Mambo gani mtu anapaswa kufanya kabla ya kuacha kazi

Tobias nombo

New Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
2
Reaction score
1
Napenda kujua ni mambo gani mtu anapaswa kufanya kabla ya kuacha kazi kutoka kwa mwajiri wake? Kwa mtu anayetegemea kujiingiza katika ujasiriamali au biashara, afanye nini?
 
wakikujibu........nitag mkuu...........
 
Usiache kazi kabla hujajua nini unaenda kufanya mtaani,fanya kazi huku unashughulikia huo ujasiriamali muda ambao sio wa kazini,ukiona umeanza kupata faida inayokuridhisha hapo ndo utaamua mwenyewe uache kazi ufanye mambo yako,au ufanye mambo yako huku unaendelea na kazi
 

I agree
 
Asipofuata ushauri wako, atajuter...
 
Huyu anaamini kalamu 2 zilimshinda Fisi.
 
Acha kaz
Uone kazi
Kupata kazi


Usidanganywe na motivational speakers wa kibongo ambao 88% wameajiliwa.
Kuacha kazi ni swala la kibinafisi. Shida yenu mmeisha aminishwa kwamba no Job no Life.

Kwamba maisha yako kwenye kuajiriwa. Mbona sisi tumejiajiri na maisha yanaenda na tunapambana kufa na kupona?

Acha kuogopesha watu.
 
Huo muda mwingine nani anasimamia?

Shemeji?Mk?Binamu au Mdogo wako?

Biashara ikiwa changa inamuhitaji sana mwenye biashara
 
Jamani msiache kazi bila kuwa na kazi.

Nina shemeji yangu aliacha kazi miaka 4 iliyopita kwa kusikiliza haya mambo ya kilimo kinalipa sasa hivi yupo katika hali mbaya sn kimaisha
 
Jamani msiache kazi bila kuwa na kazi.

Nina shemeji yangu aliacha kazi miaka 4 iliyopita kwa kusikiliza haya mambo ya kilimo kinalipa sasa hivi yupo katika hali mbaya sn kimaisha
Hizi ndo news huwa zina Trade, Sikiliza kila mtu anasimama pekee yake.

Kwani huko Kazini kuna nini zaidi ya kufa na Tai shingoni?

Huwezi tolea mfano wa mtu mwingine kwa ajili ya mwingine.

Fulani alishindwa ni yeye, anapata shida ni yeye, biashara imemshinda ni yeye.

Yeye hawezi kuwa mwingine,

Hawezi tumika kama rejea.
 
Kwahiyo hutaki tuseme walioshindwa?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…