Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 557
- 858
Zab 92:12-13 SUV
[12] Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. [13] Waliopandwa katika nyumba ya BWANA Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.
Inawezakana umejenga imani kuwa hakuna mtu anaweza kuwa mwenye haki katika dunia hii, sitahangaika kupingana na wewe, ninachohitaji unifuatilie katika ujumbe huu, mwisho utachagua ubaki na msimamo wako au uachane nao.
Tunapongumzia mtu mwenye haki, tunamzungumzia yule mtu anayeishi yale maisha yanayompendeza Mungu, mtu mwenye maadili ya ki-Mungu, mtu anayefuata sheria na mafundisho sahihi ya ki-Mungu.
Yapo mambo yanayomfanya mtu atambulike mbele za Mungu na mbele watu kuwa ni mwenye haki, watu ambao wanapatikana hapa hapa duniani na sio mbinguni.
Yafuatayo ni mambo yanayomtambulisha mwamini kuwa ni mtu mwenye haki wa MUNGU;
1. Kumcha Mungu, mtu anayemcha Mungu katika roho na kweli anatambua Mungu ni nani kwake, hapendi nini kwake na anapenda nini kwake, atakaa katika mstari huo akitambua ni wa kuhemishiwa maana yeye ni muumba wa vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
2. Kufanya matendo mema, huwezi kumkuta mwana wa Mungu kweli kweli anatenda dhambi, anaishi maisha ambayo ni machukizo mbele za Mungu, anawafanyia wengine mambo yasiyofaa, anawadhulumu wengine haki zao, na hana huruma kwa wengine. Ataepuka mambo yote mabaya mbele za Mungu na kuishi maisha matakatifu, maisha yanayompendeza Mungu.
4. Kufuata sheria za Mungu, hatupo chini ya sheria ila hatupaswi kuishi tunavyotaka wenyewe, hatupo huru kuishi maisha yeyote, japo tuna uhuru wa kufanya tunayotaka, yawe mazuri au mabaya. Tukichagua kuishi maisha yaliyo machukizo mbele za Mungu tunamkosea Mungu na hatuwezi kuitwa wenye haki wa Mungu. Mtu akitaka kumpendeza Mungu anapaswa kuishi sawasawa na neno lake, afanye yale Mungu anamwelekeza, anajiepusha na yale Mungu anamkataza.
5. Kuwa mwenye upendo na huruma, huitwi mwenye haki alafu hupendi watu wala huna huruma nao, huwezi kuangalia mambo yako mwenyewe alafu ukajiita mwenye haki, huwezi kukosa huruma ya kiutu kwa wenye dhambi ukaitwa mwenye haki. Kama vile Kristo alivyoagiza tuwahurumie wengine, mcha Mungu atakuwa mfano mzuri wa haya.
6. Kuwa mtu wa Imani, itashangaza kuitwa mwenye haki wa Mungu alafu ukawa huna imani, humwamini Mungu katika maisha yako, una tangatanga katika imani nyingi tena zingine za miungu, jambo ambalo linaondoa sifa njema kwa mtu yeyote anayesema amemwamini Yesu Kristo.
Mwenye imani thabiti anayo sifa ya kuitwa mwenye haki wa Mungu, anamwamini Mungu katika mazingira ambayo watu wengine wanapingana nayo kabisa, yeye anaweza kuona jambo la ki-Mungu na akabaki akisubiri kile Mungu ameahidi katika mazingira yaleyale.
Sifa hizi chache zinaonyesha vile mtu anaweza kuwa na vigezo vya kuitwa mwenye haki, sifa ambazo zinaweza zikawa kwa mtu yeyote atakayeamua kumwamini Yesu Kristo, mtu atakayeamua kuachana na imani potofu na kukaa katika imani sahihi.
Bila kujalisha tumezaliwa na wazazi wa namna gani, tunaweza tukaingia kwenye kundi la wenye haki, ikiwa tu tutakuwa na sifa nilizokutajia hapo juu, kwa sababu hatuwi wenye haki kwa kuzaliwa na wazazi wazuri na wenye uwezo mkubwa kifedha.
Yak 5:16 SUV
[16] Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Bidii tu mbele za Mungu haitoshi kama unaishi kwenye maisha yasiyompendeza yeye, ila mwenye haki, mtu mwenye imani, mtu aliyejitenga na maisha ya dhambi, maombi yake yanafaa sana mbele za MUNGU. Maana yake maombi yake yana matokeo makubwa sana.
Utachagua uwe kwenye kundi gani, ila nakushauri uwe kwenye kundi la wenye haki, kwa sababu huhitaji kutoa damu yeyote uwe kwenye kundi hili, kazi yako ni kuchukua hatua kuanza kuishi yale maisha anayoyataka Mungu kwako.
Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukaribisha kwenye kundi hili zuri la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, ni moja ya kundi linaloweza kukusaidia kumjua Mungu wako vizuri kupitia neno lake. Ukipenda hili wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.
Mwisho, nikukaribishe kwenye channel ya wasap kupata maarifa mbalimbali bonyeza link hii kujiunga=>>Samson Ernest | WhatsApp Channel
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana