Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Biashara ya utoaji wa huduma za mikopo kwa ajili ya ukarabati na maboresho ya nyumba ni moja ya njia za kujenga utajiri kupitia uwekezaji huu.
Hii sio njia ya moja kwa moja ya kuwekeza kwenye ardhi na majengo. Njia hii inahitaji uwe na maarifa sahihi na taarifa sahihi za uwekezaji kwenye ardhi na majengo ili ujenge mafanikio makubwa.
Leo ninashirikisha mambo nane (8) muhimu ya kuzingatia kwenye biashara ya mikopo kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za kupangisha.
Mambo 8 Ya Kuzingatia Kwenye Biashara Ya Mikopo Ya Ukarabati.
Moja.
Tathmini hali ya soko la nyumba za kupangisha.
Kila mtaa unakuwa na hali ya kipekee ya soko la nyumba za kupangisha. Mtaa "A" unaweza kuwa na hali mbaya ya soko la nyumba za kupangisha hata kama mtaa "B" ambao upo karibu na mtaa "A" una hali nzuri.
Hali nzuri ya soko la nyumba za kupangisha ni kiashiria kizuri cha kujenga mafanikio kupitia utoaji wa mikopo ya ukarabati wa nyumba.
Unapotoa mikopo wakati mzunguko wa soko mahalia unaanza kushuka ni vigumu sana kupata mafanikio makubwa kupitia utoaji wa mikopo kwa wamiliki wa nyumba za kupangisha.
Mbili.
Andaa mikataba mizuri.
Mkataba unatakiwa kuandaliwa na wakili mzoefu kwa kushirikiana na kocha au menta wako.
Kazi ya wakili itakuwa ni kuandaa mkataba ambao utakuwa na suluhisho bora wakati wa chanagamoto zitakapotokea.
Kocha/menta kazi yake ni kuhakikisha mkataba unakusaidia kutengeneza kiasi kikubwa cha kipato endelevu kila mwezi.
Tatu.
Kuweka shabaha kwenye nyumba za kipato chanya.
Unatakiwa kutoa mikopo kwenye nyumba ambazo huingiza kipato chanya kwa kila mwezi. Nyumba ambazo haziwezi kupata wapangaji bora kwa zaidi ya miezi kumi (10) kila mwezi zinaweza zisiwe chaguo lako.
Ingawa kiasi unachotoa ndicho huamua nyumba ambayo inaweza kurejesha mkopo kwa wakati husika au kutorejesha.
Nyumba zinazoingiza zaidi ya 2% ya bei ya nyumba kama kipato ghafi hufaa zaidi kupewa huduma za mikopo ukilinganisha na nyumba zenye kipato kidogo.
Nyumba zinazoingiza chini 1% ya bei ya nyumba kama kipato halisi nazo hizi hufaa kwa kupewa mikopo ya ukarabati.
Nne.
Toa malighafi na vifaa, sio fedha.
Ni muhimu kutoa vifaa na malighafi ya ukarabati na maboresho ya nyumba badala ya kutoa fedha. Hii itapunguza uzembe wa wakopaji kutumia mkopo wa ukarabati kwenye mambo mengine ya matumizi binafsi.
Jambo hili ni muhimu haijalishi mwenye nyumba ni mwaminifu au sio mwaminifu. Hutakiwi kumpa fedha mkopaji, badala yake mpe kila kitu anachohitaji kwa ajili ukarabati wa nyumba yake ya kupangisha.
Fedha zote za mafundi zitoke kwenye akaunti maalumu siku ya kuwalipa mafundi ya ukarabati wa nyumba. Mkopo asipewe mkononi mwenye nyumba kwa ajili ya kuwalipa mafundi ukarabati wa nyumba.
Tano.
Usitoe faini bila sababu za msingi.
Faini ya ucheleweshwaji wa marejesho inatakiwa kutolewa kwa umakini sana. Kama mwenye nyumba ana historia ya uaminifu, unatakiwa kubadilisha kiasi cha marejesho ya kila mwezi.
Usimtoze faini. Faini itozwe kwa wateja ambao wameonyesha usumbufu wa kukusudia. Hii itakuongezea jina zuri la biashara bila kupunguza kiasi cha faida unayotakiwa kutengeneza.
Sita.
Usimamizi mzuri wa nyumba za kupangisha.
Hali nzuri ya soko la nyumba za kupangisha haiwezi kukusaidia endapo kuna usimamizi mbovu wa nyumba za kupangisha.
Mkataba mzuri hauwezi kukusaidia endapo nyumba ya kupangisha inasimamiwa vibaya. Mwenye nyumba hataona manufaa makubwa ya kupewa huduma za mikopo endapo hakuna usimamizi mzuri wa nyumba za kupangisha.
Usimamizi wa nyumba ndiyo unaoweza kuamua kiasi cha kodi unachoweza kuanza kutengeneza kwenye nyumba za kupangisha.
Saba.
Toa mikopo haraka na riba nafuu.
Hakikisha humcheleweshi mwenye nyumba kuanza kupangisha nyumba iliyofanyiwa ukarabati na maboresho. Kuchelewa kwa mwezi mmoja, unamwingiza kiasi kikubwa cha hasara.
Hasara hii inatokana na ucheleweshwaji wa utoaji wa huduma zako za mikopo kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za kupangisha.
Kuwa mkweli wakati wa utoaji wa huduma za mikopo kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za kupangisha. Kama umeishiwa mtaji fedha, unakuwa muwazi kwa wateja wako.
Unapochelewa kutoa mikopo kwa wenye nyumba, unajichelewesha kukusanya kodi kama marejesho ya mkopo.
Usikubali uwe nyuma ya muda bila sababu za msingi. Unapotoa mikopo unatakiwa kuwa haraka ili mwenye nyumba aendelee kuingiza wapangaji bora kwenye nyumba yake.
Kwa kufanya hivi, mtaji fedha wako utakuwa unakua haraka zaidi na utakuwa unatumia kiasi kidogo cha usimamizi wa kampuni yako ya mikopo.
Nane.
Weka shabaha kwenye nyumba zenye kipato chanya.
Nyumba yenye kipato chanya ndiyo kigezo kikuu cha kutoa mikopo na sio mwenye nyumba mwenye uwezo mkubwa wa kifedha.
Mwenye nyumba ambaye hajiwezi kifedha lakini anamiliki nyumba yenye kuingiza kiasi kikubwa cha kodi anastahili kupewa mkopo kuliko mwenye nyumba anayemiliki nyumba ambayo haina kipato chanya.
Mafanikio yako yamejengwa kwenye utoaji wa mikopo kwa ajili ya ukarabati na maboresho ya nyumba ambazo zinaingiza kiasi kikubwa cha kipato (kodi) chanya kila mwezi.
Unapotoa mikopo kwa wenye nyumba ambao wana uwezo mkubwa wa kifedha lakini wanamiliki nyumba zisizokuwa na kipato chanya hupelekea kutoka nje ya malengo ya kampuni.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
WhatsApp; +255 752 413 711