Mama yake Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes 1950s

Mama yake Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Hii makala niliiandika siku kama ya leo mwaka jana. Leo niko hapa najibu maswali kuhusu Abdul Sykes. Ndugu zangu hebu someni hayo makala hapo chini:

TAHARUKI YA BI. MUGAYA NYANG'OMBE NA WANA TANU: NANI KAMLISHA NYERERE SUMU KUMUUA?

Ningependa kuchangia moja katika niyajuayo ya Bi. Nyang'ombe mama yake Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mkasa huu amenihadithia Mama Daisy mke wa Abdul Sykes ambao ulitokea katika miaka ya mwanzo ya TANU baada ya Mwalimu Nyerere kurejea kutoka UNO mwaka wa 1955.

Ilikuwa kawaida ya TANU ikiwa wana jambo muhimu na kubwa wanataka kujadili kufanya kikao nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukukuu.

Pamoja na kuwa watakuwa na kikao walikuwa na kawaida ya kuwa katika nyumba ile na watu wao wa karibu.

Bi. Mruguru bint Mussa mama yake Abdul atakuwapo, Bi. Nyang'ombe mama yake Nyerere pia atakuwapo halikadhalika Mama Maria Nyerere atakuwapo hapo.

Inawezekana hawa walijumuishwa katika mkusanyiko ule wa viongozi wa TANU kama kichaka cha kuficha yale yaliyokuwa yakijadiliwa ili ionekane kuwa hapakuwa na kitu pale nyumbani kwa Abdul ila ni ndugu kutembeleana.

Ingia katika link hiyo hapo chini usikilize taharuki iliyokumba moja ya kikao kama hiki siku Mwalimu Nyerere alipougua ghafla baada ya chakula cha mchana na ikadhaniwa amelishwa sumu na maadui wa TANU.

(Tazama video nazungumza dakika ya 40).

Tunamkumbuka Mwalimu Julius and we. Je, tunamfahamu mama yake mzazi?

MUGAYA NYANG'OMBE (1).jpg
 
Back
Top Bottom