Mambo gani ya muhimu natakiwa nizingatie nikifungua barbershop?

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Nimekuwa na shauku ya kuanzisha barbershop, au saloon ya kiume hata ya kike naipenda nikipata msimamizi maana mimi sijui hayo mambo ila naogopa maana mambo ya kuwindana kama tuko paredi hapana.

Saloon ya kiume kuna jamaa ananiambia ni biashara nzuri kama utapata site na kinyozi mzuri sijawahi ifanya, nilikuwa nimejichanga changa hapa niko kama na Tsh 3M siwezi kuanzisha barbershop kwa mtaji huo?

Hata ya kike kama wazo linafaa naweza kupata abc ila nitajaribu lwa hii ya kike maana inaugumu wake yakiume simple kuisimamia hata nikiiga kunyoa sitachukua muda nimeelewa ila ya kike changamoto sana nasikia inalipa mno kuzidi ya kiume.

Maana wanawake wako lazi wale dagaa watoto wao ili hela nyingine akasukie.

Nipeni ushauri juu ya hili kama mada inavyojieleza na kichwa cha habari chajieleza barbershop natakiwa kuwa na mtaji wa kiasi gani sitaki yenye madoido mengi sana ila kwa wazo langu huu mtaji unanifaa au niendelee kujichanga changa.

Location napotaka kufungulia ni Katoro, ndio naona pako na heka heka sana kwenye miji inayokuja kwa kasi kibiashara.

Nakaribisha maoni nasoma comment
 
Milioni 3 haitoshi kufungua barbershop ,hiyo itatosha kijisaluni cha kawaida sana, barbershop hamna hamna uwe na milioni 10.
 
Babashopu pesa ndogo iyo Mkuu ila Muhimu weka Komoto(Superblack) Basi mchezo kwisha hata iyo 3M fungua ila weka huduma ya KOKOTO
 
Kwa mtaji wako na kwa mazingira uliyopo hiyo pesa unaweza kufungua saloon ya kawaida tu na sio barbershop. Kikubwa anza na huo huo mtaji lkn unakua unaboresha taratibu kadri unavyokua unapata pesa, hatimae unaweza kufikia lengo lako la kuwa na barbershop.

Tena kwa ushauri wangu ni vzr ukaanzia chini zaidi ili upate muda wa kuisoma biashara yenyewe( maana hujawahi ifanya) ili upante ABC
 
Asante kwa wazo hili
 
Changamoto kubwa ya hii biashara ni vinyozi. Aisee vinyozi wengi hawajielewi kbs, sijui sababu ni kutokwenda shule wengi wao??
Kama ikipendeza bora hata wewe mwenyewe ukajifunza huwezi jua mbeleni, kama usemavyo wengi wanatangatanga pia hawana msimamo wezi yaani kiufupi ukitaka upate hela yako kwenye hizi saloon kuwepo akinyoa chukua chako mapema kama barbershop kubwa ambavyo hufanya
 
Nimekuwa na shauku ya kuanzisha barbershop, au saloon ya kiume hata ya kike naipenda nikipata msimamizi maana mimi sijui hayo mambo ila naogopa maana mambo ya kuwindana kama tuko paredi hapana.

Saloon ya kiume kuna jamaa ananiambia ni biashara nzuri kama utapata site na kinyozi mzuri sijawahi ifanya, nilikuwa nimejichanga changa hapa niko kama na Tsh 3M siwezi kuanzisha barbershop kwa mtaji huo?

Hata ya kike kama wazo linafaa naweza kupata abc ila nitajaribu lwa hii ya kike maana inaugumu wake yakiume simple kuisimamia hata nikiiga kunyoa sitachukua muda nimeelewa ila ya kike changamoto sana nasikia inalipa mno kuzidi ya kiume.

Maana wanawake wako lazi wale dagaa watoto wao ili hela nyingine akasukie.

Nipeni ushauri juu ya hili kama mada inavyojieleza na kichwa cha habari chajieleza barbershop natakiwa kuwa na mtaji wa kiasi gani sitaki yenye madoido mengi sana ila kwa wazo langu huu mtaji unanifaa au niendelee kujichanga changa.

Location napotaka kufungulia ni Katoro, ndio naona pako na heka heka sana kwenye miji inayokuja kwa kasi kibiashara.

Nakaribisha maoni nasoma comment
3mil mbona ni viti 3 tu ? Salon uwe 15m hapo sawa...
 
Back
Top Bottom