Mama Ummy bint Anzuani shujaa wa siasa za mageuzi Tanga

Mama Ummy bint Anzuani shujaa wa siasa za mageuzi Tanga


MJUE MAREHEMU MAMA UMMY BINT ANZUANI MUASISI WA MAGEUZI TANGA

Binafsi sikutegemea kuwa mkutano wa Tangamano, Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa 1995 utakuwa mkubwa kiasi kile.

Niliyoshuhudia Tangamano siku ile nilijua wazi kabisa kuwa CUF itashinda Tanga na kitakuwa chama kikubwa kuipita CCM.

Utabiri wangu ulikuwa sawa na umedumu toka siku ile hadi leo miongo miwili.

Ratiba ilionyesha kuwa baada ya mkutano ule mgombea wetu wa CUF kiti cha Urais Tanzania Bara Prof. Ibrahim Lipumba na msafara wake wataelekea moja kwa moja kutoka Viwanja vya Tangamano mkutanoni hadi nyumbani kwa Mama Ummy, Ngamiani kwa ajili ya dhifa iliyoandaliwa kwa heshima yao.

Msafara wetu ulitanguliwa na kimulimuli cha gari ya polisi hadi nyumbani kwa Mama Ummy Ngamiani Barabara ya 11.

Nani huyu Mama Ummy?
Msikilize Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso:
 
Sisi tukitaka Video tunaenda YouTube, ila hapa JF tunakuja kusoma sio kuangalia.

Pia ningependa kujua kwanini unatumia herufi kubwa kwenye title tofauti na watu wengine? Naona ni kero.
 
Sisi tukitaka Video tunaenda YouTube, ila hapa JF tunakuja kusoma sio kuangalia.

Pia ningependa kujua kwanini unatumia herufi kubwa kwenye title tofauti na watu wengine? Naona ni kero.
Figga...
Yawezekana katika matumizi ya kichwa cha habari nafanya kosa kutumia herufi kubwa.

Yawezekana pia nakosea kuweka video hapa barzani.

Hakuna mtu aliyenizindua katika haya.

Ikiwa nafanya kosa na wengine wakawa wananistahamilia pengine kwa kunistahi kwa huu uzee wangu tafadhali nielekeze.

Hakuna binadamu ajuaye kila kitu.
 
Back
Top Bottom