ZINGATIA HAYA KIJANA ILI UWEZE KUAJIRIKA AMA KUJIAJIRI MAPEMA
Wimbi la ukosefu wa Ajira ni kubwa duniani kote sio tu Tanzania. Ni tatizo linalohotaji suluhisho la kimkakati ili kulipunguza kama sio kuliondoa kabisa. Wasomi kwa sasa ni wengi na kila mwaka wanaohitimu vyuo kwa ngazi mbalimbali ni wengi sana. Na kupelekea tatizo la Ajira kuwa la kudumu maana uhitaji ni mkubwa kuliko uwezo wa kuajiri wahitaji wanaohitaji hizo nafasi katika sekta binafsi na za serikali.
Haya machache yatasaidia vijana kupenya kwenye soko la Ajira kama yakizingatiwa vizuri:-
1. Tengeneza thamani yako ambayo itaendana na jambo unalolitaka ama kutamani kulifanya. Na hii ianzie huko chuoni. Jijengee utamaduni wa kujua mambo kama jinsi ya kuwa na mazungumzo yenye tija hata kwa wanafunzi na watu waliokuzunguka pia jinsi ya kujumuika na watu katika masuala mbalimbali ya elimu,uongozi,biashara,kilimo n.k. Na hii thamani inatengenezwa na wewe mwenyewe.
2. Kuwa mbunifu juu ya jambo unalolifanya,usilifanye kwa ukawaida ama kwa mazoea bali liongezee hata ubunifu wa ziada ili liwe lenye kupendeza na kuvutia zaidi. Hii itanzia unavyopangilia mambo yako. Mfano hapa mjini Dar es salaam wapo wengi wanaouza juisi lakini ubunifu anaoutumia Mack Juice ama Zanana Juice ni tofauti na hawafanani ila wote wanapata wateja kwa namna walivyoamua kujitangaza.
3. Ujuzi na maarifa uliyonayo ndio mtaji wa kwanza hata kabla ya kuwaza pesa. Mfano mhitimu wa chuo aliyesoma Bacholer of Business Administration anaweza kuwa mtaji mkubwa wa ujuzi kwa wajasiriamali kuwaonesha namna bora ya kuweka mipango mizuri ya biashara zao na waweze kukua zaidi. Huo ni mfano mmoja tu ila wasomi ni wengi na wenye ujuzi mbalimbali usijifungie ndani Bali ujuzi wako ni faida kwa wengine.
4. Penda kujitolea. Hili ni jambo ambalo linaweza kuanzia hata chuoni kwa kutafuta kazi za kujitolea katika taasisi mbalimbali ili kupata uwezo wa kufanya kazi ya kile unachokisomea ili baadae iwe rahisi kwako kujitofauti katika soko la Ajira na wengine maana ujuzi wa mambo kwako utakuwa juu tofauti na yule anayesubiri tu kazi nyumbani bila hata kujitolea hata kwenye kazi za kijamii.
5. Jenga tabia njema kwa kubadili mtazamo kuwa jambo fulani linawezekana. Hii itakusaidia kuacha kulalamika na kuona kila jambo ni gumu ama kujihisi wewe huna bahati ni mtu wa mkosi.
6. Kwa kila jambo unalolifanya jaribu kuwa makini nalo(Be serious) yaani lifanye jambo kwa umakini hata kama kazi hiyo umepewa na rafiki yako ifanye kwa umakini na usifanye kwa mazoea na kwa wakati. Hii itakusaidia kujenga uaminifu hata siku nyingine itakusaidia kupewa kazi kubwa na ambayo inaweza kukufanya kuaminika kirahisi. Kwahiyo ushikaji weka pembeni mtu anapokupa jambo la muhimu la kuyafanyia.
7. Zidi kujifunza ili kupata ujuzi zaidi. Katika dunia ya sasa kujifunza hakukomi katika maisha ya kila siku maana unaweza kujiita msomi ila ukajikuta kumbe wewe ni msomi aliyepitwa na wakati. Vitu vinabadilika kila siku na soko la Ajira linabadilika kila siku kwahiyo ni lazima kuwa wakujifunza kila siku na kila wakati. Jambo lolote unalolitaka kwa dunia ya sasa unaweza kulipata ila itategemea na jitihada zako. Unaweza kujifunza kwa kuhudhuria semina mbalimbali maana sipo hata za bure unaweza kusema sina hela,kuna kozi za mtandao mfano kutoka Alison,Niajiri Platform Tanzania n.k,kupitia google,youtube n.k
8. Kujitangaza. Hii itatokana na CV yako nzuri,namna bora ya uandishi wa barua kwenye Kuomba kazi,kuwa Mwakilishi katika masuala mbalimbali unayoyafanya kulingana na ujuzi wako wa ziada ulionao kwenye taasisi,semina,matamasha, n.k
9. Kuacha woga na hofu bali kujiamini na kuyaendea mambo. Ukisikia fursa ni jambo la muhimu na linakuhitaji wewe ujipange na ujue namna ya kuliendea na mahitaji yake ya msingi.
10. Fanya kwa Malengo katika jambo lako. Ukipata nafasi jua malengo ya kazi na yako binafsi hii itakusaidia kufanya kitu kwa bidii na kwa mafanikio makubwa.

Upvote
0