Sikujua kama bado Watanzania tunaamini uchawi!
Mlienda kwa mganga na nyie ndio akafanikiwa "kunyofoka" kwa yule dada au?
Ni stori ndefu Gaijin...bt kifupi tu na sie tulimpandia hukohuko, otherwise bro alishapotea, na kuna picha majirani walimpiga jamaa katoka ofisini dem kamwambia aoshe vyombo, bro kachuchumaa anaosha vyombo, inasikitisha sana
Mnajua watu wengine mnafeli mitihani kirahisi kweli..
Anajua mapato yote(sina vyanzo vingi kivile!). Na matumizi yote yanayozidi tzs 100,000 (mara nyingi namshirikisha kwa taarifa au uamuzi) lakini hata kama akitaka kujua mapato na matumizi yote mpaka shilingi moja bado anayo acess na record zangu (generally narecord kila kinachoingia na kutoka kila siku!)SMU
Hivi mwanadani wako anajua mapato yako yote na vipi yanatumika
* Nikijitazama bill yangu ya viatu asiione kamwe maana anaweza zimia.
Anajua mapato yote(sina vyanzo vingi kivile!). Na matumizi yote yanayozidi tzs 100,000 (mara nyingi namshirikisha kwa taarifa au uamuzi) lakini hata kama akitaka kujua mapato na matumizi yote mpaka shilingi moja bado anayo acess na record zangu (generally narecord kila kinachoingia na kutoka kila siku!)
Heheh samahani najua hili la uchungu kwako lakini limenichesha sana!
Na kilichonichekesha ni ile watu kuona mtu anaosha vyombo ni kupotea......
Kweli binaadamu tunafoutiana.
Ila pia hongereni kwa kumuokoa bro wenu
Asante...nashukuru Mungu nimeweza kujidiscipline vizuri...mwazo nilikuwa najaribu kufanya mwisho wa mwezi lakini nikawa najikuta vitu vingi nakuwa nimesahau na hivyo kushindwa kubalance mapato, matumizi na pesa iliyopo mkononi/benki...lakini baade nikajilazimisha kufanya kila siku, na nimefanikiwa kufanya hivyo kwa miaka kadhaa sasa. Utaratibu huu umenisaidia sana kujua ni sehemu gani pesa inatumika zaidi na kufanya marekebisho kwa kadri ninavyoweza.Hongera kwa kuwa muwazi na kuwa organized vya kutosha kuweza kuweka record ya matumizi.
Ni njia moja nzuri sana ya kuhakikisha huendi nje ya uwezo wako, na rahisi kupaona pa kubana matumizi ikihitajika kufanya hivyo
Anyway inachekesha bt its so painful to ma bro...na ukiacha matusi anayoyarusha kwa yule dada mwingine, na mengineyo, ndo nahoji kwanini wadada wanakuwa na roho za kishetani hivi, mbona wanaume wapo wengi tu. Kwani we Gaijin huamini uchawi?
Hususan ikiwa hukujua kuwa upo kwenye mtihani na mtoa mtihani anakuchanganya hujui mambo matano au sita!
1. Ulevi/matumizi ya madawa ya kulevya,ni kero na uwezekano wa kuwa responsible unapungua. Ni tatizo sana kwangu, labda sababu situmii kilevi cha aina yeyote, hasameheki kabisa.Jaribu kuangalia mambo haya sita na uyapange kwa uzito wake wa kusameheka - yaani namba 1 likiwa ni zito kabisa kusameheka hadi 6 jepesi zaidi kusameheka. Yaani lile la kwa 1 kimsingi linaweza kabisa kuvunja uhusiano (definitely) na lile la 6 laweza kushtua au kutikisa kidogo (most probably) lakini linaweza likapita katika historia na watu wakadumu. Ukipenda unaweza ukaelezea kwanini namba zako zivyo hivyo vilivyo.
Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
Unaweza kupanga yote 6 au kupanga makubwa matatu (your top three). Siji kama wanaume na wanawake tunashindwa kusamehe vitu vile vile au la.
MMM
6. Violence, kama anawapiga wa mtaani mie hayanihusu kabisa, ila kwetu akina tata mwanamke kupigwa na mpenzi ni part ya mapenzi jamani.
1. Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
(hili halina mjadala-Halikubaliki)
2. Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
(hili nalo vile vile-Halikubaliki)
3. Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
(Hili atafikishwa na polisi pia, sheria za nchi zichukue mkondo wake)
4. Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
(Hili I will try kumsaidia kidogo, ikishindikana basi)
5. Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
(Hii ni non-factor as far as si extreme. Wazazi wake wanampenda na nitawachukulia tu kama watu wazima, na ku deal nao)
6. Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
(Hili halinikeri hata kidogo. Namshauri atafute wakili wa kumtunzia will yake tu, akifa mali yende kwa nani)
1.Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine
Hapa wala hamna majadiliano...leo unaletewa mtoto kesho ngoma.Sijui nayo atasubiri mpa ikule ndo akwambie umgonjwa!!?
2.Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating)
Nampakia vitu vyake ...namsindikiza mpaka nje alafu namtakia maisha mema huko kwa kimada.
3.Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
Kofi moja la shavu when things are heated is forgiveable...kipigo cha kuniachia makovu/kunipa manundu HAPANA.
4.Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva
Kama hasaidiki kwenye swala zima la kuacha basi inabidi tuagane maana itakua kero kwangu.Besides...sitaki mtoto wa mtu anifie mikononi kwa madawa ya kulevya.
5.Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts
Well kama tulikubaliana kushirikishana kila kitu hapo ni imani yangu kwake itashuka maana sitojua kama kuna mengine ananificha.I mean sihitaji kujua ana ngapi maana sio zangu ni zake ila nikijua tu kwamba ana acc NBC...CRDB na Benki ya Posta inatosha.Kama hatukukubaliana hivyo haitonisumbua.
6.Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
Hili dogo sana na linatatulika kwahiyo halihitaji kusamehe wala kutokusamehe.