RGforever
JF-Expert Member
- Apr 3, 2011
- 6,878
- 5,432
Mambo ambayo hayafai katika Katiba ya Nchi
Kuna vikundi mbalimbali vimejitokeza nchini vinavyowashawishi wananchi kutoa Maoni yao kulingana na Maslahi yao Binafsi. Vikundi hivyo vinawashawish watoe Maoni bila kujali maslahi ya Watanzania wote ila Yao binafsi na watu wao. Wanajaribu kuleta Ubaguzi na Kuvunja haki za kibinadamu.
Watanzania kwa Ujumla tulikemee hili kwa Nguvu zetu zote bila kuona uwoga wowote ule wa viongozi hao na wananchi wao katika Mchakato wa Katiba Mpya
TUKEMEE YAFUATAYO AMBAYO HAYANA TIJA KWA WATANZANIA
UDINI
Kamwe watanzania wenzangu tusikubali nchi yetu iongozwe kwa Matakwa ya Udini,iwe ukristo,uislam,upagani n.k... Katika katiba Mpya Nchi hii ibaki bila kuwa Na Dini.. Bali Dini iwe maamuzi ya mtu binafsi bila kubugudhi/kuathiri uhuru wa mtu Mwingine yoyote yule...ambaye ni tofauti na Imani yako
MAHAKAMA ZA KIDINI
Kuna Vikundi vinaamasisha watu, kuwa katika katiba mpya kuwepo na Mahakama za Dini ambazo zitagharamiwa kwa kodi za mtanzania. Ndugu zangu kamwe usikubali hili... Mahakama za kidini hazina Maslahi kwa Mtu ambaye si wenye Dini husika. Ni kwa maslah ya Dini yenyewe. Katiba ya Nchi hii ni kwa Maslahi ya wote si ya watu fulani. Mahakama hizo zitakuwa zinahusika na Mambo ya Kidini.
Je! Kwa mtu ambaye hana Dini kodi yake ikalipe viongozi wa kwenye Mahakama hizo???. Ni kitu ambacho hakiwezekani hata siku Moja. Tulikemee kwa Nguvu zote watu wa katiba Mpya wakija
KUWE NA UHURU na HAKI
Katika hili niweke msisitizo kabisa. MTANZANIA yoyote yule awe na uhuru wa Kufanya Atakavyo ili mradi asivunje Katiba na Sheria za nchi husika...
Imetokea kuwa kuna Sheria inayowakataza Watanzania Wengine Kuchinja na Kuuza Bidhaa za Nyama kwa Jamii,bali anayetakiwa kuchinja ni Mwislam pekee[mfano mzur ni katika machinjio mbalimbali hapa nchini] na ikitokea hivyo amefanya hivyo anakamatwa na Polisi... Huku ni kuweka Nchi katika tabaka la Udini na kuona wengine hawana Maana.. Kwahiyo katika Katiba Mpya tukemee hili na Mtu yeyote yule awe MWISLAM,MKRISTO, MPAGANI awe huru na MALI YAKE mwenyewe na kufanya atakavyo
MADARAKA KIDINI
Kumetokea Watu wanaotaka madaraka kulingana na Dini zao.. Kwamba Rais akiwa Dini X mwaka huu Basi Mwakani awe Dini Y au Z.. Na iwe hivyo kuanzia Juu mpaka yule wa chini kabisa. Mf Mwalimu mkuu akiwa dini X basi mwl.mkuu msaidizi awe dini Y,daktar,Nesi,n.k bila kujali elimu zao. Kamwe kwenye katiba Mpya kupigwe Marufuku watu kumchagua Mtu kwa sababu ya Dini yake. Bali achaguliwe kulingana na Sifa zake na Uwezo wake na Kwa kura za Watanzania
Pia Mtu yeyote yule aliye na sifa za Uongozi Mtanzania kutoka sehemu yeyote ile awe na haki ya kikatiba kugombea Uongozi
ADHABU YA KIFO
Katika katiba mpya, mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa Mujibu wa Sheria na Angetakiwa kupata adhabu ya kifo hasiuawe Bali Afungwe kifungo cha MAISHA pekee
SHULE ZA SERIKALI
Katika katiba Mpya Shule zote za Serikali ziweke Utaratibu wa Sare kwa Ajili ya Wanafunzi wote na zifuatwe. Kamwe Shule za Serikali zenye michanganyiko za Dini mbali mbali Pasiwe na Sare tofauti kwa wanafunzi.. Kuwe na Sare inayotambulika shule husika.
HABARI ZA UOCHOCHEZI/KUVUNJA AMANI
Si kitu cha kushangaza Watanzania wa Leo kupata habari kwa urahisi zaidi. Lakini je! Habari hizo zinaukweli ndani yake??. Na je anayezitoa Amefanya Research?....Mfano mzuri ni Kuhusu Idadi ya Watu, Matamko ya uchochezi,Kutukana Viongozi Waliopita,Kutukana Bunge n.k n.k. Katika Katiba Mpya Tukemee Habari ambazo hazina ukweli ndani yake na hakuna Research iliyofanyika[NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK] na Vyombo hivyo vipewe Onyo na kama Vikikaidi basi vifungiwe
ASANTENI
KATIBA MPYA KWA WATANZANIA WOTE