PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,102
- 1,919
Wasalaam,
Ikiwa ni kipindi cha kutafuta wadhamini kwa Wagombea urais, wala siyo kipindi cha kampeni, wagombea urais wanajaribu tu kuongea yale matamanio yao maana hawaruhusiwi kunadi ilani zao, ila utakuta watu wanasema, wapinzani wanamshambulia Magufuli wala hawasemi watafanya wakishinda uchunguzi, ni kujifariji kwamba hamuelewi kinachozungumzwa na wapinzani wa Magufuli. Hapa nimekuwekea Mambo 6 yanayoonekana kwa mgombea urais Tundu Lisu mpaka sasa.
1. Maneno yake yanapoza roho za wastaafu wengi viongozi kutambuliwa juhudi zao, wanavumilia mengi Ila roho zao zinaumizwa pale inapoonekana hawakufanya kitu wakati ndio waliomwinua mheshimiwa.
2. Maneno ya TL yanaumiza sana vyombo vya habari visivyomtendea haki kwa kuogopa serikali, ujue ukweli huwa unaumiza roho ila inabaki kugugumia moyoni, najua hata media zinatamani Lissu ashinde vipate kupumua.
3. Maneno ya Lissu na siasa zake zimeibua watu wapya waliokuwa wameachana na siasa, Ila CCM imeelekeza vijana wake kujibu mapigo harakaharaka huku mitandaoni kuziba au kuzuia upepo wa Tundu Lissu.
4. Siasa za Lissu zinawagusa moja kwa moja wapenda haki wote. Hawa ukiwauliza nani wanapenda awe Rais watakwambia Lissu, ila watasema hatoweza kulingana na siasa za Magufuli na CCM, kwamba Lissu ataishia kuwatamanisha ila hatopewa nchi.
5. Lissu anasikilizwa sana na wanadiplomasia wengi nchini ikiwemo mabalozi wetu, pamoja na kuwa wao ni sehemu ya serikali, ila huko waliko mambo wanayoyaona nchi zile nitofauti kabisa na Mambo yaliyo nchini mwao.
6. Siasa za Lissu zinawagusa watu wote hata kama hajawahi kujenga hata hospitali moja nchini, kumnyanyapaa mtu unayemlisha haifanyi akuheshimu.
Hayo ni baadhi tu Mambo machache niliyoyaona na yanayowafanya wapinzani wake Lissu kuzidi kumshambulia kwa kejeli ali khari akizidi kujizolea umaalufu mkubwa kuliko wakati wowote.
Lisu akishinda ni furaha kwa wote, ila Magufuri akishinda, vijana hasa wanachuo watalia maana atakuwa na hasira zaidi kwa watakaoonyesha mapenzi ya wazi kwa wapinzani, kutukanwa na kusimangwa itakuwa sehemu ya maisha yao, huo ndo uhalisia japo maendeleo ya miundombinu yanazidi kuonekana.