Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Mwenza wako anakupuuza sana pale ambapo unakuwa unajirahisisha sana kwake, unajitutumua sana ili kumfurahisha, unahatarisha uhai wako ili uthibitishe kwamba wewe ni husband material/wife material.
Mwenza wako anapata kiburi , majivuno, jeuri na dharau ya kukupuuza na kukuona tambara la deki pale ambapo anakufokea, anakujibu vibaya, hakusikilizi, anakudhalilisha, anaakushambulia kwa maneno makali sana- lakini anakuona unamuomba msamaha,unapiga magoti unatishia kujiua,unaanza kulia,unakopa fedha nyingi sana ili umpe akupende,unajinyima usingizi ili ajue ûnampenda sana,unapauka ,unakonda kwa ajili ya kumfurahisha yeye.
Je ufanye nini kama mwenza wako anakupuuza?
Njia za kukabiliana na mwenza mwenye dharau, kiburi, ujuaji,ambaye anakupuuza sana kwa makusudi
Njia zifuatazo zinafanya kazi kwa binadamu wote ulimwenguni na endapo utazitumia lazima upate HESHIMA popote.
1.Acha kumpa umuhimu wowote maishani mwako
Mpuuze ambaye anayekupuuza,jitenge naye ambaye amekutenga,acha kumpenda ambaye anaekuchukia,acha kutenga muda kwa ajili ya yule ambaye amekusahau,ambaye anakuona takataka muone takataka,anayekuja mzigo muone mzigo,anaekuona hauna pa kwenda acha kumtegemea kwa chochote,anaekudharau kaa naye mbali.
Watu wenye kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, ubishi, utemi, dharau, misimamo mikali,watu hawa UDHAIFU wao huwa wanataka kunyenyekewa sana,kuombwa msamaha,kupigiwa magoti,wanataka ugeuke mtumwa ili akupande kichwani,wanataka ulie ili wao wacheke,wanataka ujichukie ili wao wakuone kichekesho,wanataka udhalilike ili wao waonekane bora zaidi yako.
2.JIPENDE NA UJITHAMINI
Kama mwenza wako anakupuuza,anakudharau,anakuona mzigo, anakuona bwege,anakuona takataka,anakuona tabaka la chini anza kwa kufanya mabadiliko yafuatayo.
Wekeza 90% ya muda na fedha zako kwa ajili ya kuboresha maisha yako.
Kula vizuri, vaa vizuri, tumia manukato mazuri,tafuta usafiri kama uchumi unaruhusu, Badilisha kila kitu cha ndani , badili mpangilio wa vitu chumbani,nunua vitu vipya vya kufanya chumba chako kiwe chenye kupendeza.
-Fungua biashara,au tafuta kazi mpya,kama unaweza kujenga fanya hivyo,ukiweza kutembea sehemu za kifahari kama vile kujitoa "out" fanya hivyo.
-Kutana na marafiki wapya ambao haujawahi kuonana nao hapo awali.
wakati mwenza wako yupo busy na wanaume au wanawake wengine,tumia muda huo kuboresha maisha yako,kuwa mtu mpya,vaa nguo mpya,tumia simu mpya,badili mazingira ya chumbani kwako,jifunze vitu vipya.
Wakati huo utaokoa fedha zako na muda wako ambao ungepotea kwa kumnyenyekea, kuomba msamaha, kupiga magoti, kutishia kujiua, kutuma sms mfululizo, kupiga simu mfululizo.
Ukianza kupendeza sana wakati ambao mwenza wako amekuacha ghafla au anakupuuza sana litakuwa pigo kwake kwamba yeye hana faida yoyote wala hana umuhimu wowote maishani mwako.Hivyo yeye atajiona laana ya furaha na mafanikio yako tofauti na matarajio yake ya kukuaminisha kwamba hauwezi kuishi bila yeye.
3.FANYA UWEKEZAJI MKUBWA SANA KWAKO
Mwenza wako akija au akipata taarifa zako anatakiwa kujua kwamba maisha yako yanazidi kuwa bora kuliko kipindi yupo pamoja na wewe.
lakini kama ukifanya kinyume chake labda kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama, kumjengea, kusaidia ndugu zake,kumpa mtaji, kumchukulia mkopo n.k yeye atakuona bwege, atakuona haujielewi, atakuona tambara la deki kisha atatumia fedha zako kama adhabu kwako.
vilevile atakuwa na kiburi cha kukuacha kwa sababu anajua hana cha kupoteza.
Ukifanya uwekezaji mkubwa sana ili kuzuia mahusiano kuvunjika unakuwa unachimba kaburi lako wewe mwenyewe kwa sababu ya uwekezaji wako.
Mwenza wako akikuacha endapo utamuomba msamaha, utapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kupiga magoti, kutishia kujiua, kumbembeleza sana, kumnyenyekea,kumwambia hauwezi kuishi bila yeye,kuanza kulia moja kwa moja unamfanya awe na dharau, majivuno, kiburi,atakuwa jeuri,atakuwa haambiwi makosa,atakuwa haambiliki, anakuwa mjuaji sana,akifanya makosa makubwa sana atageuza kibao kwako kwa sababu anajua hauwezi kumuacha walahauwezi kuishi bila yeye,atafanya makosa lakini utaomba msamaha.
Mwenza wako ataacha kukuupuuza pale ambapo atagundua kwamba wanaume au wanawake wengi sana wanataka waingie maishani mwako.
Mwenza wako atakupuuza, atakuona takataka,atakudharau sana kama unaishi kwa kutegemea huruma yake,kama anajua hauna pa kwenda,kama anakuona umekonda sana, umepauka, unanuka, hauna kazi yoyote wala biashara yoyote,hauna furaha yoyote,upo na upweke kupitiliza atakuwa na uhakika kwamba hauwezi kuishi bila yeye, hauwezi kumuacha hata akifanya makosa makubwa sana.
Mwenza wako atakuthamini sana kama akiwa na hofu ya kukupoteza,hofu ya kukupoteza haiwezi kujengeka kama umepauka, unanuka, umekonda, haujiamini, unalia, unapiga simu mfululizo,unatuma sms mfululizo,unalalamika sana.