Mama Yake Adebayor Mchawi

Focus120

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
1,089
Reaction score
793
Mshambuliaji wa kilabu ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.
Duru zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.

Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga''aliwauliza maripota.
Mchezo wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham umeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi January kufuatia kushuka kwa mchezo wake.
 
mfyuuu akuroge kwalipi ange taka si angekuua kabla hujazaliwa au ulivokua mdogo akuroge mkubwa hivo na unamsaidia mitoto mingine hasara huna adabu kwa mama ako ushuke kiwango wewe useme mamako anakuroga mbona mambo yalivo kunyookea hukusema hayo aalaas! umejitafutia laana ndo mwisho wako huo mpaka uka ombe radhi kwa mamako
 
Adebayor mwenyewe amesema ajamfukuza mama yake kwenye nyumba ya Togo lakin ameondoka mwenyewe.

Pia huyo mama yake amekuwa akimwambia Adebayor hautofanikiwa hautofanikiwa.

na huyo dada yake alioenda kuongea ubaya hivyo kwenye radio amejengewa jumba la zaidi ya pound za UK Million 1.

Na cha ajabu nyumba ameipangisha bila ata kumwambia Adebayor.

Source Adebayor.

Maoni yangu ni kuwa kuna familia nyingine hasa Afrika Magharibi wana roho mbaya unaweza onewa wivu na ata ndugu zako wa damu.

Cha muhimu kama mkijadili muangalie upande wote
 
Wasiongelee mambo ya familia kwenye media wanawapa faida wanauza habari.Aitishe mkutano wa familia na wazee wayamalize.maisha nimafupi kugombana hakusaidii
 
Ndio maana iliitwa familia mambo yenu ya familia ongeleen ndan tena mkiwa mmefunga milango na saut zimeshushwa chini sis hayatuhusu
 

Kuna mchezaji mmoja wa ghana alikuwa moto sana Nii Lamptey walimfanyia mambo mpaka akashindwa kutoka kimataifa watu wa magharibi mi nawaona nuksi sana sisi tuna roho mbaya ila west wamevuka hicho kiwango
 
Afrika ndio maana haiendelei kila siku kuamini ushirikina ukifanikiwa Mungu ukishuka kiuchumi unasnza mtafuta mchawi mmh
 
Wazaz wake wanajua mafanikio yake yametokana na juju,kwahyo inawezekana kwa sasa ni kukosea masharti,kuna mate wangu mtogo alisema adebayor kabla ya mech lazima kwao togo wazike ng'ombe mzima kama kutoa sadaka kwa mizimwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…