Ni hbr ya kusikitisha kwa kweli. Suala la zima la kupata watoto ni neema tu kutoka kwa Mungu. Kuna wengine wapata bahati hiyo na kuna wengine hawakubahatika ktk hili.
Pia wapo ambao hawajabahatika kwa sababu ya uzembe wao wenyewe kwa kuwa na matumizi mabaya ya viungo na miili yao, lakini wapo pia ambao hawakubahatika kwa sababu ya matatizo ambayo mtu anazaliwa nayo.
All in all, huwa ninasikitika kusikia hbr hizi za wadada kuiba watoto kwenda kupeleka prove kwa mumewe/ndugu wa mume kuwa na wao wanaweza kuzaa.
Cha msingi, sisi wenye ndugu na tuachane tabia za kuingilia ndoa za wenzetu kwa masimango ya kuzaa au kutokuzaa maana ndiyo chanzo cha haya yote
Na kwa familia ambazo hazijabahatika, waache tabia za kuiba watoto. Ni vyema watulie wamuombe Mungu, huenda kwa imani yao, one day wanaweza kubahatika kupata watoto.
HP