Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Wakuu Salaam,
Nitakuwa nilkileta hapa mfululizo wa mambo muhimu ambayo wenzetu katika nchi zilizopiga hatua huko Ulaya ya Magharibi tunaweza kupata la kujifunza. Kwa leo nitajikita kwenye angle ya usafirishaji.
Bila kupoteza muda na kukuchosha mpenzi msomaji naanza kuyataja mambo hayo kama ifuatavyo;
i) Barabara: Katika Highway nyingi, barabara zao zimejengwa kwa mfumo wa one way ambazo zinakuwa na lanes hadi kufikia 4. Vivyo hivyo kwa opposite side, kunakuwa na oney way ya magari ya kurudi yenye lanes kufikia hadi 4. Barabara inakuwa imetenganishwa katikakati kwa maana ya kwamba magari ya kwenda hayakutani na magari yanayorudi. Ndio maana kwa wenzetu ajali ni chache sana.
ii) Leseni ya udereva: Leseni hazitolewi kama Karanga. Utapata leseni kwa kuonesha kuwa umefaulu kwa nadharia na vitendo ukiwa barabarani. Udereva unaweza kujifunzia kwa private driving schools, ila mtihani utafanyika kupitia mamlaka za Serikali. Kumbuka kwa wenzetu wana zero tolerance kwenye rushwa. Kwahiyo hakuna masuala ya short cut ili upate Leseni.
iii) Fines kubwa kwa makosa ya barabarani: Sijasoma vizuri sheria ya usalama barabarani ya hapa nyumbani. Lakini, kwa harakaharaka kutokana na uzoefu wangu, naweza kusema hapa nyumbani ni miongoni mwa nchi ambazo madereva hawalipi fines za maana pale wanapofanya makosa kutokana na makosa wanayokuwa wamefanya kwa uzembe. Kule kwa wenzetu hawana mchezo pale dereva anapokamatwa kwa kosa la uzembe mfano kulewa, overspeeding, overtaking isiyozingatia sheria n.k.
iv) Magari kukaguliwa na mamlaka husika: Kila mwaka, magari yote yanatakiwa kukaguliwa kama yanakidhi vigezo vya kuwepo barabarani. Hivyo kila mwenye gari atatakiwa kupeleka gari lake sehemu husika na wataliangalia endapo linahitaji marekebisho au la. Endapo halifai, hautaruhusiwa kuliweka barabarani. Sasa ole wako uendeshe gari ambalo halijafanyiwa ukaguzi.. Fine yake utakusanya mishahara yako hata miezi miwili.
v) Usafiri wa umma kufuata ratiba maalumu: Hapa inahusisha zaidi Bus na Trains. Vyombo hivi hufuata ratiba ya kuondoka na kufika bila kujalisha kuna watu wangapi katika chombo hicho. Hata kama kuna mtu mmoja, muda ukifika chombo lazima kiondoke. Unakuta kila baada ya dakika 15 au nusu saa chombo kinaondoka. Na kinafika katika kila kituo kwa wakati na kuondoka kwa wakati. Japo changamoto chache hutokea kuvuruga ratiba, lakini kwa uzoefu wangu nimeshuhudia ratiba ikifuatwa kwa zaidi ya 90%. Kwa wenzetu katika mambo mengi ya umma ikiwamo usafiri yanaendeshwa kwa ubia kati ya Sekta binafsi na Serikali. Kwahiyo kampuni ikipata hasara pesa za walipakodi zinafidia gap la hasara na ndio maana haijalishi kuna watu wangapi lazima chombo kitembee.
vi) Usafirishaji wa Mizigo: Kampuni za kusafirisha mizigo zinatumia Apps ambazo mteja anaweza ku-track mwenendo wa mzigo wake. App inakueleza muda wa kuchukuliwa mzigo wako na muda wa kufika. Na mzigo unafika kwa wakati kama ilivyopangwa. Hivyo hauna haja ya kusumbuka, ni kucheki tu kwenye App kuwa mzigo wako umefika wapi na unafika muda gani nyumbani kwako. Hakuna haja ya kupiga simu mbilimbili kuulizia mzigo wako.
