Mama ni mama, vyovyote alivyo hapaswi kusemwa vibaya za ya kumuombea

Mama ni mama, vyovyote alivyo hapaswi kusemwa vibaya za ya kumuombea

mwanzo wetu

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2014
Posts
1,581
Reaction score
462
Habari za wakati wanafamilia.

Nianze kwa kusema kuwa ni mda wa kukaa pamoja Kama Taifa bila kuangalia itikadi zetu za vyama.

Niwapongeze pia wapinzani kwa asilimia 💯 wameonesha ustarabu mzuri kwa kuwa wakimya najua wamezingatia kauli mbiu ya mama ni mama hivyo Mungu awasaidie waendele kutulia na mama hata waangusha maana mama ni nuru na tabia za Mama mtoto akilia lazima afutwe machozi kimsingi mama hapendi kuona mtoto wake akilia hata Kama amemchapa yeye, kimsing ni tofauti na baba yeye akikuchapa utasikia lia ndio utajifunza sisi wazazi wa kiume huruma ni ndongo sana.

Natengemea kila mmoja amuombee mema Mh. Rais Samia bila kujali yupo upande gani wa kisiasa wote tunapaswa kumuombea mema yeye Kama mama wa Tanzania ili ajawe na Furaha na hatimae atupikie chakula kizuri na kitamu na tule huku nyuso zetu kitabasamu.

Nimekua nasikia mama hakosei na hii ni kweli mama hakosei siyo kwamba mama hawez kukosea Lahasha ilaa makosa ya Mama huwa yatajwi na mtoto ila mama anaweza kusema makosa ya mtoto bila shida na mtoto akakaa kimya.

Hitimisho nikuwa mama Yetu hatakiwi kusemwa kwa lolote zaidi ya kuacha atutafutie chakula ili tulale tumekula hii ndio adabu ya toka zamani ya mtoto kwa mama.

Mungu mbariki mama Yetu Samia, Mungu ibariki Tanzania ya upendo.
 
Unaijua katiba wewe? Hebu tuwekee kipengele cha Katiba kinachosema Rais akiwa ni KE hastahili kukosolewa.
 
Aliepewa kapewa hayo makatiba yenu tupa kulee
 
Back
Top Bottom