezi kuendelea kwa sababu hatutaki kuambiwa ukweli majina yaendelee kama kawaida.
Dr Ndalichako ebu fikiria suala la sms mtandao, watahiniwa watakiwe kuandika namba zao za simu ambazo zitaingizwa kwenye database na kuconnect na server ya baraza matokeo yakitoka tu automatically yanamfikia mlengwa. ingawa kwa vijijini bado safari ni ndefu kwa huduma hii. check if possible