Mambo gani ya kuzingatia wakati wa kununua gari?

RICH-HARD

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2016
Posts
346
Reaction score
337
Ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kununua Gari ya kutembelea?

Natanguliza shukrani
 
Siku zote hua Kuna mambo makuu matatu ya kuzingatia kama yafuatayo:-

1: Sababu ya kununua gari/gari kwa ajili ya nini?
Hapa lazima uangalie na uzingatie ni kwanini unataka kununua gari, inaweza kua ni kwa ajili ya kutembelea, kubebea mizigo na kadhalika.

2: Bajeti yako, hapa ni lazima ulinganishe na uchanganue gari inayaweza kufanya na kutimiza zile Sababu zilizofanya uwaze kununua gari na mfuko wako.

3: Gharama za uendeshaji, je kulingana na vyanzo vyako vya mapato utaweza kulihudumia gari unalotaka kulinunua?
Gari ni kama mke/mtoto, linahitaji matunzo na kulijali pia.

Ukizingatia hayo itakusaidia kuondokana na msongo wa mawazo kwa ajili ya kumiliki gari.
Kuna msemo "unasema kosea yote ila usikosee kuchagua mke", nafikiri gari ndio linafata hapo kwenye hiyo list baada ya mke.
 
Shukran mkuu
 
Back
Top Bottom