Mama Mobetto atoa ya moyoni sakata la kuporwa bwana na mama Diamond

Mama Mobetto atoa ya moyoni sakata la kuporwa bwana na mama Diamond

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Mobeto-3.jpg

Mama Mobeto.


KWA siku kadhaa kumekuwa na ubuyu mzito kuwa, mwanaume anayedaiwa kumuona mama wa msanii wa Bongo Fleva, Sanura Kassim almaarufu Bi Sandra anayetambuliwa kwa jina la Salum Shamte aliporwa kutoka kwa mama mzazi wa mwanamitindo wa kimataifa Bongo, Hamisa Mobeto, Shufaa Lutingunga, Ijumaa Wikienda limeichimba.

Kufuatia tuhuma hizo nzito, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo ambapo lilifanikiwa kumweka ‘mtukati’ mama Mobeto ambaye aliyafungukia madai hayo.

Mama Mobeto aliliambia gazeti hili kuwa, siku hizi ameamua kukaa kimya kwa sababu akiwa anafuatilia kila

kitu kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii, anaweza kupoteza maisha huku siku zake zikiwa bado hazijafika.

Mama huyo alifunguka kuwa, mwanaume huyo aliyemuoa Bi Sandra anamfahamu kama rafiki, lakini hajawahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Alisema kuwa, jambo hilo halikuwahi kutokea hata mara moja hivyo anashangaa watu wanavyopandikiza maneno.

“Huyo kaka (Shamte) ninamjua kama rafiki yangu tu na hatukuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi hata mara moja.

“Ninashangaa mno kuona au kusikia watu wanakomalia kuwa mimi nilikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

“Lakini siku zote mtu akiamua kusema, ninamwacha aseme au afanye awezavyo,” alisema mama Mobeto.

Kwa upande wake Bi Sandra hakupatikana hewani ili kusikia upande wake hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

dangotes.jpg

BI Sandra na Mumewe.




Muungwana
 
Magufuli taratibu baba, legeza kidogo, mimi huwa nadhani ni utani tu wa mitandaoni kumbe kuna kauzu kweli kajiweka kwa mama yake Diamond? ****'make wallahi kuna mijitu mikauzi kwelikweli nchi hii hasa wakishaferi maisha.
 
Aache hizo nae kwan kuna ajabu maana hamisa alishatoka na petit mume wa dada ake dai,kisha akakionja kiparachichi cha dai na juisi yake ndo hio anairingishia kila kukicha huku dai akigoma kuionja juisi yake kama vile haijatoka kwenye parachichi lake
 
Back
Top Bottom