Mama, "Kwani si tunaalika watu kuhalalisha hilo hilo (tendo la Ndowa)"


Inawezekana labda wewe hujanielewa! Unapoulaumu mfumo dume ( kuwa mwanamke analaaniwa kuchupachupa na mwanammeanasifiwa) huku hujuwi kuwa pengine kwa hili la kuchupachupa hata wanawake wenyewe hawalipendi. Na ndio maana nikakwambia ulishawahi kufanya utafiti kujuwa kuwa hili la wanawake kuchupachupa nao wanataka waitwe"Vikike" kama wanavyoitwa wanaume vidume?
 

ukisema "stable relations out of marriage lazima itakuwa na flaws chungu mzima, tayari umeshaji contradict.

Halafu "stable marriage nje ya ndowa" ni kitu gani?

Bottom line, kuna mapenzi yanayostawi nje na ndani ya ndoa, ndoa si kitu kibaya wala kizuri. Kama unaweza kustawisha mapenzi bila ndoa, ndoa si lazima.

Kuna watu wamekaa bila ndoa miaka kibao, wameishi vizuri tu. Kwa pressure wakaamua kuoana, baada ya kuoana wamedumu miaka miwili tu.Talaka.

ndoa ni kama kukaa ndani ya nyumba mliyofungiwa. Hamuwezi kutoka mpaka mvunje milango (talaka) jambo ambalo litaleta kelele na bughudha (aibu kwa jamii, bado tuna stigmatize talaka). Kwa hiyo hata hao wanaodumu katika ndoa hatujui kama wanadumu kwa mapenzi ya kweli au kwa sababu wanakwepa aibu tu ya kuachana.

Watu wanaoamua kukaa wenyewe kwa kuelewana bila ndoa wanaweza kusema wanapendana kikweli bila kushurutishwa na ndoa. Ni kama watu walioamua kukaa pamoja ndani ya nyumba huku milango ikiwa wazi. kila mmoja ana uwezo wa kuondoka bila kuvunja mlango, lakini haamui kufanya hivyo kwa sababu anapenda kuwa pamoja na mwenzake.
 

Una introduce kitu kigeni kabisa ambacho mie sijakiongelea halafu unakiunganisha tu kama vile nimesema kwamba wanawake wanapenda kuchupachupa.

Mie sijasema kwamba wanawake wanapenda kuchupachupa, nimesema mfumodume unasifia wanaume kuchupachupa (urijali, kiwembe etc) lakini hapo hapo unadharau umalaya huo huo kwa mwanamke (mama huruma, jamvi la wageni etc)

Mtu akiisema hii double standard ya mfumodume hamaanishi kwamba wanawake wanao"chupachupa" wanapenda kufanya hivyo.

Hii kilatini inaitwa "Non sequitur", it does not follow, umeunganisha vitu viwili ambavyo havina uhusiano, out of nowhere.
 
Nakubaliana nawe,ila nilichotaka kusema hapa ni kwamba unapoupa ujinga huu jina la mfumo dume naona kama unauvika nguo vile,kama umenielewa!

Mfumodume haiwezi kuwa nguo, mfumo dume ni expose. A derogatory name ona apar with ubeberu.

Mfumodume ni ujinga, wewe umekubali kwamba huu ni ujinga, kwa nini kuuita ujinga huu (common name) exacting name hiyo ya "mfumodume" kuwe kuuvika nguo ujinga huu?

Kwangu mimi ni kuuvua nguo zaidi, kwa sababu nimekuwa specific, nimeeleza aina gani ya ujinga.
 

Ndugu yangu tunanapokuwemo ndani ya jamii huwa tunafuata mambo ya kijamii na hilo ndilo lilopo ulimwengu mzima. Kama utataka utuletee mila za wenyeji wako tutapata shida kwani wengi wa waliomo humu wapo nchi tofauti.
Hebu turudi humu ndani ya jamii yetu na kuangalia jee hawa wanawake wana msimamo gani kuhusu huo unaoiita kuonewa kwa kuitwa malaya.

