Mheshimiwa Ngongo,Heshima kwenu wakuu,
Mama Salma Kikwete aingia Arusha kwa staili ya kutupa fulana,kofia na scuff.Nilikuwa maeneo ya Stadium chini ya mti eneo maarufu kwa wacheza draft na madereva taxi ghafla mlio wa ving'ora vya polisi uliashiria wenye nchi wanapita kufumba na kufumbua Mama Salma Kikwete ndani ya Landcruiser anapita na kupunga mkono na tabasamu la aina yake anawarushia fulana,kofia na scuff hali inayosababisha mtafaruku na purukushani za kugombea zawadi za Mama Kikwete.
Naomba kuuliza sheria ya gharama za uchaguzi inasemaje,wajuzi wa sheria hii naomba msaada !
nyie huyu mama na mumewe akili zao sawasawa, ama kweli Mungu hukupa mke wa kufanana nae.
Kuna mtu alisema hapa JF "ukitaka kupima akili za mume angalia matendo ya mkewe"
Salma Kikwte ana tamaa ya madaraka kuliko aliyonayo mke wa mgabe na Lucy Kibaki. Kwa tamaa yake ya madaraka na elimu ndogo ameamua kumshawishi mume wake warushe karata kwa watoto wao ili nao wauze kitakachosalia huku wao wakiwa wazee.
Jibu ni moja, tar 31 Oct.... Chagua Slaa (PhD) kukomesha udhalimu huu.
Nimeshapata tiketi ya Precision nakuja Dar jumamos kwa ajili ya kupiga kura. Wife kanithibitishia kuona jina langu kituoni. Naja ndg naja na kura yangu mkononi kumpa Slaaa
Salima Kiwete ametoka kwenye ukumbi wa CCM mkoa hapa Arusha palipokuwa panafanyika kikao cha wanawake kama dakika 45 zilizopita, nimeona akiwapungia mikono watu waliokuwa jirani na eneo hilo cha kushangaza watu walikuwa wanabaki kumkodolea macho badala ya wao nao kumpungia... jamani ccm hamtakiwi