Mambo 10 niliyoyaona Leo Singida Vs Simba

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
1. Simba imeshinda lakini bado Chemistry haijapatikana
2.Che Malone Fondoh ni ukuta wa Yericko kweli sio masihara
3.Kibu Dennis amebadilika sana, hakuna mchezaji wa kumweka benchi awe wa
kigeni au wa nje
4.Loius Micquisone amebaki jina tu
5.Yule Maroon Tchakei ni fundi hasa wa mpira
6.John Bocco anaikosesha sana Simba ushindi, Robertinho awe anamuingiza
kipindi cha 2 kama anampenda
7.Robertinho anapaswa kumuamini Shaaban Chilunda
8.Robertinho anapaswa kuamini kiungo Abdallah Hamis badala ya Kanoute
9.Simba isipobadilisha aina ya uchezaji, Al Ahly watatuadhibu tarehe 20 hapa hapa kwa Mkapa
10.Licha ya kufunga goli Mosses Phiri bado ni mzito na kiwango kimeshuka.
 
MTAPIGA Kila kelele.
WAKUBWA TULIISHA WAAMBIA MJIANDAE KISAIKOLOJIA. TULIYOYASHAURI WAKATI NA KABLA YA USAJILI YALIPUUZWA.

 
We jamaa una kisirani
 
Umeongea vema kama shabiki.

Vinginevyo kocha ndiye anayejua ni nani anayefaa kucheza wakati gani kulingana na aina ya mazoezi yaliyofanyika.

Uzuri ni kwamba kila shabiki anadhani anaweza kufundisha mpira, lakini ukweli hauko hivyo.
 
Nafasi ya Miqson bora tungesajili namba sita ya maana pale kati
 
Badilisha heading ibaki simba tu...Naona walikuwa wanacheza wenyewe bila upinzani
 
Kote tuko pamoja, ila hapo #8 hapana Abdallah Hamis hapana, mengine niko na wewe 100%
 
Umeongea vema kama shabiki.

Vinginevyo kocha ndiye anayejua ni nani anayefaa kucheza wakati gani kulingana na aina ya mazoezi yaliyofanyika.

Uzuri ni kwamba kila shabiki anadhani anaweza kufundisha mpira, lakini ukweli hauko hivyo.
Halafu tunataka mawazo ,mipango na mbinu zetu za kijiweni ,ndio zitumike na kocha mwenye LESENI A CAF PRO
 
Nafasi ya Miqson bora tungesajili namba sita ya maana pale kati
Acheni mihemko yakimpira hivi unajua uongiaji wa miquisson ulileta mikimbio na movement zenye madhara san langoni mwa wapinzan akilink na mosses phiri au nyie mnaangalia madhaifu tu mazuri hamuangalii pasi ya goli ilitok kwa miquesson kwasasa ni bora yake kuliko chama anaepoteza pas10+ kwenye mechi za mkoan sabb y poor control
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…