Mambo 6 yasiyoweza kusameheka kirahisi katika ndoa/mahusiano

@Mzee Madoshi. I feel you. Hata mie nashangaa sana "mtoto wa nje" kuwa namba wani, wakati mie naona ni faida tu wakiletwa na mie nikawalea. Au weye ni bagheshi ndo kuwa hawajali haya mambo.
 
Mzee Mwanakijiji imetosha baba tufumbulie basi fumbo hili. Naona wote tu wakosaji,hatujamwelewa mtoa maswali yamkini yeye hajalenga katika majibu yote yaliyotolewa.Kwani umesema "ulitarajia kutoa maswali matano sasa kumbe umetoa sita ? Na hivyo ndivyo waalimu huwafelisha wanafunzi" Wengi wamejibu maswali sita huu ni ukosaji wa kutozingatia maelekezo ya mtoa maswali!!
 

Kwangu mimi...

Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion)
Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence)
Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts

...............................
 
Inaonekana suala la "mtoto wa nje" limekuwa katika top 3 za watu wengi sana... labda tuulize kwanini kama mambo yote ni mazuri katika familia lakini hili limetokea mtu yuko tayari kuvunja ndoa? Na hili ni muhimu kwenye level tatu...

a. Labda wanawake wanaona kama mume alienda nje huko kuna uwezekano akapata watoto, na siri kubwa hapa iko ni kwamba mara nyingi mume akizaa nje hakuna dalili ya mwili kwake so wanaume wanaweza siyo tu kuzaa nje lakini hata kulea watoto huko kwingine bila mke kujua. Mara nyingi hili limekuwa likiumbuliwa sana kwenye misiba... ndipo watoto "mnakutana".. Na wapo wanawake ambao wanalichukulia hili kama sehemu ya maisha ya wanaume... hivyo naona wapo wanawake ambao hili likitokea linaweza kutetemesha nyumba bila kuivunja.

b. Sijui ni kwa kiasi gani kwa upande mwingine mwanamme kulea mimba ambayo anajua si yake. Fikiria kwa mfano, ulikuwa safari ya muda mrefu na unaporudi unakuta mwenzako ana mimba - hii ni rahisi kujua kuwa mimba si yako na hivyo kuwa na uchaguzi wa kuendelea na mwenzako au hata kumlazimisha abortion au kuachana naye. Je katika mazingira hayo mwanamme anaweza kukubali ujauzito huo kwa sababu ya mapenzi yake kwa mke wake?

c. Hili la level ya tatu nitaanzishia mada kuamkia kesho kwa sababu litagusa mahali fulani very delicate na "penyewe" hasa...
 
mi naweza samehe yote inategemea tu nimejulishwa wakati gani na je nimegundua mwenyewe au amenitubu kwangu mwenyewe na sababu za yeye kufanya alichofanya ila kitu sitakaa nisamehe ni dharua kwangu

mimi ni

Cheating........kwani ndiyo ianyoleta mtoto wa nje
Undisclosed accounts
Intrusion ya wakwe na hii wakati mwingine inafanyika bila hata wao kujua kuwa wanaingilia ; mathalani kumwita kikao cha siri nyumbani mwanenu hata kama mna nia njema lazima mtajenga picha mbaya kwa mwenzie

Kukiri kosa ndio raha ya msamaha....................na si kusameheana tu pasipokujua unasamehe kitu gani na athatri ni kubwa kiasi gani; mfano; cheati mwenzi atakuomba msamaha kumbe cheating ameifanya na mtu wako wa karibu................ama cheating hiyo imezaaa matunda yaani kuna mtoto amepatikana au ujauzito ambapo wewe huambiwi wakati uombwapo msamaha.......................tusameheane kwa hekima
 
Si mpaka huyo kimada akubali umchukue mtoto wake wa mwaka mmoja umlee wewe. Haya mambo ni more complicated than you think.

God forbid; hata mimi mtoto wa nje atakuwa ni kikomo cha ndoa yangu.


Hizo bold nyengine ni utata; yani unataka kuiba upendo wa mtoto kwa mamaye (mwanamke mwenzio) ufaidike na nini? Jiweke kwenye position ya mwenye mtoto. Hakuna mtu mwenye haki ya kuiba umama wa mwenzie bana hata awe mgumba.

 
Hivi mnavyosema hamuwezi samehe mtoto wa nje inamaanisha ukiletewa huyo mtoto utadai talaka au utatimua mtoto?
 

Kwangu mie hilo ndio naona gumu, kuna wakwe wanaweza kukufanya ukaiona ndoa chungu. Unaanzia wapi kuwafukuza wazazi wa mumeo au kuwapuga marufuku kufika kwenu?
 
Kwa mie siwezi hata kujua nita react vipi maana hiyo kwangu itakuwa shock ya century.

