Mambo Huisha,, Yawe mazuri hata kwa kiasi gani. Binadamu tukubali tu.

Mambo Huisha,, Yawe mazuri hata kwa kiasi gani. Binadamu tukubali tu.

Sonko Bibo

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2019
Posts
957
Reaction score
1,493
Jambo lolote lile zuri,
Unaloliona leo litafika mwisho tu.
Tukubaliane na hali ili maisha yendelee.

Wanaume tukubali tu.
So usiwekeze sana nguvu na mali kwa mwanamke wako hata kama unamuona mzuri na mrembo kiasi gani..
Wanawake msiweke akili zenu na kujikita sana kwenye kuhudumiwa intensively na huyo mwanaume wako ishi kawaida sana.
Tuchukuliane kwa ukawaida na sio kwa umalaika huu tunaotaka kila mmoja wetu awe nao kwenye maisha yetu..
Kila lenye mwanzo lina mwisho..

Kama ulikuwa na kipato kikubwa usifadhaike sana unapohit bottom,,
Maisha hayakudai chochote as long as tunapumua kikubwa jitihada ziwepo ila sio zile za kujiangamiza kisa unataka uwe juu..

Tuthaminiane kwa utu kwanza na sio uwezo wa pesa,,
Ukiona watu wanakuvalue kisa kile ulichonacho ujue kuwa hao ndio watu unapaswa kuwaepuka haraka sana..
Maana kama wanaokusifu na kukupamba ni wanawake basi jua tu kuwa hao wote ni malaya.
Na kama ni wanaume jua kuwa nao wana roho zile zile za kimalaya malaya tofauti tu ni kuwa wamezaliwa upande wa wanaume..
Ndio maana baadhi wameishia kuwa mashoga maana wana tamaa kubwa na mali za wanaume kama walivyo wanawake malaya.
Wazee msiwahubirie vijana wenu kuhusu umasikini uliopo nyumbani na kuwafanya wajihisi kuwa wao ndio sababu ya huo umasikini hivyo kwamba inawabidi wasome sana ili kuuondoa.
Kitu ambacho kinawafanya kuwa na msongo mkubwa wa mawazo wamalizapo chuo..
Yaani unakuta kijana amemaliza chuo halafu mara buuuumm!! Anataka apate kazi yenye mshahara milioni mbili kwa mwezi wakati yuko peke yake hana hata familia..
Anazikataa kazi za laki tatu na laki nne kuwa haimtoshi ilihali yuko single.

Sasa unajiuliza huyu kijana anawaza pesa nyingi hivi hayo matumizi makubwa ameyatolea wapi? Unakosa jibu.

Kumbe kakijana ka watu kamebebeshwa mzigo wa umasikini wa kwao kichwani na kuaminishwa kuwa ni lazima kauondoe.

Matokeo yake Taifa linazalisha watumishi wezi kuanzia ngazi ya Uraisi mpaka Mawaziri kushuka hadi kada za chini.
Taifa linakosa utashi na uadilifu kitu kinacholiua bara la Afrika..
Afrika wazazi tunapambanisha watoto wetu wakasome ili wawe wa kwanza darasani yaani ni ubinafsi tupu.
Kwani kuwa kwake wa kwanza kwenye mitihani kunalisaidiaje taifa kupiga hatua?
Tunaongozwa na Rika la wazee waliofeli kuliletea bara letu maendeleo wakabaki kusifu na kukimbilia kufanya starehe nchi za ulaya kwa mbwembwe.
Wazee wamewaambukiza vijana ulimbukeni na minyororo ya utumwa baada ya kufanikiwa kidogo wanakimbiza watoto wao kuwasomesha nje ya Afrika..
Halafu wanataka Afrika yenye maendeleo?
Afrika haiwezi kupta maendeleo kamwe kama watu wake hawatakuwa na Identity yao wenyewe.
Sasa vijana badala wakachukue maarifa nje walete barani kwetu wao wanaenda kubeba identity za nje na kuleta barani kwetu wakiyaacha maarifa..

Hata hivyo hawaoni umuhimu na ulazima wa hayo maarifa maana wao wanazitazama circle ndogo ndogo yaani familia zao ambapo wanaona zina maendeleo tayari so maarifa ya nini tena?
Wao wanabeba utamaduni tu mifumo batili ya maisha ndio wanaleta kwetu Afrika.

Tutambue kuwa haya mafanikio kwenye units ndogo ndogo yana mwisho maana hakuna mifumo endelevu ya pamoja.

Usishangae kama umejipambania ukatoka kimaisha halafu baada ya muda tu ukafilisika au wanao wakaishi maisha duni.
Tambua kuwa juhudi zako si kitu sana maana mifumo ndio shida haswa..
Wengi wanajitahidi ila wanaishia kwenye lindi la madeni makubwa ya mikopo isiyolipika..
Itoshe kusema japo ni ukweli mchungu na usiokubalika..
Kizazi cha miaka ya 60, 70, na 80 kimefeli na sasa watu hao wapo tayari kuona kizazi cha 90 na 2000 kikifeli zaidi bila kuwapatia miongozo mizuri.
Na hakika wote tutafeli na kuishia kwenye umasikini wa kunuka..
Tukiishia kuwaabudu matajiri wachache wahuni wahuni tena ambao ni viongozi wetu wanaokazana kuiba mali za nchi na kuuza sehemu za urithi wa vizazi vijavyo kwa maslahi yao peke yao ambayo nayo sio kwamba ni makubwa kiasi hicho..

Niishie kusema tu Kila kitu huja mwisho..
Tukubali na watawala inawapasa kukubali kuwa hata wao mambo yao yatafika mwisho siku moja..
Wasistaajabu sana siku meza za utawala zitakapogeuka
Hususani kule Uganda tunamuona mtu na mwanae wanakabidhiana kijiti gizani vivyo hivyo Rwanda..
Tanzania ya CCM ipoje kwani? Si ni machifu tu ndio wanapokezana vijiti na kuteuana watoto wao?....
 
wakikuelewa matajiri niko pale 🤓 👉👉
Wanatakiwa waelewe sio kunielewa,,
Mimi ni mjumbe tu nipitae sina nguvu wala ushawishi huo..
Ila uhalisia utabaki kuwahukumu watakaokuwepo kwa wakati husika..
 
20241025_225201.jpg
 
Back
Top Bottom