vii) Automated transport system: Wenzetu mambo yao mengi yapo automated. Mfano ukitaka kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine uta-search kwenye google au app ya usafiri na itakueleza usafiri gani utatumia na utatumia muda gani kufika mahala hapo. Hakuna haja ya kumuuliza mtu wala kupiga simu kwa mwenyeji wako. Mambo yote unayapata online. Mtu anakupa address yake tu, kisha mnakutana hapo kwake bila kuulizana maswali mengi hata kama haujawahi kufika sehemu hiyo. Ile app itakueleza kama utatumia Bus, Train au Tax aina gani na gharama ni kiasi gani. Unaona mambo yalivyo rahisi? Hapa kwetu mtu wa kutoka Muleba akifika Dar kwa mara ya kwanza na anataka kwenda Mbagala kwa mjomba wake ni lazima apige simu za kutosha na lazima aje kupokelewa kwa Magufuli. Bila hivyo ni lazima apotee.
Kwa sasa naomba nikomee hapo.
-------
Inaendelea
Wakuu,
Bila kupoteza muda wala kukuchosha ndugu msomaji naomba katika sehemu hii nijikite kwenye masuala ya kijamii kama ifuatavyo.
Kwanza, kwa wenzetu ni wajibu wa Serikali kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya huduma za kijamii. Serikali inajukumu la kusimamia ukusanyaji wa kodi na kutumia kodi hizo kwa kiwango cha juu sana kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma nzuri. Hivyo kwa wenzetu suala la kodi si la mchezo na kila mwananchi anayehusika lazima alipe kodi ipasavyo. Hali kadhalika, Serikali inatumia kodi za wananchi na kiwango cha rushwa, ufisadi na matumizi mengine ya ovyo ya pesa za umma haupo au pengine ukiwepo ni kwa kiwango cha chini sana.
Nitagusia masuala machache hapa:
Elimu: Kwa nchi karibia zote za Scandnavia (Sweden, Norway, Finland, Denmark) na nyinginezo, elimu katika Taasisi za umma ni bure kwa wazawa kuanzia Nursery mpaka Chuo Kikuu. Kwa nchi nyingine zimeweka ada ndogo ambayo ni very affordable kiasi kwamba mwanafunzi mwenyewe (mzawa) anaweza kujilipia hata kwa kufanya kazi ya vibarua. Ikumbukwe kuwa katika nchi zenye mfumo wa kulipia ada mfano katika level ya chuo kikuu mwanachuo anaweza kupata mkopo kwa silimia 100 bila kujalisha unasomea jambo gani.
Jambo la muhimu hapa ni kuwa, mazingira ya elimu katika Taasisi za umma ni mazuri kiwango cha juu sana. Mfano, chukulia mazingira ya Feza schools hapa Bongo ndio mazingira ya elimu katika Taasisi za umma ambako elimu inatolewa bure kabisa kwa wazawa. Ingekuwaje hapa Bongo kama mazingira ya shule za Feza ndio ingekuwa kiwango cha mazingira ya elimu kwa Shule za Serikali? Vipi tunaweza kufikia level hizo kwa shule hata za Kata hapa Bongo? Itakuwa mwaka gani?
Afya: Kama ilivyo kwa elimu, nchi nyingi za wenzetu huduma za afya zinatolewa bure au kwa gharama za chini sana. Kodi za wananchi zinahusika hapo. Suala la BIMA kwa nchi nyingi ni lazima wala si hiyari. Wenzetu hadi mbwa anakatiwa BIMA. Ukienda hospitali unapatiwa huduma zote hakuna haja ya kuletewa chakula na ndugu kama ilivyo Bongo. Kwahiyo hata ukikaa mwezi mzima hospitali bila kutembelewa na ndugu utapata huduma nzuri na mahitaji yote muhimu. Mazingira ya hospitali ni kama hotelini, unalala chumba chako na mazingira swaaaafi kabisa.