ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Mamsapu analia ana lalamika,
Mama Mzazi ametutembelea nyumbani. Majuzi wakati alipokaribishwa chakula cha jioni mezani ma mamsapu (mai waifu wangu) , mama alimuuliza mamsapu kama kaniwekea na mimi ile mboga ambayo walikuwa wanakula na chakula (sikuwepo nyumbani wakati huo kutokana na mihangaiko yangu). Mamsapu akamtania kuwa "hajaweka" akidhani mama hayupo "serious" .
Jana nilichelewa pia kurejea, lakini cha ajabu nilipofika nyumbani sikukuta mtu sebuleni (sitting room), nilipoingia chumbani, nikamkuta mamsapu akiwa amelala kajifunika gumbi gu,mbi, nikamfunia na kuuliza "vipi unaumwa??" akasema hapana, sikujali, nikarejea mezani kupata chakula, wakati nikijiandaa kula, mara mama akatoka chumbani kwake akiwa na bakuli mkoni, akaweka mezani na kuniita kwa jina langu na kuniambia kwa kilungha..."nimekuwekea hii.....akinionyesha kipaja cha kuku!!" Napo sikujali, nikamjibu tu "Asenti...!!" akatabasamu. Nikamuuliza kwani nyini wenyewew mshakula..akajibu ndio. Sikuwa na neno zaidi nikaendelea kula huku yeye akiwa amekaa pembeni yangu...mara nikasikia mlango wa chumbani kwetu unafunguliwa ..mamsapu akatoka na kuchukungula kidogo kisha akaingiza tena shingo ndani na kufunga mlango na kutoa mgumo "Mh...!!".
Mama akaniaga, naenda kulala ..nikamruhusu ..lakini alipokuwa akiondoka akasema kwa kilugha tena .."jana hawakukuwekea hiyo mboga tulikula sisi nikaona leo nikununulie mwanangu..." nikajibu tu sawa asante...
Mie na Mamsapu wangu hatutoki kabila moja hivyo hatuelewani pale mtu wa kwetu akiongea kikabila , niliporejea chumbani tena nikamkuta Ma msapu kakaa kitandani huku kashika tama na machozi yanamtiririka...nikamuuliza nini..akang'aka, "Naona mama yako leo ameamua kukufichia mboga??" haya bwana..lakini naona amenidharau sana!!!" sikuelewa, akanieleza yaliyotokea jana yake na siku hiyo, kumbe mama alimtuma mjukuu wake (mwanangu) klwenda kununua hicho kipaja cha kuku lakini hata mwenyewe hakula akaweka chiumbani kunusubiri..kabala mamsapu alimuulizaz akajibu amenitunzia mimi wamanae kwa kuwa jana walininyima nyama (kuku)...Ma msapu kakasirika sana anahisi ahaminiki na mama yangu, .Sielewi kama mapenzi haya ya mama kwa mwanae (mimi) ni mapenzi ya kujenga au kubomoa!! ..sijui wanaume wenzangu mna uzoefu gani na wazazi wenu wa kike, rafiki yangu mmoja kaniambia mama yake mzazi alikuwa halali jamaa akiwa hajarejea kwenye mihangaiko, atakaa sebuleni weee mpaka asikie mwanae ameingia ndani, amekula ndipo nae anyanyuke kwenye kochi sebuleni kwenda chumbani....Mwingine anasema eti hata hawa wake zetu nao wanawapenda zaidi kaka zao kuliko sie waume zao, na wakizeeka, watawapenda zaidi watoto wao wa kiume kuliko wakwe zao....