Mambo 13 usiyoyajua kuhusu mnyama kakakuona

Mambo 13 usiyoyajua kuhusu mnyama kakakuona

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Inakadiriwa kuwa mnyama huyo huishi kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika pori. Lakini hiyo ilikuwa inafahamika zamani kipindi ambacho mnyama huyo alikuwa anaonekana tofauti na sasa.
48acd354e5173296381c9753dc09450e.jpg

1:KUNA AINA 8 ZA KAKAKUONA DUNIANI.
Aina hizo nane za kakakuona zimetoka katika familia inayofahamika kama manidae. Aina hizo za kakakuona zipo duniani kwa zaidi ya miaka 80 milioni ya mabadiliko yao.
Kati ya hizo, aina nne za kakakuona zinapatikana katika Bara la Ulaya na wengine barani Afrika. Hawa wanafahamika kwa majina ya tree kakauona, giant kakakuona, cape kakakuona na kakakuona wenye mkia mrefu.

2:ULIMI MREFU KULIKO MWILI WAKE.
Kakakuona ana ulimi wenye urefu unaozidi mwili wake.
Akiurefusha kwa kuutoa nje ya kinywa unafikia urefu wa sentimita 40.
Ulimi huo ambao pia unanata, huutumia kwa ajili ya kukusanya wadudu ambao ndiyo mlo wake wa pekee, hana mwingine zaidi ya huo kutokana na kukosa meno.

3:NDIYE MNYAMA PEKEE DUNIANI AMBAYE MWILI WAKE UMEFUNIKWA NA MAGAMBA MAKUBWA.
Magamba yanayofunika mwili wa mnyama huyo ni makubwa kuliko ya viumbe wengine. Magamba hayo kitaalamu yameundwa na kitu ninachoitwa ‘keratin’, ambayo yanafanana na yale yanayounda kucha za binadamu.
Asilimia 20 ya uzito wa mwili wa mnyama huyo unatokana na magamba.
Kakakuona hutumia magamba hayo kama silaha ya kujilinda dhidi ya maadui.

4:MAANA YA JINA "KAKAKUONA"
Maana ya jina hilo ilianzia nchini Malaysia, Indonesia na Brunei likimaanisha "kitu kinachojikunja". Kakakuona hupenda kujikunja kama mpira.
Hiyo ikiwa kama mbinu anayotumia kujilinda dhidi ya maadui.
Licha ya kuwa hutumia mbinu hiyo kujilinda, lakini anapojikunja ndiyo inakuwa rahisi kwa watu kumkamata na kumbeba.

5:HUISHI JUU YA MITI NA KWENYE MASHIMO.
Baadhi ya kakakuona huishi juu ya miti, wengine hujichimbia ardhini na kuishi ndani ya mashimo.
Wengi wanaoishi juu ya miti ni wale wenye mikia mirefu wanaopatikana barani Afrika.
Wengine huchimba mashimo marefu ardhini na kuishi humo ili wasikutane na binadamu.

6:NI MWEPESI KUSHAMBULIWA NA WANYAMA WENGINE.
Ukiachilia mbali adui yao mkubwa ambaye ni binadamu, adui wengine wa wanyama huyo ni jamii ya chui na simba.
Hata hivyo, maadui hao hushindwa kuwashambulia kakakuona kutokana na namna wanavyojilinda kwa kujikunja na jinsi mwili wao ulivyo na magamba. Kutokana na hali, hiyo inakuwa vigumu kwa simba au wanyama wengine kuwashambulia kwa kuwala.
f583afbae1c22478b71e8330ec5fccc5.jpg

7:HAKUNA ANAYEFAHAMU MIAKA ANAYOISHI.
Inakadiriwa kuwa mnyama huyo huishi kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika pori.
Lakini hiyo ilikuwa inafahamika zamani kipindi ambacho mnyama huyo alikuwa anaonekana tofauti na sasa.
Hata hivyo, kutokana na aina ya maisha ya wanayoishi, inasemekana kuwa wanaweza wasiishi miaka mingi, licha ya kuwa bado haifahamiki kwa sasa, inawezekana wakaishi kwa miaka 20.

8:HUTEMA SUMU KALI KAMA TIMDIKALI.
Kakakuona akiona adui hujilinda kwa kujikunja, lakini akiona hali inakuwa mbaya zaidi, hutema sumu kali mithili ya tindikali inayoweza kumdhuru adui.
Pia, wakati mwingine hunyoosha mkia wake na kuuzungisha na kumkata adui aliyekaribu yake.

9:MAMILIONI WAMEUAWA NA KUUZWA NDANI YA MIAKA 10.
Inakadiriwa kuwa kakakuona 100,000 hukamatwa kila mwaka barani Afrika na Ulaya na kuuzwa.
China na Vietnam ndizo nchi maarufu ambazo nyama na magamba yake huuzwa.
Kutokana na hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hifadhi za Asili (IUCN) limemweka kakakuona kwenye orodha ya wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka duniani.

