Mambo gani yanayokukera huku Uswahilini kwetu na hasa kwenye nyumba za kupanga?

Uswahilini ukijielewa tu basi ushakuwa adui yao
 
Wadada kukaa kwenye vikorido na milango ya wapangaji wengine

Wadada kukaa karibu na toilet, Jambo linalotufanya watu tushindwe kutekeleza haja zetu huko machooni kwa raha mustarehe, yaan mtu inakubidi uingie toilet kwa target na ukiingia inakubidi ufungulie bomba la maji mpka mwisho ili wasisikie Mambo yaleeee.

Makelele ya wale wenye visabufa vya kichina, yaan jitu lnaweka maplay list yake nikama kaombwa kufanya hivyo kuwasikilizisha manyimbo yake siku kucha.

Uchafu vyooni na mabafuni

Umbea na kufuatilia maisha ya wapangaji wengine.
 
Kinachonikera uswahilini ni yale mambo ya kupangiana maisha. Yaani unakuta mtu huna amani, maisha yao ni ya kusemana kutwa kuvaliana sare za kusutana. Yaani hawabadilki
 
Ukibeba Chpsi vtoto vyao vinakodoa mimacho kama mijusi iliyobanwa na mlango wa Gereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…