Mambo 10 niliyoyaona Leo Singida Vs Simba

Ukiiangalia Simba kiufundi sasa hivi inavyocheza na aina ya wachezaji waliopo ni vitu viwili tofauti. Ukiondoa nafasi ya kungo mkabaji asili ambaye kosa lilifanyika wakati wa usajili makosa yote yaliyobaki ni makosa ya benchi la ufundi.

Kosa la kutokuwa na kiungo mkabaji asili linarekebishika lakini ndilo linawafanya mabeki wakati wawe wafikike kiurahisi sana ndio maana mpaka sasa Simba kupata "clean sheet" ni tatizo sana. Udhaifu wa kukosa kiungo mkabaji asili huwa unatatuliwa kwa timu kukaba pamoja na kushambulia pamoja na hii inahitaji sana wachezaji wawe na utimamu wa mwili. Tujiulize je wachezaji wa Simba wana utimamu wa mwili kwa asilimia 100 jibu ni hapana. Wachezaji wa Simba wakifika dakika ya 60 kwenda mbele timu inakata upepo. Kwa hiyo kocha wa viungo ana kazi kubwa ya kufanya. Na kuhusu Adel Zrane ambaye ndiye aliifanya Simba ikawa ngangari kwenye utimamu wa miili ya wachezaji nimeuliza sana alifanya dhambi gani mpaka viongozi hawatki kumrudisha. Anyway hili tuwaachie viongozi wao ndio wanajua sababu.

Kosa lingine kubwa kwa sasa ni kikosi cha Simba kuwa kikubwa kuliko uwezo wa benchi la ufundi kiasi benchi la ufundi halijui kiufundi nani anafaa kuanza mechi fulani nani aingie nani atoke zaidi utakuta Kocha na wasaidizi wake wamekaririr tu baadhi ya wachezaji bila kuangalia mahitaji ya timu kwa mechi husika.. Benchi la ufundi halijui hii mechi inahitaji mshambuliaji mrefu tumchezeshe Boko au mechi hii inahitaji mtu wa "pressing" tumchezeshe Baleke vivyo hivyo kwa nafasi nyingine uwanjani. Wao Boko akifunga basi ni huyo huyo hata mechi zinazohitajika awepo Baleke. Imefika mahali nadhani watu wengi hawajaliona hili Simba inapokuwa inaongoza mwishoni sasa hivi kila mechi lazima benchi la ufundi likimbilie kuingiza watu wa kulinda matokeo mwishoni mwa mchezo. Robertino aambiwe kabisa hii sio Vipers hii ni Simba Lunyasi ambayo ushindi mnono unapatikana mapema wa goli nyingi halafu kinachofuatia ni burudani zile dakika 20 za mwishoni badala ya mashabiki kubaki wengine wanomba dua, wengine wanashika roho mkononi, wengine wanaminya sehemu za siri, wengine wanazima TV/Radio majumbani, wengine wanatoroka vibanda umiza n.k.

Kosa lingine kubwa kiufundi ninaliona ni kuhusiana na nafasi ya mchezaji namba 10 pale Simba. Bahati nzuri sana Simba sasa hivi inao wachezaji wengi mafundi wanaoweza kuicheza hiyo nafasi kiufasaha na kuitendea haki. Kwa mfano goli la pili la Simba dhidi ya Singida Fountain Gate ndio aina ya magoli Simba huwa inafunga lakini sasa hivi yamekuwa nadra sana. Hiyo yote inchangiwa na benchi la ufundi kumng'ang'ania Saido wakati uwezo wake wa kuichezesha timu "one two" au kupunguza wachezaji wawili watatu pale mbele umepungua sana. Kwa kawaida mchezaji anayecheza namba kumi anakuwa jukumu kubwa sana lu kuchukuwa mipira katikati kupunguza watu wawili watu ili kuitembeza timu kwenda mbele kwa kasi, kuwahi mipira yote inayondondoka baada ya mshambuliaji kuruka na mabeki wa timu pinzani, kuwahamisha mabeki wa timu pinzani kushoto na kulia lakini huyo mtoto pendwa wa Robertino hili linamshinda. Na mbaya zaidi hata pasi anazopewa na wenzake asilimia kubwa huwa zinaishiai miguuni kwake.

Mwisho ushauri wa bure kwa viongozi wa Simba tafuteni video zote za Simba wakati wanamaliza msimu uliopita mzitazame mara mbili mbili na hasa ile mechi ya Simba dhidi ya Yanga. Halau liiteni benchi la ufundi waonyesheni hizo video halafu muwambie Simba ndio inatakiwa icheze namna ile. Kama hawawezi kufanya hivyo basi tutabaki tunaamini kuwa Mgunda ndiye aliyefanya boli liwe linatembea na ile "pressing" ya akina Baleke waliyokuwa wanakabia juu na viungo wakina Muzamiru wanafika kwa wakati kutibua mipango ya viungo wa timu pinzani, mabeki na hata makipa walikuwa hawana kazi kubwa kiasi kulikuwa na " clean sheets" za kutosha. Vinginevyo viongozi wasione aibu wamrudishe Mgunda kwenye nafasi yake ya kocha msaidizi.

Ni mtizamo tu.
 
Eti baadhi ya wachezaji huwa wana tabia za kulogana .... sio simba tu hata kwa timu zingineee
 
1. Simba kila mara ina pangiwa marefa mademu

2. Simba kila mara ina cheza mechi baada ya Mechi ya Yanga. Na siyo kubadilishana. Hii ni upangaji wa Matokeo.
3. Simba ina bebwa. Goli la Singida lilikuwa halali. Goli Ba Bocco dhidi yq Tz Prisons ni Offside Kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…