"Mama kuwa na umri zaidi ya miaka 35 au Baba kuwa na miaka zaidi ya 40 kunaweza kupelekea kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo, kupata infection wakati wa ujauzito, Mama mjamzito kuumia sababu zipo nyingi ambazo zinapeleka mtoto kuzaliwa na mtindio wa ubongo" Dkt. Alvin Miranda.
vijana wenye malengo ya kupata watoto, jitahidi uzae ukiwa under 35
vijana wenye malengo ya kupata watoto, jitahidi uzae ukiwa under 35
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa Mayo Clinic ya nchini Marekani Utindio wa ubongo ni hali ambayo huathiri mwili wa binadamu kuwa na uwezo wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine pamoja ambapo baddhi ya watu wenye utindio wa ubongo huweza kutembea lakini wengine huhitaji msaada lakini pia uwezo wa kusimama na kukaa (movement and posture) ikisababishwa na kuharibiwa kwa ubongo unaoendelea kukua hasa wakati mtoto akiwa bado hajazaliwa.
Dalili zinazoweza kuonekana kwa mtu mwenye utindio wa ubongo ni pamoja na kupata changamoto wakati wa kula, kuongea, ukuaji, kusikia, afya ya akili, kuhisi na kadhalika. Inashauriwa kumuona daktari mara baada ya kubaini dalili kama hizi kwa mtoto kwa ajili ya msaada zaidi.
Kumekuwepo na taarifa mtandaoni inayosema iwapo mtoto akizaliwa na wazazi wenye umri wa miaka 35 na zaidi huweza kusababisha utindio wa ubongo kwa mtoto atakayezaliwa.
Uhalisia wa taarifa hiyo upoje?
JamiiCheck imepitia tafiti mbalimbali na kubaini kuwa upo uwezekano wa kuongezeka kwa hatari ya watoto kuzaliwa na utindio wa ubongo kwa wazazi wenye umri wa miaka 35 na zaidi lakini pia wazazi wenye umri chini ya miaka 20.
Utafiti uliochapishwa katika tovuti ya National Library of Medicine ya nchini Marekani unaeleza kuwa kati ya watoto 1391 wenye utindio wa ubongo waliohusika katika utafiti huo ulibaini kuwa kati yao asilimia 19% mama zao walikuwa ni wenye umri wa miaka 35 na zaidi huku asilimia nne 4% ni watoto ambao mama zao walikuwa chini ya umri wa miaka 20.
Aidha umri wa mzazi wa kiume pia unaweza kuwa na athari kwa mtoto kwani katika utafiti mwingine tovuti ya National Library of Medicine inasema mzazi wa kiume mwenye umri wa kuanzia miaka 40 wanahusishwa na kuongezeka kwa uwezekano kwa mtoto kuzaliwa na utindio wa ubongo huku ukiongeza kuwa watoto ambao huzaliwa na akina mama walio na umri chini ya miaka 20 au zaidi ya 35 wapo hatarini kupatwa na utindio wa ubongo ikilinganishwa na akina mama walio kwenye umri kati ya 25 hadi 29.
Kadhalika mtoto kuzaliwa kabla ya wakati mfano kabla ya wiki ya 37 ya ujauzito huweza kumsababishia mtoto utindio wa ubongo kwani mtoto anakuwa bado hajaimarika vizuri kuishi baada ya kuzaliwa na hivyo kuwa katika hatari ya ubongo kuharibiwa.
Wazazi wenye umri chini ya miaka 20 pamoja na wazazi wenye umri wa miaka 35 na zaidi huwa na hatari ya kujifungua watoto wenye utindio wa ubongo kwa sababu umri wao huongeza uwezekano wa kutokea changamoto ambazo huchangia kupatwa kwa utindio wa ubongo kwa mtoto, mfano katika umri wa chini ya miaka 20 kuna uwezekano wa mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, kupanda kwa presha wakati wa ujauzito (preeclampsia), anemia, Genetic mutations yaani mabadiliko katika mfuatano wa DNA na kadhalika.