kilambimkwidu
JF-Expert Member
- Jul 21, 2017
- 6,097
- 7,199
Nimekubali maneno yenu wanajamvi juzi nlipoleta uzi ulohusu Meseji ya G9t alontumia mamkwe akinisisitiza kwamba mimi na mke wangu "tujitahidi ili usingizi wetu uzae matunda", wengi wenu mlisema kwamba mama huyu ni "mswahili" na anaingilia faragha yetu. Sema ukweli sikumjibu ile meseji. Jana kaja kivingine.
Jana usku majira ya saa5 kanishushia 'jiwe lingine' tena kantumia kwa njia ya Whatsapp. Anasema...
"Bwn Asifiwe. Sisi wazima. Najua uliiona meseji yangu ya juzi japo haukuijibu. Ninachokusihi mwanangu ni kwamba uongeze pilika basi ili ujenge mji wako ungali bado kijana. Usijisikie vibaya. Nasema hivo kwakua enzi zimebadilika, na ya Mungu mengi".
Mie nimemjibu....
"Asante mama. Pole sikujibu meseji yako kwakua nilijua jibu la kweli ni ujauzito. Tuvute subira. Asante, usiku mwema mama yetu"
Bado hajasema chochote. Vp, nipo sawa wakuu, ama!?