Mambo 10 usıyoyajua kumhusu BRUCE LEE

Mambo 10 usıyoyajua kumhusu BRUCE LEE

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
BRUCE LEE.jpg

Mambo 10 usiyoyajua kumhusu Bruce Lee

Wapenzi wengi wa filamu wanamtambua na kumuenzi sana marehemu mwigizaji Bruce Lee kutokana na weledi wake kwenye filamu na sanaa ya Kung Fu zilizowazingua wengi kwenye taaluma yake ya uigizaji. Bruce Lee (1940 - 1973) aliyejulikana kwa majina kamili kama Lee Jun-fan alisifika sana kwa kubuni mtindo wa kupigana kwa Kungfu kwa jina ‘Jeet Kune Do’ na kuigiza filamu nyingi.

Kando na kuwa alipenda sama mchezo wa ndondi, kuna mambo mengi ya kushangaza ambayo yalizingira maisha ya Bruce Lee wakati wa taaluma yake ya uigizaji na karate ambazo zitakushangaza.

1. Bruce Lee alifanya mazoezi kwa makonde 5,000 kila siku ili kuwa na ujuzi wa juu zaidi katika kupigana. Alikuwa na bidii na hilo linaeleza kwa nini makonde yake yalikuwa mazito kwa wapinzani wake kwenye filamu na mapigano. 2. Bruce Lee alikuwa akiitoboa mikebe kwa vidole vyake. Siku za zamani, mikebe haikutengenezwa kwa mabati nyepesi, lakini aliweza kuvifungua kwa vidole vyake. Aliwahi kujeruhiwa kwenye vidole vyake alipokuwa akionyesha ujuzi wake kwenye maonyesho ya ‘Big Boss’ na hiyo ndiyo sababu alifunga vidole vyake kwa bandeji kwenye filamu nyingi alizoigiza. 3. Bruce Lee alikuwa na kasi ya aina yake. Alionyesha kasi yake kwa kuweka sarafu mikononi mwa mtu na kuichukua kabla ya mtu huyo kuifunika kiganjani ili kumzuia kuitwaa.

4. Viungo vya kutoa jasho kwenye makwapa vya Bruce Lee viliondolewa kwa upasuaji mwaka wa 1972.

Alisemekana kukerwa na kutokwa kwa jasho jingi kwenye makwapa na jinsi jasho hiyo ilivyoonekana vibaya, hali iliyomfanya kufanyiwa upasuaji huo.

Sijui jinsi upasuaji wa aina hiyo unavyoweza kufanyika.

5. Akiwa mvulana barobaro, Bruce Lee alikuwa mtoto nyota wa uigizaji huko Hong Kong.

Alikuwa ameigiza filamu 20 alipokuwa na miaka 18.

6. Bruce Lee aliandika mashairi mengi ambayo zilijumuishwa kwenye kitabu chake ‘The Tao of Jeet Kune Do’.

Marafiriki zake waliarifu kuwa alipenda sana kuandika mashairi kila mara. Waliomuita msanii hawakukosea.

7. Bruce Lee alitembea na bunduki aina ya 357 Magnum. Hilo lilikuwa kwa sababu ya usalama wake kwa kuwa ikiwa kila mtu alitaka kupigana naye ili kudhihirisha ubabe wao, basi alihofia maisha yake kama mtu yeyote yule.

Jesse Glover alidhibitisha kuwa alikuwa na ujuzi mkubwa na uhakika wa kipekee wa kufyatua risasi kwa kutumia bunduki.

8. Kifo cha Bruce Lee bado kinaaminika kuwa cha kutatanisha. Madai mengi yaliibuka zikiwemo kutumia bangi kama ilivyodhaniwa na baadhi ya madaktari wake, kuuawa kwa sumu ambapo watu wengine waliamini kuwa Raymond Chow alitaka auawe.

Chanzo cha kifo chake bado kinajadiliwa na jamaa, marafiki na mashabiki wake.

9. Bruce alipenda kusoma sana na kupekua vitabu kutoka kwenye jalada hadi ukurasa wa mwisho.

Alikuwa na maktaba ya zaidi ya vitabu 2,000.

Alijulikana kwa kusoma kitabu, kutazama runinga na kuinua kifaa cha uzito cha kufanya mazoezi kwa wakati mmoja!

10. Bruce Lee hangeweza kuogelea.

Kakake mdogo, Robert na dadake, Phoebe walifichua kuwa Bruce alichukia maji na hangeweza kuogelea.
Ufichuzi huo ulidhibitisha udhaifu wake mkubwa uliohusiana na maji.

