Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Mambo 5 Muhimu Ya Kuyajua Unapoingia Kwenye Mahusiano!
(1) Sio kazi ya Mwanaume kukuhudumia hivyo acha kabisa kumuambia matatizo yako mwanaume ambaye ndiyo unakutana naye. kama akikusaidia sawa, asipokusaidia basi vumilia, msome taratibu, angalia mambo mengine katika mahusiano na si kuhusu pesa.
(2) Acha kusikiliza stori za rafiki zako; Kwanza kuhusu namna wanavyopewa pesa na wapenzi wao. Wanawake wengi wanaotangaza kuhudumiwa hawahudumiwi, ni uongo. Ukisikia “Mimi mwanaume wangu hivi, mwanaume wangu vile” wengi ni uongo wanakupanikisha tu. Pili acha kuwasimulia marafiki zako kuhusu ubahili wa mapenzi wako. Kuwaambia kuwa hakujali na mambo kama hayo, kwakua wanataka kuonekana basi watakujaza upepo utamuacha kumbe nao hawapewi chochote.
(3) Mpime mwanaume wako kwa mambo madogo madogo; Kama vile, ukienda kwake anakupa nauli, labda akija kwako anakuja hata na mkate, labda ukiwa na shida anakusaidia, kujali hata kama ni kwa kidogo. Mkitoka out analipa au anakuachia wewe, kupima kama anakuomba pesa au hakupi ila haombi?
Hapa ndipo utajua kama mwanaume wako ni mbahili au la, kama vinauli anakupa, vivocha anakupa, mara moja moja akija kwako analeta mkate. Mara moja moja ukimuomba pesa ya saluni anakupa basi hana shida. Achana na mambo ya kulipa kodi, sijui kuhudumia ndugu zako, kukupa pesa yake ya mshahara, kukununulia nguo na vitu kama hivyo.
(4) Vijana wengi nao ndiyo wana tafuta maisha; Iko hivi, kijana ndiyo anatafuta maisha, kwanza hawana hela, lakini hata kama wanazo wana mambo yao yakutekeleza, hawezi kuhonga kijingajinga wakati hata ndoa bado. Wengi wanaohonga ni wazee na wameshajiwekeza.
(5) Hakuambii mambo yake, ni kweli hapaswi kukuambia kila kitu; Kabla ya mwanaume kumuambia mambo yake anapaswa kukuamini kwanza, akujue ni mtu wa namna gani, ukiingia kwenye mahusiano usitake kujua kila kitu kuhusu mali zake. Atakuona kama tapeli, hivyo usiulizie sana mali zake, subiri akuamini ndiyo aanze kukuuliza. Unapomsimulia shoga yako akakuambia kama hakuambii hakupendi si kweli, anatakiwa kukuamini kwanza ndiyo akuambie mambo yake.