Ila kwa sasa nikiongelea kinadharia tu; ntadai talaka basi. Simchukii mtoto nachukia process nzima ilomleta mtoto duniani (cheating) na kwa kuwa kuna mtoto maanake hata nikisamehe sitasahau kamwe kwani the kid is there to remind me.

Hivi mnavyosema hamuwezi samehe mtoto wa nje inamaanisha ukiletewa huyo mtoto utadai talaka au utatimua mtoto?
 

Pole mzee Madoshi...sio nia ya yeyote hapa kuwafanya watoto ambao ni wa nje wajisikie vibaya au kuonyesha hawafai ila ni kwamba tu watu hawakubaliani na wakati/pia namna waliyokuja duniani maana mahusiano yao yanakua yameingiliwa. Sioni kama ni haki kumtaka mtu aliyedanganywa na mtu aliyempenda na kumwamini akubali tu kwamba mwenzake amemdanganya na ushahidi aupokee na kuupenda kama hawezi. We huoni kwamba ni bora mtu akachagua kuondoka badala ya kubaki alafu akupokee huku akiwa amejawa na chuki dhidi yako?Ndo mwanzo wa manyanyaso hao ujue (japo sio wote wanafanya hivyo ila wapo)...wanatabasamu na kusema nimesamehe mkaribishe mtoto nyumbani alafu adhabu ya wazazi wako unapewa wewe.

Kujibu maswali yako....Mtoto wa nje ni mtoto kama mwingine ila sio lazima awe na nafasi nzuri kwa mama aliyedanganywa sawa na watoto wa huyo mama....given the circumstances.

Anayo haki....sidhani kama kuna mtu ameshauri ''mtoto wa nje'' azuiwe asiwafahamu ndugu zake wengine, maana hata huyo mama mwenyewe nyumba akiamua kuondoka haina maana atawaficha hao wengine.

Sio yeye na ndio maana hamna anaesema anawachukia, ila huyo mtoto anakua kumbukumbu ya kudumu ya kilichotokea mpaka yeye kuja duniani. Kwahiyo mtu anapokimbia mahusiano yake anaikimbia hiyo kumbukumbu kwasababu hawezi kuishi nayo.

Heheheheh....hicho ni kisingizio cha wengi wanaotoka kwenye mahusiano yao ila ukweli ni kwamba asilimia kubwa udhaifu upo kwa yule anaetoka nje kwa kushindwa kumweka mwenzake sawa kama ndio tatizo, kwa kuikosea heshima ndoa na mwenzi wake n.k.
 
Hivi mnavyosema hamuwezi samehe mtoto wa nje inamaanisha ukiletewa huyo mtoto utadai talaka au utatimua mtoto?

Kila mtu anafanya kadiri anavyoweza.
Mtu akiamua kwamba anaweza kusamehe na kuendelea na mahusiano yake anaweza kumpokea mtoto au kufanya mtoto asiishi pale (which is the best thing to do in my opinion...kwa wote)....yani sioni kwanini mama mtu atataka kuja kumdump mtoto wake kwa mama wa kambo wakati aliamua mwenyewe kuwa nae na anaweza kumuangalia. Swala la matunzo baba anaweza kuwa anapeleka na kumuona mtoto huko huko....na kama umri wake unaruhusu nae anakuja kusalimia kwa muda mfupi.

Asiyeweza kusamehe anaondoka!!!Kumfukuza mtoto hakubadilishi chochote...
 

Kimada/affair nje ya uhusiano (extramarital affair/cheating) - 2
Akaunti za siri (mipango isiyomshirikisha mwenza) - undisclosed accounts - 6
Mtoto wa nje/mtoto wa bwana mwingine - 1
Kupiga au kumuumiza mtu kwa kipigo (domestic violence) - 4
Ulevi/Matumizi ya madawa ya kuleva - 3
Kuingiliwa na wakwe (in-laws intrusion) - 5

 
Kuna mtu kadokeza kuwa wengi ambao wanasema "yote yanasameheka" ni kuwa hawajawahi kuingia kwenye hizi issue!
 
Asante kwa ku share ilo dokezo maana nilkuwa naumiza kichwa na kujiuliza hawa wanaosamehe yote wametokea dunia hii hii au Jupiter. Kumbe ni suala la ideal na real (theory na practice)

Kuna mtu kadokeza kuwa wengi ambao wanasema "yote yanasameheka" ni kuwa hawajawahi kuingia kwenye hizi issue!
 
mkuu mmm umesahau
...kunyimana unyumba hili nalo kusameheka ni ngumu zaidi ya hayo 6..na ndilo linachangia wengi kuyafwata hayo 6 ulioweka.wengi wamekuwa wakiteseka kawaida na kufikiria soln ni kunyimana unyumba la hasha utaletewa mwenza si mda mrefu na mgongo wa sita tunalala kama kawaida
pepo mchafu toka na isiwe hii kwako unaesoma ;wish you ndoa njema yenye misukosuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…