Mr Sir1
JF-Expert Member
- Sep 23, 2018
- 1,749
- 7,945
Inawezekana ikawa bado mapema kumhukumu moja kwa moja ila kubwa linalomuangusha Mama ni kutaka kupendwa na kutekeleza kwa wakati mmoja. Kama kiongozi inapaswa ajue wapi pakubembeleza mahaba na wapi pa kuweka sura ya mbuzi.
Katika jaribio la kujionyesha yeye ni tofauti na mtangulizi wake, anaishia kuwa muungwana kupita kiasi. Magufuli alifanya makosa mengi mno ikiwemo kutokuwa na utu lakini haimaanishi Mama ajifanye muungwana sana ili aonekane bora mwisho wa siku watampiga na hata asijue kapigwa na nini.
Kama Mama anahitaji hasa kuweka legacy yake, angeanza na Baraza la Mawaziri. ilipaswa alifumue lote. Aweke watu ambao kawateua yeye, ambao watakuwa answerable kwake yeye na sio kuendelea na teuzi za Magufuli.
Maana kuna baadhi ya wateule wanahisi kuwa mama hana mamlaka juu yao kwa vile sio yeye aliewateua. Kuna baadhi wanaamini kuna waliokaribu na Mama ambao wana sauti kuliko mama. Kuepukana na hili angeanza upya na watu wapya. Tofauti na hapo daima atatazamwa kwa mlinganisho na Magufuli ama kumithilishwa na Magufuli kabisa.
Ili aonekane yeye kama yeye, aepuke sana kujiweka na magroup kidhahiri kabisa. Mfano kuhusishwa kwake na Kikwete kushawapa wakosoaji wake pa kuanzia. Ambapo ni kumlinganisha na Kikwete. Ina maanisha kila alifanyalo watu washalipa hatma kuwa litakuwa kama la Kikwete.
Mama aanze kusimama kama Samia. Sio muendelazaji wa Magufuli ama mshauriwa na Kikwete.
La mwisho, japo ana nia njema ya kurejesha uhusiano wa kimataifa; angetulia kidogo na hivi visafari vya hapa na pale, awaache wasaidizi wake. Maana japo safari zake zinaweza kuwa na tija, mbeleni zitatumiwa kama bakora ya kusema hakukaa nyumbani alikuwa busy na safari kama Kikwete.