Makala hii imeletwa kwako na AFYA ZAIDI CONSULTANTS, Wataalam na washauri wa afya na vipodozi. Kwa elimu na ushauri zaidi tafadhali tembelea website yaowww.afyazaidi.org
Kuwa mjamzito ni kitu cha furaha sana kwa wengi. Ni mafanikio. Huongeza upendo na furaha. Kwa wachache huwa ni kama ajali. Na hupatwa na huzuni. Tofauti hizi hutokana na mipango ya wanawake hao, hali zao za kimaisha na maandalizi yao.
Baada ya kupata ujauzito kazi kubwa iliyopo mbele ni kulea vizuri ujauzito huo hadi kujifungua mtoto mng’aa! mng’aa! mng’aa…… Unaleaje vizuri ujauzito wako? Mambo gani huhatarisha afya yako na mtoto aliyepo tumboni?
MAMBO YA KUFANYA
Mwanamama mjamzito pamoja na mwanaume wake ni lazima wahakikishe afya njema ya mama na mtoto aliyepo tumboni kipindi chote cha ujauzito. Hii ni kwa siku nzima na kwa siku zote za ujauzito. Wahakikishe mazingira mazuri kwa mama mjamzito na mtindo mzuri wa maisha ili awe na afya njema.
Mama mjamzito afanye mambo yafuatayo:
Tunakutakia afya njema!

- Kuanza kliniki na kuhudhuria kila mwezi bila kukosa
- Kupata elimu na ushauri wa mambo yanayotokea wakati wa ujauzito
- Jua dalili zote za hatari wakati wa ujauzito, tahadhari za kuchukua na mahali pa kwenda kupata msaada
- Kuwa na bajeti ya malezi ya ujauzito na dharura yoyote inayoweza kujitokeza
- Kula chakula bora na kwa mtindo mzuri
- Kunywa maji ya kutosha, kula matunda mengi na kula sana mboga za majani
- Fanya mazoezi ya kutosha na ushughulishe mwili wako
- Kupumzika kiasi cha kutosha – Lala angalau masaa 8 usiku na masaa 4 mchana
- Kujiburudisha na kujifurahisha kiasi cha kutosha kila siku, siku nzima
- Kuwa msafi mara zote. Hakikisha mazingira yote, vyombo vyote, nguo zote na mwili wote ni safi
- Jikinge dhidi ya magonjwa yote – Ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa
- Tumia dawa zote vizuri kama ulivyoelekezwa na daktari, famasi na nesi
- Hakikisha usalama mara zote. Hakikisha mazingira yote, vyombo vyote, nguo zote na viatu vyote ni salama
- Kuwa makini zaidi na kemikali zote – Dawa, vipodozi, vyakula vya kutoka kiwandani, dawa za kuua wadudu, rangi za kupaka nyumba nk – Pata ushauri kutoka kwa wataalam wa afya. Mara zote uliza kama hazitakudhuru au kumdhuru mtoto aliyepo tumboni
- Fanya uchunguzi wa mara kwa mara na pata matibabu mazuri na kwa wakati
- Jua siku unazotarajia kujifungua. Kisha jiandae vizuri, angalau mwezi mmoja kabla. Fika mapema hospitali ambayo umepangiwa kujifungulia
- Epuka/Acha kabisa kuvuta sigara, kunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya
- Acha kabisa matumizi mabaya ya dawa, dawa zisizoruhusiwa kwa wajawazito na vipodozi visivyo salama
- Acha kuvaa nguo za kubana na viatu vyenye visigino virefu
- Usifanye kazi ngumu
- Usiwe na msongo wa mawazo. Waza vizuri bila kuwa na simanzi, msongo na uchungu
- Epuka kukasirika mara kwa mara. JHakikisha unakuwa na furaha na amani mara kwa mara
- Epuka jua kali, vumbi, wanyama wafugwao nyumbani na mabanda yao
- Epuka vyakula visivyopikwa na kuiva vizuri. Vinaweza kukusababishia magonjwa
- Epuka kula sana na kulala sana. Kula kiasi sahihi na jishughulishe vya kutosha
- Epuka ugomvi na ajali
- Usiwe msiri kwa wataalam wa afya. Toa taarifa na maelezo ya kutosha ili usaidiwe vizuri
- Epuka kujifungulia nyumbani au sehemu pasipo na wataalam. Jitahidi siku zikikaribia kuwa karibu na hospitali uliyopangiwa kujifungulia, na kuwa na uhakika wa usafiri wa kukuwahisha muda wowote ukihisi dalili
Tunakutakia afya njema!