10:HAWAONI VIZURI.
Ni aina moja katika ya nane za kakakuona wenye uwezo wa kuona vizuri hasa muda wa mchana.
Hawa ni wale wanaopatikana barani Afrika.
Wengine hawana uwezo wa kuona vizuri kutokana na kuwa na macho madogo.

11:WANA UWEZO MKUBWA WA KUNUSA NA KUSIKIA.
Licha ya wengine kuwa na macho madogo na kushindwa kuona vizuri, kakakuona ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kusikia sauti yoyote kwa haraka kwa sababu masikio yake yameinuka. Pia, ana uwezo mkubwa wa kunusa harufu yoyote.

12:NI VIGUMU KUJAMIIANA
Tofauti ilivyo kwa baadhi ya wanyama, upande wa kakakuona tendo kujamiiana ni gumu kutokana na tofauti za kimwili kati ya jike na dume. Mwili wa kakakuona dume una uzito mkubwa zaidi ya asilimia 50 ukilinganishwa na jike.
Mbali na hivyo, hawana msimu maalumu kukutana na kujamiiana, tofauti na ilivyo kwa wanyama wengine kama binadamu.

13:UHUSIANO NA WANYAMA WENGINE.
Imezoeleka kuwa, mnyama huyo huwa karibu na wanyama wengine wa jamii yao, kwa maana ya wale wanaokula wadudu.
Hata hivyo, hivi karibuni wanasayansi wamebainisha kuwa wamekuwa karibu na wanyama kutoka jamii nyingine kama wale wanaokula nyama.

[HASHTAG]#IFAKARA[/HASHTAG] BABY [emoji6] [emoji6] [emoji6] [emoji6]
 
Inabidi tu nikubali maana kakakuona mwenyewe nasikia ana mizengwe yake pale itokeapo ameonekana kitaa.
 
weeee usitubebee akil miaka milion.80 nan kasema yesu enyew ana miaka 2017 sa hivi afu ww unatuambia miaka milion 80 nan kasema kulikuwa na dunia
 
Mbona sijaona umeandika kama wana uwezo wa kubashiri hali au kitu fulani? Kwa mfano tukiwa wadogo tuliwahi kuambiwa kuwa ukiwawekea vitu kama vile maji, mazao n.k wakiingia katika moja Wapo ya hivyo vitu basi ni lazima mwaka huo kutakuwa na upatikanaji wa hicho kitu kwa wingi. Je ni kweli?
 
Habari nzuri, lakini kwao tendo la ndoa haiwezekani? Mbona kuna jike na dume? Ina maana Mungu aliumba idadi moja isiyoongezeka
 
Nikiangaliaga ile movie ya jangobook,kakakuona anamwambia dubu, mbona unamtesa huyo dogo nyuki wana muuma,dubu akamwambia "wee! Hayakuhusu"

HahahahahahahHahahahaha
 
Kuna ujinga nililetewa mwaka huu kwamba kuna jamii ya huyu mnyama anasumaku yaani anashika wembe na sindano, anabadili maji rangi na ukimsogezea Kioo kinapasuka. Na wakadai ukimpata huyo anauzwa million zaidi 100, mwanaume nkaingia pori huko kwa wamasai nikazunguka sana wilaya ya Ngorongoro maeneo kama (Ololosokwan, Soiti Sambo na Waso mjini) ikawa kila naye mpata hana hizo tabia ikabidi wamasai wanipeleke mbugani Serengeti tumelala huko ifadhini kwa muda wa siku 6 nimewapata 3 wote hawana hizo tabia. Nikaambiwa kuna mtu yuko Engaruka anajua huyo mnyama alipo ikabidi niende huko nafika masai ananiambia yupo ila yuko wilaya ya Simanjiro, mwanaume nkajikaza tukafunga safari mpaka huko porini tukafika kwenye maboma ya Masai wakanipatika kwenye pikipiki tukaenda kuvizia kwenye shimo lake maana anarudi kuanzia saa 2 usiku na anaondoka saa 11 alfajiri. Siku ya 4 ndo tukambaatisha wakati anataka kuingia shimoni, Duuuu! Kweli kumwekea maji ya chupa yakabadirika rangi na kuwa Kijivujivu na kumwekea Sime kwenye Magamba inavutwa kana kwamba anasumaku. Tatizo likabaki kwenye njia hipi nimsafirishe mpaka hapa mjini maana ni mkubwa sana na limkia lake ni refu sana. Ikabidi niwasiliane na mteja aje pori kufuata mwenyewe ikawa kuzungushana nimekaa pori zaidi ya Wiki tatu namsubiri mteja mpaka nikaona ni ujinga bora niondoke. Nilichojifunza huyu mdudu anamambo si kitoto.
 
Kumbe Polin wanapatkana tu kiuras bas mie kuna MTU aliniambia waga wanashuka tu kutoka angani
 
Back
Top Bottom