Mama Samia usisahau masuala ya ueledi katika sayansi ya Tehama kwenye Serikali yako

Mama Samia usisahau masuala ya ueledi katika sayansi ya Tehama kwenye Serikali yako

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
Kwanza pongezi kwa kuingoza Tanzania kwa busara.

Ombi langu tusaidie wananchi kuhusu Huduma za tehama. Ni aibu kwa taifa hili lenye miaka zaidi ya 50 lakini huduma zetu za Tehema ni very poor, unprofessional.

Ukiboresha huduma za tehama, utasaidia wananchi wengi kupata huduma kwa wakati na kumpunguzia gharama za usafiri.

Fikiria mtu anaitaji uamisho kutoka wilaya moja kwenda nyingine. Idara ya tehema ya TAMISEMI ingekuwa inafanya kazi kwa ueledi watumishi wasingeenda Dodoma kufatilia uamisho huo.

Kuna usumbufu sana kupata loss report kutoka idara ya polisi kisa tu idara yao ya Tehama ipo verry poor. Nimeibiwa vitu vyangu nyumbani lakini kila nikijaribu kujaza report hiyo mtandaoni, jibu nalopata ni system error mpaka naona kero kufatilia report hiyo maana polisi nilikaa zaidi ya masaa matano nasubiri huduma hiyo ila sikuipata.

Tazama idara za tehama za idara nyingi za serkali zipo outdated kwamba zonataarifa za nyuma sana. Wengine wameweka namba za simu sizizopatikana mfano ni nssf ambapo wadai wengi wanazungushwa bila kulipwa pesa zao idara yao ya tehama haifanyi kazi kabisa.

Unaweza kuwatumia email ya madai ya mafao yako online wasikupe majibu kabisa sasa sijui wote wanataka tujazane kwenye maofisi yao? Sijui, ila mheshimiwa Rais tia mkazo kwenye maendeleo ya tehama kwenye idara zote za serikali na hakikisha wanaoajiriwa kwenye hicho kipengele wanakuwa ni wasomi kweli.

Ukiboresha hapo kwenye tehema utasaidia wananchi wengi hasa kutupunguzia gharama za kusafiri kufatilia huduma.
 
Amekusikia mama ni mwema sana na ni msikivu kama alivyokua hayati Magufuli!
 
Back
Top Bottom