TAO OF JET KUNE DO.jpg

MAISHA YA BRUCE  LEE.jpg
 
Samahani Sana mkuu naomba kusoma ile hadithi yako ya queen of the goriller
 
Kakake mdogo, Robert na dadake, Phoebe walifichua kuwa Bruce alichukia maji na hangeweza kuogelea.
Ufichuzi huo ulidhibitisha udhaifu wake mkubwa uliohusiana na maji.

Tuseme kwa kuogopa maji, alikuwa haogi???🤣

Nadhani huyu Bruce alikuwa mtumiaji wa aina fulani za PEDs na labda hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha kifo chake, PEDs inaweza kusababisha Cardiac arrest.

PEDs ni dawa zinazotumiwa na wanamichezo kuwaongezea nguvu, kasi na ustahimilivu katika michezo.

Kumbuka katika miaka hiyo hakukuwa na sheria kali dhidi ya dawa hizo na isitoshe hazikuwa maarufu kama zama hizi za utaalamu mkubwa wa sayansi comparatively.
 
Kama umwangalia muvi za Ip Man utajua kilichomua Bruce ni nini..
Nasubir kwa hamu nione kama wataeleza kwenye muvi inayofuata!
 
Action moves za siku hizi zimejaa camera tricks, zama za kina Bruce hakukuwepo na camera za aina hiyo hivyo unachokiona (movents) almost ni hizohizo hakuna edition yoyote.
 
Fafanua vizuri mkuu nikuelewe maana umekuja na point vizuri
 
Ya ngapi hiyo ambayo itakayofuata je? Ni baada ya boyk vs don yen au ipi tena wakati hiyo waliandika final
 
Ni kweli ulilosema.
Lakini mimi nazungumzia historia halisi ya Bruce na Ip man (mwalimu wa Bruce)
Habari za kuuliwa kwa madawa ni fix, ndio maana nimesema kama wachina watatoa muendelezo wa Ip Man baada ya 2019 basi stori itakua inamuhusu Bruce, maana ip man alikufa kwa kansa ya mapafu. Muvi hii ni simulizi ya kweli labda vitu vingine wanaweka ili kunogesha stori..
Kama watatoa muendelezo basi muvi itagusia kifo cha bruce. Ndio najiuliza je wataamua kuutoa ukweli halisi?
Kifo cha bruce ni sababu ya kupeleka Tamaduni za Kichina America...wakati ilikua hairuhusiwi na Mwalimu wake Ip Man alibariki swala hilo
Nini kipo nyuma ya vifo vya hawa masta, ni njama au vifo vya kawaida.?
 
Nimekuelewa kwani hata kwenye ile filamu ilionekana ile jumuiya yao kule Marekani walipinga sana harakati za mwanafunzi wa Ip Man (Bruce)
 
Ni kweli ulilosema.
Lakini mimi nazungumzia historia halisi ya Bruce na Ip man (mwalimu wa Bruce)
Habari za kuuliwa kwa madawa ni fix, ndio maana nimesema kama wachina watatoa muendelezo wa Ip Man baada ya 2019 basi stori itakua inamuhusu Bruce, maana ip man alikufa kwa kansa ya mapafu. Muvi hii ni simulizi ya kweli labda vitu vingine wanaweka ili kunogesha stori..
Kama watatoa muendelezo basi muvi itagusia kifo cha bruce. Ndio najiuliza je wataamua kuutoa ukweli halisi?
Kifo cha bruce ni sababu ya kupeleka Tamaduni za Kichina America...wakati ilikua hairuhusiwi na Mwalimu wake Ip Man alibariki swala hilo
Nini kipo nyuma ya vifo vya hawa masta, ni njama au vifo vya kawaida.?
Hapo nimekupata sana
 
Fafanua vizuri mkuu nikuelewe maana umekuja na point vizuri

Maana ni hii; zama za kina Bruce lee katika miaka ya 70 actions nyingi walizo cheza zilikuwa ni za hakika (real), mfano akirusha mguu au ngumi speed ya movement ya mguu au mkono utakayoona katika move karibu ni speed hiyo hiyo aliyo act nayo kipindi move ilipochukukiwa, hii ni tofauti na moves za siku hizi ambapo moves hufanyiwa edition za kuongeza speed nk, ili kufanya zivutie zaidi.
 
Sawa sawa 🤝
 
Huyu mwamba alikua na kipaji cha kipekee.
 
Bruce alikufa ghafla kwasababu mwili wake ulikuwa na mafuta chini ya asilimia moja post moterm report ilionyesha hivyo....
 
Back
Top Bottom