Mama mzazi wa Nay wa mitego anahisi mwanae ni Freemason

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304


Mama mzazi wa Nay wa Mitego anahisi mwanae ni mfuasi wa jamii ya siri ya freemason na ameanza kusita kupokea fedha kutoka kwake.

Kwa mujibu wa mama yake, mafanikio ya haraka ya Nay yakiwemo kujenga nyumba ya kifahari, kumiliki magari kadhaa na maisha yake ya kimilionea, vimemfanya aamini maneno yanayosemwa na watu au kuandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa mwanae amepata utajiri huo kwa njia isiyo halali.

"Kuna kipindi ambapo nimetoa wimbo wa Mr Nay baada ya kutoka ile video nakumbuka mimi mama yangu huwa nampelekeaga hela ya matumizi kila baada ya wiki mbili au mwezi mmoja. Kuna kipindi nilimpelekea hela akasema ‘no' mbona mimi hela bado ninayo," Nay alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.

Nay anasema alimpelekea mama yake kiasi cha shilingi laki mbili ama tatu na akagundua kuwa mama yake hasemi ukweli na kuna kitu kilikuwa kikimsumbua akilini.

"Baada ya hapo akaniambia ‘kuna habari nasikia kuhusu huu wimbo wako huu nimeona mambo ya ajabu ajabu mule nimeona magazeti majirani wamekuja wameniambia hivi na hivi'," aliongeza Nay.

"Halafu bahati nzuri nilikuwa nimetoka kununua hii gari yangu ambayo natembelea sasa hivi ‘Morano' alivyoniuliza hivyo nikaona mama yangu hataki hela yangu sababu ana wasiwasi na hiki ambacho watu wanaongea. Hilo ni tatizo lililonipa wasiwasi na moyo wangu ukaingia unyonge, for real kabisa nikawa mpole."

"Lakini nikawa na imani kwamba endapo mama yangu angekuwa anatambua kwamba huu muziki ungekuja kuniweka sehemu uflani tangu zamani angekuwa ananisupport zile hustle mazingira magumu niliyokuwa napitia angekuwa anajua basi sasa hivi ningekuwa naenda naye sawa."Nay amesisitiza kuwa mali anazopata ni neema za Mungu tu.

"Mwenyezi Mungu tu ameamua kuninyooshea kuniwekea mambo yangu sawa japokuwa bado sijafika pale ninapotaka kufika," alisisitiza rapper huyo.
 
Hata ningekuwa mie ndio mzazi ningeogopa kwa video zake za ajabu ajabu
 
Lakini lisemwalo lipo. Ukiiangalia kwa makini video ya Mr Ney utaona sign kibao zilizowahi kutumiwa na wasanii wakubwa kama Jay Z, Rihanna na zinasemekana kuwa za Freemason
 
Lakini lisemwalo lipo. Ukiiangalia kwa makini video ya Mr Ney utaona sign kibao zilizowahi kutumiwa na wasanii wakubwa kama Jay Z, Rihanna na zinasemekana kuwa za Freemason

usidanganyike,huyo boya anatafuta kick tu.hana ubavu wa kuwa freemason
 
Interesting...........Labda Freemason wa mabox nay ni msanii na mama yake msanii waache waendelee na maigizo yao,murano na mjengo ni njia moja ya kujiongezee dau kwenye show zake,inamaana promoter akimpigia asianzie na laki lazima aende kwenye meter na kuendelea.
 
MawaZo ya akina mama wauza vitumbua
umenichekesha Mkuu, Mie ningekua mzazi wake basi ningemuita mtoto wangu tukaongea kwa kina na angesimama kama mzazi ukweli angeujua,naanzaje kusikiliza maneno ya majirani na nikayapasisha kumtia mtoto mkosi tuu,hajui kama nyimbo mbaya haimbiwi mtoto.........
 
Mama mzazi wa Nay wa Mitego anahisi mwanae ni mfuasi wa jamii ya siri ya freemason na ameanza kusita kupokea fedha kutoka kwake.

Kwa mujibu wa mama yake, mafanikio ya haraka ya Nay yakiwemo kujenga nyumba ya kifahari, kumiliki magari kadhaa na maisha yake ya kimilionea, vimemfanya aamini maneno yanayosemwa na watu au kuandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa mwanae amepata utajiri huo kwa njia isiyo halali.

"Kuna kipindi ambapo nimetoa wimbo wa Mr Nay baada ya kutoka ile video nakumbuka mimi mama yangu huwa nampelekeaga hela ya matumizi kila baada ya wiki mbili aumwezi mmoja.

Kuna kipindi nilimpelekea hela akasema ‘no' mbona mimi hela bado ninayo,"Nay alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.Nay anasema alimpelekea mama yake kiasi cha shilingi laki mbili amatatu na akagundua kuwa mama yake hasemi ukweli na kuna kitu kilikuwa kikimsumbua akilini.

"Baada ya hapo akaniambia ‘kuna habari nasikia kuhusu huu wimbo wako huu nimeona mambo ya ajabu ajabu mule nimeona magazeti majirani wamekuja wameniambia hivi na hivi',"aliongeza Nay.

"Halafu bahati nzuri nilikuwa nimetoka kununua hii gari yangu ambayo natembelea sasa hivi ‘Morano' alivyoniuliza hivyo nikaonamama yangu hataki hela yangu sababu ana wasiwasi na hiki ambacho watu wanaongea.

Hilo ni tatizo lililonipa wasiwasi na moyo wangu ukaingia unyonge, for real kabisa nikawa mpole."Lakini nikawa na imani kwamba endapo mama yangu angekuwa anatambua kwamba huu muziki ungekuja kuniweka sehemu flani tangu zamani angekuwa ananisupport zile hustle mazingira magumu niliyokuwa napitia.

Anajua basi sasa hivi ningekuwa naenda naye sawa."Nay amesisitiza kuwa mali anazopata ni neema za Mungu tu."Mwenyezi Mungu tu ameamua kuninyooshea kuniwekea mambo yangu sawa japokuwa bado sijafikapale ninapotaka kufika,"alisisitiza rapper huyo.
 
huwezi kua freemason kirahisi rahisi na sio kila mtu anaweza kua fremason,huyo nay hana uwezo wa kua freemason,hapa tanzania freemadon wapo 15 tu.
 
Huku kijijini tunasikia tu hizo habari za "kusadikika " bahati nzuri siku hizi waandishi wa Riwaya hawana hata "manuscript ".
 
Umaskini ni kitu kibaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…