Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Miezi 7- 9 ya ujauzito huwa kwa kiasi kikubwa salama bila ya kuwa na dhoruba zozote. Mpaka sasa tumbo limeshakuwa kubwa na umeshasikia mtoto akicheza tumboni.
Ndani ya miezi 7-9 ya ujauzito mtoto hupata mabadiliko makubwa yanayohitimisha ukuaji wake. Mtoto Huongezeka uzito kutoka kilo 1 mpaka kilo 3.2 kwa wastani na viungo hukamilisha ukuaji ili aweze kuhimili ukuaji nje ya tumbo la mama.
Katika kipindi hiki cha tatu cha ujauzito (third trimester), Baadhi ya dalili za mwanzo za ujauzito zinaweza kurudi au kujitokeza zaidi.
Pia Ni kipindi ambacho unaweza kuwa umechoka, Ukitamani wakati ufike haraka ujifungue.
• Mjamzito anaweza kutegemea yafuatayo katika kipindi hiki:
1. Mtoto kuendelea kucheza.
~ Kipindi cha pili cha ujauzito (second trimester) ulianza kuhisi mtoto akicheza tumboni, katika kipindi hiki utasikia zaidi mtoto akizidi kucheza(kujigeuza, kurusha mikono na miguu). Wakati mwingine anaweza kuwa anacheza kiasi cha kukuamsha kutoka usingizini au kusababisha ukose usingizi. Unaweza kuona movement za mtoto nje ya tumbo, ukazigusa na kuzihisi.
2. Matiti kuendelea kukua na kuanza kutoa maziwa.
~ Muda wa kujifungua unapokaribia, mwili wako nao unajiandaa kuweza kumlea mtoto. Matiti yako yatendelea kukua, ili kuwa tayari kuanza kunyonyesha. Yanaweza kuanza kutoa maziwa ya njano hivi, haya ni muhimu kwa siku za mwanzo za mtoto akizaliwa.
3. Tumbo kuendelea kukua.
~ Mtoto tumboni anaendelea kukua mpaka kufikia wastani wa kilo 3.2 katika wiki ya 37. Kukua huku husababisha tumbo kuendelea kuwa kubwa, likikua kuelekea juu na baadae kushuka chini wakati wa kujifungua unapokaribia.
4. Kupata mikazo ya tumbo.
~ Utaanza kupata mikazo ya tumbo isiyouma ambayo hujulikana kama Braxton Hicks contractions, hutokea kwa muda mfupi na kuacha. Tofauti na mikazo ya uchungu (labor contractions), mikazo hii huwa haiumi na hujitokeza bila wakati maalumu. Endapo unapata mikazo inayouma na kuongezeka Kadri muda unavyoenda wahi kituo cha afya mapema.
5. Kutokwa na majimaji ukeni.
~ Mabadiliko ya kihomoni katika kipindi hiki huchangia kuongezeka kwa majimaji ya uke. Huwa ni ya kawaida yasiyowasha wala kuwa na harufu mbaya. Onana na daktari wako haraka endapo maji mengi kwa ghafla, yenye damu damu harufu au kuwasha Yatatoka.
6. Maumivu ya mgongo na kiuno.
~ Mtoto wako anavyozidi kukua, homoni hulegeza misuli ya mifupa ya kiuno na uzito wa mtoto kuja maeneo ya kiunoni. Kaa kwenye kiti chenye support nzuri, epuka uvaaji wa viatu virefu na pata godoro zuri la kulalia. Ikiwa maumivu ni makali yakiambatana na dalili nyingine, onana na daktari mapema.
7. Kukojoa mara kwa mara.
~ Kipindi hiki utapata hali ya kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine mkojo kuvuja polepole bila wewe kujua. Inatokana na tumbo la uzazi kukandamiza kibofu cha mkojo na hivyo mkojo kutoka mara kwa mara. Ni vizuri ukavaa nguo za ndani za pamba na panty liners na kufanya mazoezi ya Kegel ili kudhibiti mkojo unaovuja. Endapo unapata maumivu wakati wa kukojoa, maumivu chini ya tumbo, homa na kukojoa mara nyingi zaidi ya kawaida, onana na daktari kwani zinaweza kuwa dalili za UTI.
8. Kiungulia.
~ Katika kipindi hiki tumbo la uzazi hukua kuelekea juu na hivyo kulisukuma tumbo la chakula kutoka katika nafasi yake, hivyo kusababisha asidi ya tumboni karudi kwenye mrija wa chakula na kusababisha kiungulia. Pata mlo kidogo lakini mara kwa mara, punguza juisi zenye machungwa, ndimu au malimao. Kiungulia kikikusumbua sana onana na daktari wako juu ya dawa.
9. Kutopata hewa ya kutosha.
~ Kutopata hewa ya kutosha au kushindwa kupumua vizuri hi hali inayojitokeza mara kwa mara katika kipindi hiki. Hii inatokana na tumbo la uzazi kusukuma mapafu na kuongezeka kwa mahitaji ya oksijeni. Mazoezi ya kutembea na kulalia mito inaweza kusaidia kupunguza hali hii. Endapo unapata shida kupumua kiasi cha kushindwa kutembea au kufanya hata shughuli nyepesi, onana na daktani wako.
10. Mishipa ya damu kujitokeza kwenye ngozi.
~ Kuongezeka kusambaa kwa damu mwilini kunaweza kusabababisha mishipa ya damu kujitokeza kwenye ngozi za sehemu za tumboni, miguuni na utumbo mpana. Hujulikana kama varicose veins kwa kitaalamu. Mishipa inayojitokeza sehemu ya chini ya utumbo mpana (rectum) huweza kusababisha kupata choo chenye damu. Hakikisha unapata maji ya kutosha na chakula chenye kambakamba kwa wingi.
11. Dalili za hatari.
~ Ukiona mojawapo ya dalili hizi wakati huu wa ujauzito onana na daktari wako haraka.
• Kutokwa na damu ukeni.
• Maumivu makali ya tumbo•
• Kutokwa na majimaji au ute mwingi zaidi ya kawaida ukeni.
• Mtoto kuacha kucheza tumboni.
~ Kwa Msaada na Ushauri Zaidi Wa Magonjwa Mbali Mbali , Wasiliana Nasi Kupitia +255655662181 au +255769600821 - ( What's sap & Call ).