Mama mjamzito : mambo ya kufanya na mambo ya kuepuka kufanya

ELAFU

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
410
Reaction score
150
Makala hii imeletwa kwako na AFYA ZAIDI CONSULTANTS, Wataalam na washauri wa afya na vipodozi. Kwa elimu na ushauri zaidi tafadhali tembelea website yaowww.afyazaidi.org



Kuwa mjamzito ni kitu cha furaha sana kwa wengi. Ni mafanikio. Huongeza upendo na furaha. Kwa wachache huwa ni kama ajali. Na hupatwa na huzuni. Tofauti hizi hutokana na mipango ya wanawake hao, hali zao za kimaisha na maandalizi yao.

Baada ya kupata ujauzito kazi kubwa iliyopo mbele ni kulea vizuri ujauzito huo hadi kujifungua mtoto mng’aa! mng’aa! mng’aa…… Unaleaje vizuri ujauzito wako? Mambo gani huhatarisha afya yako na mtoto aliyepo tumboni?

MAMBO YA KUFANYA
Mwanamama mjamzito pamoja na mwanaume wake ni lazima wahakikishe afya njema ya mama na mtoto aliyepo tumboni kipindi chote cha ujauzito. Hii ni kwa siku nzima na kwa siku zote za ujauzito. Wahakikishe mazingira mazuri kwa mama mjamzito na mtindo mzuri wa maisha ili awe na afya njema.

Mama mjamzito afanye mambo yafuatayo:
  1. Kuanza kliniki na kuhudhuria kila mwezi bila kukosa
  2. Kupata elimu na ushauri wa mambo yanayotokea wakati wa ujauzito
  3. Jua dalili zote za hatari wakati wa ujauzito, tahadhari za kuchukua na mahali pa kwenda kupata msaada
  4. Kuwa na bajeti ya malezi ya ujauzito na dharura yoyote inayoweza kujitokeza
  5. Kula chakula bora na kwa mtindo mzuri
  6. Kunywa maji ya kutosha, kula matunda mengi na kula sana mboga za majani
  7. Fanya mazoezi ya kutosha na ushughulishe mwili wako
  8. Kupumzika kiasi cha kutosha – Lala angalau masaa 8 usiku na masaa 4 mchana
  9. Kujiburudisha na kujifurahisha kiasi cha kutosha kila siku, siku nzima
  10. Kuwa msafi mara zote. Hakikisha mazingira yote, vyombo vyote, nguo zote na mwili wote ni safi
  11. Jikinge dhidi ya magonjwa yote – Ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa
  12. Tumia dawa zote vizuri kama ulivyoelekezwa na daktari, famasi na nesi
  13. Hakikisha usalama mara zote. Hakikisha mazingira yote, vyombo vyote, nguo zote na viatu vyote ni salama
  14. Kuwa makini zaidi na kemikali zote – Dawa, vipodozi, vyakula vya kutoka kiwandani, dawa za kuua wadudu, rangi za kupaka nyumba nk – Pata ushauri kutoka kwa wataalam wa afya. Mara zote uliza kama hazitakudhuru au kumdhuru mtoto aliyepo tumboni
  15. Fanya uchunguzi wa mara kwa mara na pata matibabu mazuri na kwa wakati
  16. Jua siku unazotarajia kujifungua. Kisha jiandae vizuri, angalau mwezi mmoja kabla. Fika mapema hospitali ambayo umepangiwa kujifungulia
MAMBO YA KUEPUKA NA KUACHA KABISA
  1. Epuka/Acha kabisa kuvuta sigara, kunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya
  2. Acha kabisa matumizi mabaya ya dawa, dawa zisizoruhusiwa kwa wajawazito na vipodozi visivyo salama
  3. Acha kuvaa nguo za kubana na viatu vyenye visigino virefu
  4. Usifanye kazi ngumu
  5. Usiwe na msongo wa mawazo. Waza vizuri bila kuwa na simanzi, msongo na uchungu
  6. Epuka kukasirika mara kwa mara. JHakikisha unakuwa na furaha na amani mara kwa mara
  7. Epuka jua kali, vumbi, wanyama wafugwao nyumbani na mabanda yao
  8. Epuka vyakula visivyopikwa na kuiva vizuri. Vinaweza kukusababishia magonjwa
  9. Epuka kula sana na kulala sana. Kula kiasi sahihi na jishughulishe vya kutosha
  10. Epuka ugomvi na ajali
  11. Usiwe msiri kwa wataalam wa afya. Toa taarifa na maelezo ya kutosha ili usaidiwe vizuri
  12. Epuka kujifungulia nyumbani au sehemu pasipo na wataalam. Jitahidi siku zikikaribia kuwa karibu na hospitali uliyopangiwa kujifungulia, na kuwa na uhakika wa usafiri wa kukuwahisha muda wowote ukihisi dalili
Ukizingatia somo hili pamoja na mengineyo utaishi vizuri na utajifungua salama, mtoto mzuri akiwa na afya njema. Endelea kupata elimu na ushauri kutoka kwetu na wataalam wengine wa afya ili uwe salama zaidi siku zote.

Tunakutakia afya njema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…