Halafu mbona kuna jammii ambazo wanawake wanaowa na jee mfumo huo na huu wa kawaida wa wanawake kuolewa unahisi upi unampa hadhi zaidi mwanamke?
 
Mi nadhani,kwa mtazamo wangu,hatujui ndoa ni nini,tafsiri mbovu za kidini ndo zinaleta shida hapa.Kukifuata kitu kimkumbo ni tatizo kubwa.Niliwahi kuanzisha mada siku moja hapa nikitaka kila mmoja aeleze ndoa ni nini,majibu yaliyotoka yanachekesha.Watu wanafungwa na dhana zaidi kuliko kitu halisi.Umapokuwa kwenye mahusiano nje ya ndoa mnaishi muda mrefu kwa sababu mnajiongoza wenyewe,kwenye ndoa tatizo mnataka muongozwe na dhana zaidi ya nyie wenyewe.Ndo maana mtu anakua mwaminifu nje ya ndoa,akiingia kwenye ndoa mambo yanabadilika!
 
Kiranga,ninaposema kuuvika nguo simaanishi nguo as nguo,ninamaanisha kuwa unaposema mfumo dume linakua kama neno jepesi haliendani na kiwango cha ujinga.Yani mfumo dume sio neno lenye uzito wa kutosha!
 

Ungetaka kuishi kama jamii static usingekuwa kwenye internet sasa hivi wewe, kwani jamii yetu ndiyo iliyovumbua umeme, computer na internet?

Swala si jambo limeanzia wapi, swala ni je, linafaa au halifai?

Hizi habari za kutukuza sana a failing othodoxy zinatufaa au hazitufai?

Utakuta mtu kwao masikini hajiwezi hali wala mali, na yeye anachangisha masikini wenzake kibaooo wenye majukumu kemkem, bora hata kama angekuwa anawachangisha kujenga nyumba tungejua anafanya la maana.

Kumbe muharusi mkuuubwa.

Halafu baada ya harusi wanaingia kwenye chumba cha kupanga, hata zawadi walizonunuliwa hawana pa kuziweka.

Baada ya miaka miwili talaka.

Hivyo hiyo akili?

Kati ya huyo na anayefuatisha mapenzi ya kweli yasiyo na kelele za miharusi wala ndoa za kuapishana nani afadhali?
 
Kiranga,ninaposema kuuvika nguo simaanishi nguo as nguo,ninamaanisha kuwa unaposema mfumo dume linakua kama neno jepesi haliendani na kiwango cha ujinga.Yani mfumo dume sio neno lenye uzito wa kutosha!

Hapana,

Ujinga si neno lenye uzito wa kutosha. Mtu anaweza kuwa mjinga kwa kukosa kujua (ignorance), hakuna element ya ubeberu hapa. Huyu mjinga tu, tatizo lake hajui, akielimika ataacha.Hana nia ya kumkandamiza mwanamke, ni ujinga tu ndio unamfanya afanye anavyofanya. Akielewa umuhimu wa mwanamke ataacha.

Mfumodume ni zaidi ya ujinga huu wa kutojua. Mfumo dume ni mfumo, unasukwa na kulelewa. Ni pale mtu msomi wa sheria aliyefundishwa chuoni umuhimu wa kupanga maneno vizuri mpaka kiwango cha kuandika contract, kama ex-Speaker Pius Msekwa anaposema "acheni wivu wa kike". Maana yake mtu amefuta ujinga, lakini ndani kabisa ya mawazo yake anaamini kwamba wivu ni kitu cha kike. Kwamba wanaume wako juu ya wanawake katika hili.

Utaona kwamba mfumodume ni kashfa nzito zaidi ya ujinga, kwa sababu unabeba ubeberu fulani hivi wa kutaka kumkandamiza mwanamke kwa mambo yasiyo na msingi na outdated tradition.

Lakini ujinga tu unaweza kuwa excusable, kwa sababu mtu anaweza kuwa mjinga kwa kukosa kujua right from wrong.
 
