KIMOMWEMOTORS
JF-Expert Member
- May 17, 2018
- 358
- 675
SIku hizi ni rahisi sana kununua gari, pia ni rahisi kujua kuendesha, lakini ni ngumu kujua nini kinafanya gari yako ifanye kazi. Usijali, tuko hapa kuendelea kufahamisha mambo mbali mbali ambapo leo tutazungumzia kwa ufupi kuhusu mambo 8 ambayo hupaswi kuyachukulia poa katika gari yako.
1. Oil ya injini
Wengi hudhani oil ina kazi ya kuunguza mafuta, ukweli ni kua ina kazi ya kulainisha , kupooza na kusafisha injini, hivyo basi kama hakutakua na oil ya kutosha kwenye injini yako huweza kupelekea kujitengeneza kwa carbon, joto kupanda na mwishowe vyuma vya injini yako kusuguana. Hatimae gari yako inaweza kudhuru au kuua vitu kama Cylinder Walls, Bearings, rings n.k ambavyo vikidhurika sana huweza kudhuru injini yako kabisa. Hivyo kwa sababu ya umuhim wa oil, umakini wa kuipima kila mara unahitajika sana ili kukuwezesha kuilinda injini yako na kutolazimika kuingi gharama kubwa zaidi.
2. Tairi ya Dharula
Hili halikuwekwa kwenye gari yako kama urembo, lipo hapo kukusaidia kutoka sehem moja kwenda nyingine pindi unapopatwa na dharula. Kwa hiyo ni muhimu kufaham Jack, Spana tairi yako ya dharulla vinakaa wapi ili uvipate kwa urahisi pindi unapopatwa na dharula. Kila uanzapo safari, ni muhimu sana kuhakikisha kama tairi hiyo in upepo wa kutosha kwani uzoefu unaonesha kua mara nyingine hupungua upepo taratibu na kumalizika kabisa.
3. Wepa ya mbele na nyuma
Umesha wahi kuendesha gari yako kweyemvua na wepa zako zikawa hazifanyi kazi? Hizi wepa ni viambatanisho muhimu katika gari zetu na hatutakiwi kuzichukulia poa kwa kua hutumika mara chache. Unatakiwa kuhakikisha ziko vizuri, zinafanya kazi kwa uhakika na ule mpira wake uko kwenye ubora unaotakiwa kuweza kukusaidia kusafisha kioo chako ili uweze kuona barabara kwa urahisi. Iwap itatokea kioo chako kikawa na vumbi, manyunyu kidogo yakipita ukawasha wepa zako ambazo raba yake imekwisha, kioo chako kitakua kichafu maradufu na wakati mwingine kwa sababu ya raba zake kumalizika pia huweza kuchuna kioo chako.
4. Vimiminika mbali mbali katika gari yako
Hapa tunaongelea eneo jingine muhimu sana ambapo vitu hivi vikishirikiana huweza kuifanya gari yakokufany kazi kwa ustadi na ufanisi mzuri hivyo kukuepushia gharama zisizo za lazima. Dereva au Mmiliki wa gari unatakiwa kuchukulia kwa uzito vimiminika hivyo kwenye gari yako kama vile
a). Oil ya Injini,
b) . Dawa ya kukinga injini yako na kutu (Coolant)
c). Mafuta ya kulainisha usukani wako
d). Maji ya Wepa
e). Oil ya Gia box na
f). Mafuta ya Brake
5. Kiwango cha upepo
Unaweza kudhani kiwango cha upepo katika tairi lako sio jambo la kuzingatia sana, hili ni kosa. Ni moja ya vitu muhimu vinavyokupa usalama katika gari yako. Upepo ukiwa mdogo huweza kusababisha msuguano na lami mwishowe tairi huweza kupasuka, hivyo unashauriwa usitembelee tairi yako ikiwa na upepo mdogo kwa kua inaweza kupasuka na kudhuru watumiaji wa chombo husika.
6. Chujio la hewa
Kwa wastani sisi tulio wengi hua tunaamini kulipiga upepo lile chujio la hewa kila tunapofanya service ni njia nzuri ya kulisafisha, ila ukweli ni kua hilo chujio au maarufu kama Air Cleaner hutakiwa kubadirishwa kila baada ya miezi sita kabla ya ufanisi wake wa kuchuja vumbi haujaanza kupungua. Injini inapopata vumbi , huweza kuidhuru na kuifanya ifanye kazi yake kwa taabu jambo linaloweza kukuingiza gharama zaidi kwenye uendeshaji haswa upande wa mafuta.
7. Vifaa vya Dharula
Ni muhimu kua na vitu vidogo vidogo vya dharula kukusaidia kuchukua hatua za haraka pindi gari yako inapopata dharula ambayo hukuitarajia njiani. Vifaa hivyo ni kama vile, kisanduku cha huduma ya kwanza (First Aid Kit), Mtungi wa Zima Moto (Fire Extinguisher), Pembe Tatu (Triangles), Kipimio cha upepo (Tire Gauge), Dumu dogo la mafuta, Maji ya Kunywa haswa kwa wale wa safari ndefu, Betri ya ziada na wire ya kuboost pia ni muhim.
8. Brake
Hatutakiwi kuzembea brake katika vyombo vyetu vya usafiri pindi tunapoona hali zisizo za kawaida barabarani. Unapoendesha, fuatilia kwa umakini na ukaribu iwapo ukikanyaga brake usukani wako unastuka kidogo. Iwapo kuna mstuko katika usukani wako hiyo dalili sio njema sana, na unaweza kuathiri uimara wa gari yako barabarani pamoja na mfumo wa brake (Anti-Lock Braking System-ABS)
Kwa leo ni hayo tu machache, tutendelea kujuzana masuala mbali mbali yahusuyo magari ambayo tungependa wenzetu ambao hawayajui kabisa waweze kupata mawazo yatakayowasaidia katika kufanya uchaguzi sahihi wa vyombo hivyo na kuvitunza pia ili thamani ya pesa isipotee