Kiranga nimekuelewa,kuhusu neno "kuoa" au "kuolewa" wewe unalitafsiri vipi?Kuhusu mwanamke kutokuacha nafikiri hiyo inatokana na imani fulani,sidhani kama tunaweza lizungumzia hapa.Hayo maneno ya kiswahili bado sijaona ubaya wake,tatizo tunayachukulia kutokana na dhana ya mwanamke kutokutoa talaka ambayo kama nilivyosema ni dhana ya imani fulani tena moja tu.Kwenye mfumo dume hapo napo kuna mkanganyiko.Mwanaume na mambo ya kiume.Mwanamke na mambo ya kike.Tukubali kuwa mwanamke anapoambiwa "acha kufanya mambo ya kiume" ni sifa?Sidhani,pia mwanaume anapoambiwa acha mambo ya kike,sio aibu.Unapoyataja mambo ya kikekike wewe ndie unaamua yawe tusi,kashfa au vinginevyo.Tafsiri iliyoko kichwani mwako.Lakini pia huu mfumo unaoitwa dume una mambo mengi lakini mengi zaidi yapo vichwani mwetu zaidi,sio halisi!
habari nzima ya "kuoa" na "kuolewa" ni medieval, smacks of slavery, ownership and territory marking as if we are still hunter gatherers.
Mwanamke kutokuacha inatokana na imani fulani damn right, imani hiyo ni mfumodume, kwamba mwanamke anaachwa tu, hawezi kuacha kwa sababu anaolewa tu, hawezi kuoa. Ndiyo maana nikatoa mfano wa kiswahili, mwanamke hawezi kuoa, anaolewa tu. Hujaona ubaya wa lugha kutowapa usawa katika ndoa mwanamke na mwanamme, then mfumodume umeshameza thought process yako.
Hakuna mambo yasiyo na msingi wa kibaiolojia yaliyo ya kiume au ya kike.
Mwanamke anapoambiwa "acha kufanya mambo ya kiume" unakusudia mambo gani? Maana usitake kuniuliza swali lisilo specicif na linaloweza kubeba tani za vijimambo tofauti kiasi cha kunifunga kukubali nisichokijuua. be specific, nipe mfano, mambo gani ya kiume? Mie nishatoa mfano specific hapo juu. Ex-Speaker Msekwa aliposema "acheni wivu wa kike" hakuwatendea haki wanawake, aliongea kimfumodume kwa kutumia imani ya kwamba tabia ya wivu ni domain ya wanawake, wakati tunajua otherwise.
Issue si kwamba "mwanamme anapoambiwa aache kufanya mambo ya kike" ni aibu au si aibu, issue ni, mambo gani unaona ni ya kike? Mwanamme anayeomba msaada wa hisabati anafanya mambo ya kike kwa sababu wanawake ndio hawajui hisabati? Mwanamme mwenye wivu anafanya mambo ya kike kwa sababu wivu ni jambo la kike? Mwanamme anayependa kupika anafanya mambo ya kike kwa sababu kupika ni jambo la kike? Mwanamme anayependa kucheza na watoto anafanya mambo ya kike kwa sababu kucheza na watoto ni jambo la kike?
Mie sijayataja mambo ya kike, nimekutolea mfano wa Msekwa aliyesema "acheni wivu wa kike" akimaanisha kwamba wivu ni tabia ya kike na wananume wenzie waliomkashifu hawatakiwi kuwa na wivu.
Kuhusu mfumodume kuwa na mambo mengi vichwani mwetu, lakini yasiwe halisi, umeshindwa kujenga hoja kwa mifano, umetoa a blanket statement tu. Jaribu kunithibitishia kwa mifano kwa nini unaamini hivyo.
Mie nimekuonyesha jinsi gani mfumodume ulivyo katikati ya jamii yetu. upo katika taasisi inayoheshimika sana katika jamii. Ndoa.mpaka l;ugha ya ndoa ina mfumodume.Lugha ina tabia ya kuonyesha jinsi jamii nzima inavyofikiri.
Ukiona lugha inafanya mwanamke kuwa passive katika ndoa, na mwanamme kuwa active, ujue mfumodume upo katika ndoa. Mwanamke anatakiwa kusema hewala bwana hata akizabwa kibao.
Tutaweza kuwalaumu dada zetu wasipotaka kuolewa?