jamani huyu mama ni mara chache anaongelewa, sina hakika ila niko tayari kukosolewa. Nadhani huyu mama si wakuwekwa kwenye kundi la mafisadi. Amekuwa naibu waziri kwa muda mrefu na pengine kuliko wote tulo nao. Sasa wanajamvi mnamwonaje. Narudia tena nadhani sio fisadi na kama nimekosea niko tayari kukosolewa!
kampuni mpya ya ndege...mama maua daftari umo?
pakajimmy22nd january 2010, 01:19 pm
kuna kampuni mpya ya ndege inaitwa air zara international!
jumapili 17/1/2010 walizindua rasmi safari za arusha, wakiwa wameandamana na waandishi wa habari kibao toka dar.
na watu kama mimi tukazipata habari hizo, tukaenda kufuatilia.
katika msafara huo wa uzinduzi, mkuu wa msafara wa uzinduzi alikuwa naibu waziri wa miundombinu, maua daftari.
mama huyu hakujivunga pale, akatuomba tuliokuwepo pale tusaidiane kutafuta wateja ili kuiungisha kampuni hiyo mpya.
jumatatu, waziri huyo alikuja tena arusha, akaongelea ndege hiyohiyo, kuwa itakuja tena alhamisi na kumchukua yeye na abiria wengine.
alhamisi, wanafamilia wa huyu mama walisafiri na ndege hii jioni.
kuna tetesi kwamba mama huyu ana hisa katika kampuni hii kutokana na ukaribu wake na uongozi wa ndege hii, na kufikia hatua ya kuipigia debe bila woga!
hongera mama kama ni kweli. Kilimo kwanza bana, kwani nini!
Hapana best simsafishi sikujua kuwa naye yumo kweli nimeamini kimya kingi....
sasa hii sirikali ya ccm kuna mzima kweli?