Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
1. Pep Guardiola alipohojiwa akasema kati ya wachezaji anaowakubali basi mshambuliaji raia wa Uingereza Peter Crouch ni mmoja kati ya wachezaji anaowakubali sana. Akaenda mbali zaidi kwa kusema anamkubali mshambuliaji huyo kwa kuwa katika mipira 100 ya juu basi mipira 85 ataituliza mwilini mwake.
2. Kiukweli Kocha Guardiola katika historia yake ya kufundisha soka hakuanzia kufundisha Barca kama ambavyo watu wengi wanajuwa hilo. Guardiola alishafundisha klabu ya Al Ahli ya nchini Qatar mpaka nwaka 2005, lakini Guardiola ameshafundisha pia klabu ya Mexico ya Dirados de Sinaloa.
3. Katika zurura yake akiwa kama kocha, Pep Guardiola amekuwa na wasaidizi tofauti. Lakini kuna mtu mmoja amekuwa nae saana kwenye harakati zake za kufundisha kabumbu. Lakini mtu huyu hana historia na soka. Mtu huyu yeye ni mtaalam wa kucheza na maji. Manuel Estiarte ameshashiriki michezo ya Olympic mara 6 na ni mtaalam sana kwenye sekta hio, kiasi kwamba amepachikwa jina la Maradina wa kwenye Maji. Na Katika olympic ameshabeba medali ya dhahabu.
4. Huyu bwana kustahafu kwake Soka kulikuwa ni kwa kushtukiza sana. Ilikuwa ni mwezi April siku 1 mchana, Pep alikutana na Raisi wa Barcelona kipindi hicho bwana Joan Gaspart na kumwambia kuwa anataka kuondoka. Raisi huyo kwa mshtuko akabaki mdomo wazi na kisha akamuuliza ‘lini?’ Hatimae Pep akafungua kinywa na kumwambia ‘sasa hivi’. Joan Gaspart mara kadhaa amekiri kuwa mchana ule na kikao kile na Guardiola ni vitu ambavyo hawezi kuvisahau maishani mwake.
5. Guardiola mbali na kuwa kocha, jamaa pia ni muandishi mzuri sana wa vitabu. Na ana machapisho kadhaa ya vitabu ameshayaweka sokoni na yanapatikana kwenye maktaba mbalimbali ulimwenguni.
6. Ubingwa pekee ambao anaukumbuka na kuuheshimu katika maisha yake ya soka ni ule wa timu ya watoto ya Barcelona maarufu kama La Masia ambao aliunyakuwa mwaka 2008. Guardiola anauita ubingwa ule kama ubingwa wa faraja katika historia ya maisha yake. Na anamuheshimu mchezo yeyote alieshiriki kikamilifu kuupata ubingwa ule wa timu za watoto nchini Hispania.
7. Lakini kikubwa ambacho amekifanikisha hivi karibuni, ni kitendo chake cha kutopata ushindi katika mechi 6 mfululizo. Pep mpaka sasa amesha fundisha mechi 424, na katika mechi hizo hakuwahi kutopata ushindi katika mechi 6 mfululizo.
Hii ina eleza wazi kuwa kocha huyu amekwama na anatakiwa kubadili mbinu, mifumo na falsafa zake.
Mambo 7 yanayo muhusu Guardiola…linalo muandama sasa halijawahi kumtokea maishani mwake…