Reactions: Obe
Kiranga thanx,labda ni kwa sababu nimelisikia sana ndo maana nakua kama nimelizoea.NIMEKUELEWA na nimekubaliana nawe!Labda tujadili huo mfumo dume.Hivi mfumo dume ni nini?
 
Kiranga thanx,labda ni kwa sababu nimelisikia sana ndo maana nakua kama nimelizoea.NIMEKUELEWA na nimekubaliana nawe!Labda tujadili huo mfumo dume.Hivi mfumo dume ni nini?

kutumia shorthand ya translation kutoka kwa jamii zilizoanza kutambua haya mambo kipindi, katika kiingereza mfumodume mara nyingi unaitwa "Chauvinism", "maleChauvinism" to be exact.Kwa sababu siku hizi wanawake nao kuna wengine wanakuja na sexist notions za "female Chauvinism" - not to be confused with feminism- kwamba "wanawake ni zaidi ya wanaume.

Kwa kifupi sana ni mfumo unaoaminisha watu kwamba mwanamme ni bora kuliko mwanamke.

kwa hiyo ukiona mwanamke hawezi kuoa (active) anaweza kuolewa tu (passive) katika Kiswahili, unaona kwamba utamaduni wetu umejengeka katika mfumodume.Kwamba mwanamke si mtu wa kufanya, ni wa kufanyiwa tu.

ndiyo maana watoto wa kike wengi wanakoseshwa kusomeshwa, wanaandaliwa kuolewa tu.
 
Kiranga,unamwaminisha ni bora kwenye nini?
 
Yaani huo mfumo unamwaminhsha nani kuwa mwanaume ni bora?Na huyo mwanaume ni bora kwenye nini?

Unaiaminisha jamii nzima.

Take ndoa for example. Ndoa ni kitu so central katika jamii kiasi cha kwamba ninavyokuja hapa kui-deconstruct watu wengine wanapata pause. Wanasema Astaghafirullah huyu Kiranga.

Lakini ukiangalia ninayoyasema yana ukweli. Ndoa ni stage ambayo katika utamaduni wetu wote tunategemewa kupita, ukishafikisha thirties tu watu wanaanza kukuzonga, harusi lini, wifi yetu yuko wapi, tunataka mjukuu etc.

Lakini ndoa yenyewe kiswahili mwanamme anaoa, mwanamke anaolewa.Na kiswahili hata kama mwanamke kachoka anataka kujitoa, hawezi kum divorce mume, inabidi amuombe mume amdivorce yeye mke.

Huo ndio mfumodume, umekaa katikati ya jamii yetu hata tunaposema "anaoa" na "anaolewa" hatujui kwamba ni mfumodume.

kwa hiyo, unamwaminisha nani? Jamii nzima. Unaiaminisha jamii kwamba mwanamme ni bora katika nini? Practiocally mambo yote ukiondoa mambo ya kike kama urembo, kuzaa, kulea watoto, kupika, umbea na mengine "ya kike kike" kama hayo.
 
Possibility ya huyo binti kuolewa na huyo kijana ni ndogo sana.
 
not to derail the original topic.

My sense is, huyu mama kauliza swali lililo so central katika kupata a paradigm shift katika jamii yetu.

Kwa nini tunakuwa so obsessed over sexual chastity kabla ya ceremony ya harusi/ndoa halafu tukishaihalalisha kwa misherehe inakuwa si big deal?

Watu wazima wawili wakipendana kwa kweli, what's the big deal about misherehe na other farcical extravagances?
 
Possibility ya huyo binti kuolewa na huyo kijana ni ndogo sana.

1. Kuolewa ni nini?
2. Una hakika huyo binti anataka kuolewa? dada zetu wa siku hizi nao hawa wengine washaona future ipo katika chuo na career, akiolewa mume ndio kalelewa kwenye mfumodume atataka kumsimamisha ambitions zake za chuo na career, kwa nini unafikiri kila mwanamke anataka kutakiwa kuolewa kwa sana tu?
 
Kamchumbia wa nini? Mie nilidhani uchumba maanake yake, maandalizi ya kuja kukuoa,au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…