Mama Salma Kikwete anusurika kupata ajali mkoani Mara

Pamoja na kwamba tunatoa pole kwa matatizo ya namna hii, lakini tukumbuke kwama misafara ya viongozi nayo pia ni mojawapo ya vyanzo vya ajali, hasa pale ambapo jamii husika ambapo kiongozi atapita inakuwa haijajulishwa kwamba kiongozi atapita. Tunahitaji kuliangalia suaa hili kwa upande wa pili.
 
Kule kwenye saiti yangu niliandika hivi tarehe 26 na bado naamini tutakuwa na ajali kubwa ya kiongozi fulani.. isipokuwa kama tutawakinga kwa maombi:
mkuu nilikuwa nataka kutoa koment kali ila ikabidi nicheke baada ya kusoma atiko yako.
mkuu ulijifunzia kwa yahaya husein lini haya mambo? au ndo mambo ya KAINZI krtu kale kufukunyua kusikofukunyulika?
 
Pole sana Mama Salma na tuko pamoja katika sala.Ila najaribu kuimajin hicho kisago alichopata dereva wa lori mmmmmmmhhhhhhhhhhhhh!
 
Mimi nafikiri ni faraja haya yakitokea, yaani wakubwa pia kuandamwa na ajali pia, huenda ndiyo watapata akili ya kudhibiti ajali zinozo tumaliza nchi hii.
 
Hahaaaaa...Ninahisi hivo,ama ni mtani wa watu wa Taarime

Nimejaribu kusoma posts zake hapa, sikuona kama bulesi ni mtu wa "taarime" kwa mtizamo wangu ... ila anaonekana sana kuchangia mambo ya barrick na ughaidi wao wanaoufanya kule north mara. .... and if you "aksed" (nikikopa lugha ya black americans), bulesi mara nyingi anakuwa upande wa barrick.
 

Habari hii inaonyesha imenukuliwa....tupe source basi. Vinginevyo hizo alama za kunukuu hazina maana.
 
Pole sana Mama Salma, ajali hizi zimekuwa nyingi sana kwenye barabara zetu bila shaka wakuu wtalitupia jicho kwa karibu tatizo hili.
 

Tunampa pole sana ....na tunaomba wahusika wafikirie kupunguza ukubwa wa msafara wake ...pengine haumsaidii sana!!...tazama waliomtangulia mama maria,sitti,na anna...walikuwa hawatembei na msafara wowote ....zaidi ya kuwa na askari usalama mmoja kwenye gari mwenye self defence kit na vifaa vya mawasiliano....[ikiwa atakutana na vizuizi barabarani ..iwe foleni au chochote ..mlinzi wake anatoa signal na anapita bila wasi wasi wala kuleta attention]....na Mungu amewasaidia nao hawakuwahi kupata tatizo la kutishia usalama wao !
 
Kule kwenye saiti yangu niliandika hivi tarehe 26 na bado naamini tutakuwa na ajali kubwa ya kiongozi fulani.. isipokuwa kama tutawakinga kwa maombi:

Hee, MWKJJ, umekuwa kama sheikh Yahya kaka??!! .... hebu tupe sababu za kisayansi ya wewe kuhisi hivyo.
 
Hivi nafasi ya First Lady kikatiba ikoje? Naona mara nyingine inakuwa kama ni naibu Makamu wa rais au hata zaidi ya hapo. Kuna utafiti umefanyika kujua kuwa ziara hizo huwa zinagharimu kiasi gani na huongeza "value" kiasi gani?

Ila wakuu pamoja na swali hilo, nampa pole sana Mama Salma kwa mkasa huu.
 
Habari hii inaonyesha imenukuliwa....tupe source basi. Vinginevyo hizo alama za kunukuu hazina maana.

Kwani lazima kuchangia!, I am not plagiarist. Go through all my posts and find out my writing style. Always I give credit where it belongs.

Kwa taarifa yako Kiswahili nilipata "B" na Kiingereza "A" Kidato cha nne enzi za Mwalimu. Uwezo wangu wa kuandika nafikiri hauhitaji darasa la ziada kama huelewi nilichoandika uliza nikupe ufafanuzi.

This is a "Total Obstruction" from the Topic in discussion, by the way you are free to express your views and thanks for quoting my post for technical error you have sighted hoping umeelewa nilichokuwa namaanisha. Si lazima ujaze "pointless posts" in your account. Always try to be a "Great thinker"
 

Enheheeheee! msiishie hapa jamani endeleeni....wengine tunaburudika sana na mambo ya namna hii.
Mgonjwa jibu bwana.....!
 
Enheheeheee! msiishie hapa jamani endeleeni....wengine tunaburudika sana na mambo ya namna hii.
Mgonjwa jibu bwana.....!

Hahahaha, Kule kwetu wanamsemo mmoja. "...Akikimbia na nguo zako usimfukuze maana wewe ndiyo utaonekana...."
 
Sasa je nini mwisho wa hilo tukio? Je hilo lori lilikamatwa na liliguwa na magendo gani?
 


Teh teh huu unaitwa mchanyato wa lugha toka middle school
 
Pole sana mama Salma.

Mnampa pole ya nini wakati Sheikh Ubwabwa wa Magomeni karibu na BP alitabiri?
Naomba kujua, hii WAMA ni subsidiary ya Chama Cha Maulaji? Manake FL1 kila anapoenda mahali kwa kofia ya WAMA lazima akipigie chapuo Chama Cha Maulaji..........!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…