Mambo gani muhimu kumfundisha mtoto mchanga?

Mambo gani muhimu kumfundisha mtoto mchanga?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Hupaswi kusubiria hadi ajue kuongea ndipo uanze kumfundisha. Unaweza kuanza kumfundisha tokea akiwa na umri wa siku moja.

Miongoni mwa mambo ya kumzoesha mapema ni pamoja na:

1. Kunawa mikono kila anapojisaidia
Usbadilishie tu nguo, bali umnawishe na mikono ili ajue kuwa hilo tendo hufuatiwa na kunawa mikono. Hiyo tabia itajikita kwenye ufahamu wake na hivyo kuwa rahisi kuendelea nayo atakapojitambua

2. Kusali kabla ya kula
Kama imani yako inaelekeza kusali kabla ya kula, mzoeshe na yeye pia. Kila unapotaka kumnyonyesha umwambie msasali kwanza, na ufanye hivyo. Nafsi yake itadaka kinachofanyika na hivyo itakuja kuwa tabia yake atakapojitambua.

3. Kujisomea vitabu vizuri
Uwe na wakati wa kumsomea vitabu vizuri vya watoto kila siku. Ikiwa huna nafasi ya kufanya hivyo Mchana, hakikisha kuwa unafanya hivyo Usiku.

4. Kujitegemea
Kama nyumba ina nafasi ya kutosha, muhamishie kwenye chumba chake angali mdogo. Anaweza kulala kwenye chumba cha wazazi wake mwanzoni, labda miezi sita ya kwanza, lakini siyo kwenye kitanda kimoja na wazazi wake. Anapaswa kuwa na cha kwake.

Baadhi ya watu huwahamishia kwenye vyumba vyao kuanzia siku ya kwanza, lakini wengi wa wanaofanya hivyo hufunga kifaa cha "kummonitor" chumbani kwake.

Hayo ni baadhi ninayoamini ni ya muhimu mtoto kufundishwa tokea akiwa mchanga.

Mengineyo ni yapi?
 
Mtoto mdogo lakini anajua kuogelea.

 
Ni kweli wanawafanyia hayo watoto wadogo kiasi hicho?
 

Attachments

  • 8_day_old_Baby_Monet_s_First_Swim_in_the_Seal_Beach_Pool(240p).mp4
    1.1 MB
😄😄😄
 

Attachments

  • Baby_Monet_Swims_@_5_Days_Old_-_Her_first_BORN-TO-SWIM_EXPERIENCE__SmartFishAcademy.com(144p).mp4
    3.1 MB
Back
Top Bottom