mama mjamzto

mbugi2013

Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
39
Reaction score
4
mama mjamzito miez 5 akijiskia maumivu chn ya kitovu mara kwa mara,tatzo nn.
 
mama mjamzito miez 5 akijiskia maumivu chn ya kitovu mara kwa mara,tatzo nn.
Nenda haraka kamuone Daktari.

[h=1]Dalili za kukutahadharisha[/h]Kama utaona baadhi ya yafuatayo, mwone daktari haraka iwezekanavyo:

  • Damu au maji maji zikitoka ukeni
  • Unarudiwarudiwa na uchefuchefu na kutapika
  • Kufura kwa uso au vidole
  • Kuumwa na kichwa kusikoma
  • Kizunguzungu au kuona kusikodhahiri
  • Uchungu au kiharusi kwenye sehemu ya chini ya tumbo
  • Homa na kibaridi
  • Kubadilika kwa mwendo (mazunguko) ya mwanae tumboni.
  • Mkojo kidogo zaidi au kuwashwa wakati unapokojoa
Kumbuka, inakufaa ufanye kila kitu uwezacho kujiweka na mtoto wako na rai.

 
mama mjamzito miez 5 akijiskia maumivu chn ya kitovu mara kwa mara,tatzo nn.

Habari yako,

Maumivu chini ya kitovu au kitovuni kwa mama mjamzito si jambo geni bali huwatokea wengi tu, sio jambo la kuogofya sana na wakati mwingine huwa inashauriwa kupata medical attention.

Nini sababu?

Kawaida mimba inapokuwa huwa inasababisha ngozi na nyama za misuli ya tumbo kuvutika hii hupelekea maumivu.

Wakati mwingine husababishwa na ukuaji wa mfuko wa mtoto/mji wa mimba 'uterus', hivyo mfuko huu hukandamiza sehemu ya kitovu na kusababisha maumivu. Mwanamke hupata aina hii ya maumivu wakati wa trimester ya kwanza ya ujauzito.

Mwanamke mwenye kupata aina hii ya mkandamizo utokeao ndani, ile sehemu ambayo hupatwa na mkandamizo huu huwa 'sensitive' na wakati mwingine huwasha pale inapogusana na nguo. Aina hii ya maumivu kwa kwaida huitwa "Umbilical Hernia" yaani kitovu kinatokeza kwa nje kama uvimbe hivi, hivyo ni vyema uonane na daktari wa masuala ya uzazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…