Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
1. Mchezo ulikuwa super ingawa mashabiki walikuwa na hofu sana walipoona mabadiliko ya kikosi, kikosi alichokuwa akikipanga mara kwa mara kocha Fahdu kiliwafanya wapinzani wajue namna ya kuwakabili ndani na nje ya uwanja.
2. Simba leo ilikuwa faster sana kutokana na kiungo Fernandez Mavambo kumiliki vizuri sehemu ya katikati akishirikiana na fundi wa mpira Yussuph Kagoma.Mavambo hata hivyo apunguze kujisahau, anaweza kukaa na mpira halafu ghafla akaporwa na adui, hilo alifanyie kazi tarehe 8.
3. Duchu amecheza vizuri sana na huenda ikawa safari ya mwisho kwa Kevin Kijiri ingawa to me naamini Kijiri bado mzuri sana, cjui kwann bado kuna hasira ya kujifunga ile mechi vs Yanga.Ila Duchu awe makini sana ukabaji wake ndani ya penati box vinginevyo kuna siku atakuja kusababisha penati ya kijinga kama leo, kama sio refa kukausha ilikuwa inawekwa kwenye kisanduku ile.
4.Valentine Nouma ni beki mzuri sana, ana nguvu, ana mashuti, ana krosi, mimi sioni hofu yoyote tarehe 8 akasimama kushoto kusukuma mashambulizi badala ya Tshabalaa ambaye anaelekea kufika mwisho.
Soma Pia: FT | Coastal Union 0-3 Simba SC | NBC Premier League | Sheikh Amri Abeid Arusha | 01 March, 2025
5.Abdulrazack Hamza anasifiwa ni beki mzuri, ni kweli lakini ajirekebishe.Yuko slow sana na anachelewa kufanya maamuzi.Hamza hawezi kupiga pasi ndefu, yeye akipewa mpira anamwangalia Camara au Malone/Chamou au Kagoma au Kapombe au Tshabalala au Nouma, huwezi muona Hamza anapewa mpira anairusha kwa Mpanzu au Ateba kama alivyokuwa akifanya Serge Wawa.
Halafu apunguze kujiamini kwa sababu hana kasi kama leo angetuingiza chaka kwa uzembe wake.Mechi ya kwanza Hamza alimshika Dube kwa sababu ya spidi akala kadi ya njano, afanyie sana kazi suala la spidi na kurudisha mipira nyuma.
6.Aisee Joshua Mutale kwa kweli mpira hapa bongo umemkataa, kuna wakati nilikuwa namhisi vibaya Edwin Balua kuwa kamchezea nn ili nyota yake ife.Mutale nini kimemkuta.Kama kuna kamba amefungwa zifunguliwe kama alivyofunguliwa Mukwala.
7. Elie Mpanzu ni mashine haihitaji kelele nyingi kujua mwamba huyu anajua boli, siku Mpanzu acheze na Feitoto, kushoto Kibu, katikati Chama na Jonathan Sowah, mamake walai.
8.Jeans Charles Ahoua ni mchezaji mzuri lakini mechi kubwa kubwa kama hii na Yanga haiwezi.Hebu tuwe wa kweli ukimwangalia Ahoua anacheza vile utaweza kumfananisha kweli na Kibu anavyocheza au Mpanzu? Akianza na Yanga itakuwa faida kubwa kwao Yanga.
9.Mukwala alikuwa amepigwa pini, pini zimefunguliwa sasa hivi pini amepigwa Ateba, tunaomba pini hizo zifunguliwe kwa Ateba.Vinginevyo nipeni mimi nimpeleke kule kwa watu wangu, hamtaamini.
10.Wale Coastal wana wachezaji wawili wanastahili kuchezea Simba, kale ka winga Bakary Seleman aliyeingia kipindi cha pili na Semfuko Charles fundi sana wa mpira yule kijana, anaweza kusaidiana na Yussf Kagoma bila shaka yoyote.
11.Tarehe 8 Machi ni Simba na Yanga, tafadhalini viongozi wetu, kufungwa na Yanga mara ya 6 mfululizo halafu nyie mnaona sawa tu haikubaliki, haikubaliki, haikubaliki.Narudia, kufungwa na Yanga mara ya 6 mfululizo iwe mwisho tarehe 8 Machi, wakitufunga hatutakuwa na sababu tena ya kulalamikia GSM wala nini.