Mama ndalichako tafadhali litazameni hili la ufaulu wa kutoka kidato cha pili kuingia cha tatu

Mama ndalichako tafadhali litazameni hili la ufaulu wa kutoka kidato cha pili kuingia cha tatu

proff g

Senior Member
Joined
Jul 16, 2016
Posts
146
Reaction score
113
SERA
Tangu sera mpya ya Elimu ya mwaka 2014 iliyopitishwa na Raisi wa awamu ya nne Dr Jakaya M Kikwete pamoja na waziri wa elimu wa wakati huo Dr Shukuru Kawambwa kumefanyika mabailiko katika mambo mbalimbali. Kubwa hasa nihili linalotambua kuwa Elimu msingi ni kuanzia darasa la awali, darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

UTEKELEZAJI
utekelezaji wake umeleta mabadiliko katika alama za ufaulu hasa darasa la saba kuingia kidato cha kwanza pamoja na kidato cha pili kuingia kidato cha tatu. kwa mfano miaka ya 2000 ilihihitaji mwanafunzi wa kidato chapili anapofanya mtihani wake wa upimaji afaulu kwa kiwango cha wastani wa 30, kimsingi mwanafunzi afaulu kwa daraja D kwa kila somo katika masomo yake 9. Hali ya sasa, inahitaji mwanafuzi awe na ufaulu wa wastani 6.7 kwa maana afaulu masomo mawili kwa daraja la D au afaulu somo moja kwa daraja la C aweze kuingia kidato cha tatu.

RAI
waziri wa Elimu mama Ndalichako litazameni hili linaathiri ubora wa elimu, watoto hawaweki jitihada kabisa katika ujifunzaji wao hasa shule za kata, ufaulu unaonekana ni mkubwa kwa kidato cha pili lakini wanapofika kidato cha nne wengi wao safari inaishia hapo, wazazi hasa hawa wavijijini wanafurahia hali hii lakini mwisho wa siku watoto wao wanabaki nyumbani. Mimi kama mwalimu inaumiza kuona watoto wengi hawana mwendelezo mzuri.
 
Back
Top Bottom