MAMA na MWANA ya RTD .- tukumbushane

MAMA na MWANA ya RTD .- tukumbushane

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
5,937
Reaction score
1,440
Wadau
Hiki kilikuwa ni moja ya vipindi maarufu vya RTD hsawa kwa watoto hasa kwa watoto wa primary enzi hizo.

Watanzagaji wake nadhani alikuwa ni Debora Mwenda.

Kuna zile hadithi zilikuwa zinenda kwa mtindo wa series. teh teh teh teh teh .

Je mnaikumbuka hadithi ya Binti chura.?????? Wewe unakumbuka nini kwenye vipindi hivyo vya mama na mwana.

Karibuni katika flash back
 
umenikumbusha mbaali sana
miminakumbuka ile hadithi ya 'hadithi isiyo na mwisho'

nilikuja kuitazama movie yake later....
 
aliekua msikilizaji wa kipindi hiki ni lazima azikumbuke hadithi hizi. ADILI NA NDUGUZE; UA JEKUNDU:
 
Kunyenge...maji ya uzima,na ule wimbo wa wanyama...africa yote inapenda twist!!
 
hadithi ya zimwi sijui.......... kilikuwa kizuri sana kile kipindi mana ikifika jmosi mchana akili yote haikai vizuri hata kula unasahau mtu. thanks mkuu kwa kutukumbusha those happy and favourite days. wish miaka irudi nyuma..........
 
umenikumbusha mbaali sana
miminakumbuka ile hadithi ya 'hadithi isiyo na mwisho'

nilikuja kuitazama movie yake later....

hadithi ipi hiyo kamanda ?

Saint Ivuga said:
jumamosi mchana
Sasa ikitokea muda muda huo wa kipindi unatumwa kununua chumvi robo kilo wa mangi sio kununa huko........ teh teh teh teh
kinyoba said:
aliekua msikilizaji wa kipindi hiki ni lazima azikumbuke hadithi hizi. ADILI NA NDUGUZE; UA JEKUNDU:
Kweli kabisa hizi siries na zilikuwa kiboko
Hivi bado hiki kipindi kipo maana FM radios na TV zimefanya RTD iwe redundant
 
....nchi ya samawati...nadhani ndi ilikua hadithi ya binti chura..na kibanda cha bibi mwenye matongo tongo...

naona wanazirudia TBC 1 lakini hazina mvuto sana
 
Ua Jekundu..lol lol ..
Mpiga Filimbi wa Hamelin or Hamelun sikumbuki vizuri.
Binti chura ilikuwa tamu nimekumbuka mbali mie.
Jmos moja hatukuwa na betri ,faza hakuwa home ikabidi tuanike betri juani ili tu tupate kusikiliza mama na mwana mchana
lol tunatoka mbaaaaaaaaaaaaaali sana
 
....nchi ya samawati...nadhani ndi ilikua hadithi ya binti chura..na kibanda cha bibi mwenye matongo tongo...

naona wanazirudia TBC 1 lakini hazina mvuto sana

wamtafute Debora mwenda awape burudani watoto
 
naona wote mmesema jumamosi mchana, ila nimegundua hamjui ilikuwa saa ngapi.
Kipindi kilikuwa saa 8 mchana ila sikumbuki kilikuwa kinaisha mida gani, either kilikuwa kinaisha saa 8 na nusu au saa tisa au saa kumi
 
..........
Jmos moja hatukuwa na betri ,faza hakuwa home ikabidi tuanike betri juani ili tu tupate kusikiliza mama na mwana mchana
lol tunatoka mbaaaaaaaaaaaaaali sana

Hahhaahha 1st lady umenichekesha sana. thanks. Nimesahau hata story za kifisadi. hili jukwaa la chit chat ni kama panadol

naona wote mmesema jumamosi mchana, ila nimegundua hamjui ilikuwa saa ngapi.
Kipindi kilikuwa saa 8 mchana ila sikumbuki kilikuwa kinaisha mida gani, either kilikuwa kinaisha saa 8 na nusu au saa tisa au saa kumi

Yah muda wa hadthi ambayo wengi ndio tulikuwa tunapenda ulikuwa ni dk zisizozidi 30.. Nimesahau sehemu nyingine ya vipindi ilikuwa walikuwa wanaongelea nini.
 
Ua jekundu
adili na nduguze, nduguze kuwa manyani etc.
Kulikuwa na clubs za watoto ilikuwa raha
 
Siku zimeeenda! Mama na Mwana kilikuwa kikipendwa hata na watu wazima pia! Kilikuwa na kimesheheni mafundisho kwa watoto. Pia kulikuwa na kipindi cha Watoto wetu, hapo utapata Kwaya,Ngonjera, Tenzi nk kutoka ktk shule za msingi ktk mikoa mbalimbali ambayo iligawanywa ktk kanda mbalimbali. Hapo namkumbuka Aloycia Maneno, Nyambona Masamba, Christina Chokunogela, Halima Mchuka na wengine tele. Leo utasikia watoto wakiinba nyimbo za mapenzi na mtangazaji anasifia kipaji cha mtoto! Aibu..!
 
Naikumbuka sana Hadithi ya Binti Chura.
Wakati inaendelea kusimuliwa nikapata bahati ya kupata kitabu chake Maktaba, nikakiazima nikarudi nacho home, Jmos iliyofuata tukajikusanya watoto na kitabu chetu. Those days... When life was so gud!
 
Umenikumbusha those good days,kipindi kilikuwa kizur sana. Adili na nduguze,Neema na kaka zake na kisa cha Akajase mbamba.zilikuwa simulizi za kusisimua ambazo unahakikisha hukosi mwendelezo wake.
 
Akajasembamba.....hii hadithi nakumbuka iliniingia sana lakini siikumbuki vizuri, na pia Adili na nduguze, Ua jekundu, binti chura, nchi ya samawati, Hazina ya Mfalme Suleiman, Alibaba na wezi arobaini n.k......those days bana
 
Enzi hizo mida ya saa nane j,mosi unasikiliza huku harufu ya ugali inanukia jikoni sio siku hizi loh aibu aibu tupu mambo ya dot com
 
Back
Top Bottom