Mama wachungaji acheni kuwapotosha wanawake wezenu

Mama wachungaji acheni kuwapotosha wanawake wezenu

Loading failed

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2023
Posts
2,603
Reaction score
7,501
Ndugu zangu

Ukweli upo wazi kwamba kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwezake ila watadumbukia shimoni wakiongozana

Wanawake wengi wanaojiita mama wachungaji au wake wa wachungaji tunajua wazi kabisa huko nyumbani kuna mikikimikiki na wao wanapigania ndoa zao.

Sasa linapotokea swala la migogoro baina ya mama wa chungaji na inapofika siku ya ibada au jumapili tunawaona huko kwenye mahema wakipewa mic na badala yake haubiri kile kinachotakiwa ila mawaidha yake yote ukiyasikiliza kwa kina unajua hapa kabisa ni majeraha ya mapenzi kutoka kwa mumewe anayo na anayaweka wazi kwa kigezo cha kuhubiri.

Wapo mama wachungaji wanao nyimwa hela na waume zao na kuja kwenye kipaza sauti na kupindisha ukweli kwa kusema wanawake wanaweza

Wapo mama wachungaji wengine ni masingle maza walio haribu ndoa zao wanaokuja kwenye mic na kuwaambia wake zetu kuwa hata huyo mwanaume uliye nae sio wako njoo uombewe uonyeshwe mume wako

Wapo mama wachungaji waliowateka wanawake wenzao kifikra na pindi linapotokea swala la mahusiano kuyumba utakuta wanawashauri wanawake wenzao hata huyo mwanaume ni ajenti wa shetani

Wapo mama wachungaji wanao wapiga mabinti upofu kua mume wake atampata ibadani na kusahau mume hata huko kazini anaweza kumpata kiasi cha kuwafanya wanawake wengi kuzeeka bila kuolewa kwa kigezo hakupata mwanaume

Wapo mama wachungaji wasio na adabu wanajua kabisa mwanamke aliyeolewa anapaswa awahi kwenda kupikia watoto na mume wake, wanajua kabisa wanawake wenzao waliopo kwenye ndoa wanapaswa kwenda kutunza ndoa zao ila utakuta wanawang'ang'ania huko kwenye mahema mpaka usiku wa manane bada ya kuwaambia ukweli nendeni nyumbani ukatunze ndoa na watoto

Wapo mama wachungaji watajifanya wanamshauri mwanamke mwezao kuhusu ndoa na kumuhimiza aje ibadani kumbe nyuma ya pazia wanafurahia kuona ndoa ya mwanamke mwezao inayumba na kuvurugika

NIMENGI SANA WANAFANYA ILA KWA LEO NIMEWEKA KWA UCHACHE SANA
 
Back
Top Bottom