Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Unakutana na Polisi kila wakati, na unawaona wakifanya kazi nyingi, kama vile kuongoza magari, kuwalinda viongozi, kudhibiti makundi ya watu, kusindikiza watuhumiwa Mahakamani, kufanya upelelezi, kutoa ushahidi Mahakamani, kupokea malalamiko vituoni, kubaini, kuzuia au kukamata wahalifu, kupambana na wahalifu na kazi nyinginezo nyingi. Pia Umesikia na unaendelea kusikia mengi kuhusu Polisi kupitia magazeti, televisheni, radio na maneno ya watu.
Aidha, kila mtu ana mtazamo wake juu ya Polisi. Hata hivyo, watu wengi bado wanauelewa mdogo sana kuhusu Polisi.
Katika nchi yenye demokrasia Polisi siyo wakala wa serikali iliyopo madarakani ambao wanavaa sare zao ili kuwakandamiza wananchi na kuwadhibiti, bali Polisi ni chombo kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria ili kuwalinda raia na mali zao.
Polisi wanatoa huduma muhimu ambazo kisheria zina jukumu la kumlinda na kumwangalia kila mmoja wetu kwa hiyo kwa kiwango fulani wanafanana na taasisi nyingine maathalan kikosi cha zimamoto au mamlaka ya kodi ya mapato.
Kwa kadiri Polisi walivyo na wajibu kwa wananchi, nao wananchi wanao wajibu kwa Polisi. Raia wema wenye kuwajibika hawapaswi kuwaogopa au kuwachukia Polisi au kuogopa kwenda kituo cha Polisi pale wanapokuwa na matatizo. Bali
wananchi na Polisi wanatakiwa wafanye kazi pamoja katika kuzilinda sheria.
Hivyo basi, ni muhimu ukazielewa kazi za Polisi, jinsi wanavyozifanya na changamoto wanazokumbana nazo. Pia ni muhimu ukajua jinsi taasisi hii inavyoonekana na ukomo wa madaraka na kazi zao.
Aidha, ni muhimu kwako kujua haki na wajibu wako ili pasiwepo yeyote si Polisi wala wewe raia atakayevunja sheria pasipo kuchukuliwa hatua yoyote. Na hii ndiyo maana halisi ya utawala wa sheria.
Kijitabu hiki ni mwongozo kwa wewe kulijua Jeshi la Polisi. Ni kwa kulijua vizuri Jeshi la Polisi tu ndipo tunapoweza kuongea kwa kujiamini, na kukemea maovu yanayojitokeza katika jamii yetu, na kwa kufanya hivyo hali ya mambo itabadilika.
Kijitabu hiki kilichoambatanishwa hapa chini imechapishwa na kuletwa kwako kwa matumaini kuwa kitakusaidia kujua mambo mbalimbali kuhusu Polisi na kazi zao na utatumia elimu hiyo kudai huduma bora za kiPolisi ambazo wote tunastahili kupata.