Mama Kanumba kumtembelea Lulu gerezani

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598


Frola Mtegoa.

MAMA wa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Frola Mtegoa amesema kuwa, kutokana na matatizo yaliyompata staa wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili, amekuwa akimuonea huruma na anajipanga kumtembelea gerezani.

Akipiga stori na Ijumaa, Mtegoa alisema watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa ana chuki na Lulu, lakini moyo wake unampenda na kama isingekuwa sheria kuhitaji Lulu kufungwa basi yeye asingekuwa na tatizo naye.



Staa wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’

“Sina chuki na Lulu, tulikuwa karibu lakini nafikiri watu wake wanaozunguka ndiyo waliosababisha ukaribu wetu kuparanganyika. “Lakini moyoni ninampenda na kiimani mimi ni Mkristo.

Kwa hiyo siwezi kufurahi kuona mwenzangu anapata matatizo, ipo siku nitamtembelea gerezani!” alisema mama huyo.


Muungwana
 
Huyu kweli anataka kumtembelea Mahakamani na si Gerezani!!!
 
Baada ya kuona jamii imemtoa thamani ndio anaongea upuuzi huo? Atulie aendelee na shughuli zake, amesahau aliongea nini siku ile mahakamani baada ya hukumu?
 
Maneno ya kinafiki.
Yanapingana na maneno yake mwenyewe kwa wanahabari mara baada ya hukumu ya Lulu kufungwa.
 
anatafuta tu kiki anajua kupitia jina la lulu ataendelea kuwa relevant kwenye jamii.
 

Kweli hata mie naona. Ila ni vitu vipo damuni hivi maana ni mama wa aliyekuwa "muigizaji" mkubwa tu na yeye mama amesha-cast kwenye movie kadhaa, hashindwi kuigiza kidogo kwenye hili.
 
Inawezekana alikua tayari kashakula mibia .akili za pombe sometime zinatoa ya moyoni halisi kabisa
 
Mara alisema haki imepatikana, mara alisema lulu atarudi ila kanumba harudi na anaenda makaburini kumtembelea kanumba.
Mama atulie na lulu alitumia busara kutotaka kukata rufaa ili atumikie adhabu iishe salama salini akitoka hana deni kwa mtu yoyote.
Maana angeshinda rufaa bado kungekuwepo maneno maneno
 
Akipiga stori na Ijumaa, Mtegoa alisema watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa ana chuki na Lulu, lakini moyo wake unampenda na kama isingekuwa sheria kuhitaji Lulu kufungwa basi yeye asingekuwa na tatizo naye.
Huyu Mama mnafiki kweli....hivi si ndo yeye alikuwa akitokwa machozi debe huku akimshukuru Mungu kuwa Haki imetendeka baada ya Lulu kuhukumiwa
 
Hivi ameamua kutokata rufaa ? ....akikata rufaa ni sawa na kukalia kuti kavu !
 
Broo yangu mtoa post ishu ya kanumba na Lulu imenichosha , binafsi nikikuta ishu zao inaniboa mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…